Thursday, September 25, 2014

LIVERPOOL YAKABIDHIWA KWA SWANSEA, MAN CITY NA NEWCASTLE, CHELSEA YAPATA VIBONDE RAUNDI YA NNE CAPTAL ONE

TIMU ya hadhi ya chini iliyobaki katika Kombe la Ligi, Shrewsbury Town, itamenyana na timu ya Ligi Kuu ya England, Chelsea katika raundi ya Nne ya michuano hiyo.
Timu hiyo ya Daraja la Pili, Shrews, ambayo imeitoa Norwich ya Daraja la Kwanza katika raundi iliyoalizika usiku huu, itakuwa mwenyeji wa The Blues iliyoichapa 2-1 Bolton usiku wa Jumatano.

RATIBA RAUNDI YA NNE KOMBE LA LIGI ENGLAND...
Tottenham Hotspur vs Brighton
Stoke vs Southampton
Bournemouth vs West Brom
Shrewsbury vs Chelsea
Liverpool vs Swansea
MK Dons vs Sheffield United
Manchester City vs Newcastle United
(Mechi zitachezwa wikiendi ya Oktoba 27, 2014

CPL: MATOKEO YA CHELSEA VS BOLTON HAYA HAPA

Wauawaji; Kurt Zouma kulai na Oscar kushoto wakishangilia

CHELSEA imesonga mbele Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One baada ya kuichapa mabao 2-1 kwa mbinde Bolton Wanderers Uwanja wa Stamfrod Bridge usiku huu. 
Beki Mfaransa, Kurt Zouma aliifungia timu ya Jose Mourinho bao la kwanza dakika ya 25 kabla ya Nahodha wa Bolton, Matt Mills kusawazisha dakika sita baadaye.
Sifa zimuendee Oscar aliyefunga bao la ushindi kwa The Blues kwa shuti la umbali wa mita 25 dakika ya 55.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Azpilicueta, Zouma, Cahill, Luis, Mikel, Ake/Matic dk90, Salah/Hazard dk79, Oscar, Schurrle na Remy/Drogba dk73.
Bolton: Lonergan, Herd, Mills, Dervite, Moxey, Feeney/Spearing dk68, Danns/Mason dk82, Pratley, Kamara, Davies/Lee dk52 na Beckford

ZILE BAO NNE ZA RONALDO ULIZIONA? CHEKI ALIVYOSHANGILIA KILA BAO

Baada ya kuingoza Real Madrid kufunga mabao 8-3 dhidi ya Derpotivo, Cristiano Ronaldo amefanya kufuru nyingine kwa kupachika mabao manne wakati Real Madrid ikiiangamiza Elche kwa mabao 5-1. Ronaldo amepiga hat trick ya pili, katika mechi chache tu na ameonyesha anastahili kuwa mchezaji bora wa dunia.
Ronaldo alifunga hayo manne huku mshambuliaji mwingine nyota, Gareth Bale ambaye ndiye ghali zaidi katika soka, akapiga moja.
Real Madrid: Navas, Marcelo, Carvajal, Varane, Ramos, Kroos, Rodríguez, Illarramendi, Bale, Isco, Ronaldo Subs: Casillas, Coentrão, Benzema, Hernández, Arbeloa, Nacho, Modric Booked: Carvajal, Marcelo Scorers: Bale 20', Ronaldo 28', 32', 80', 90' Elche: Yagüe, Gallego, Pelegrín, Lombán, Cisma, Romero, Corominas, Rodrigues, Mosquera, Morales, Cristian de Jesus Booked: Gallego Scorer: Gallego 15' Subs: Suárez, Roco, Herrera, Martín, Fajr, Pasalic, Tyton Ref: Carlos Clos Gómez At: 65,000.

Wednesday, September 24, 2014

ANGALIA NYUKI WALIVYOWATIMUA WACHEZAJI MTIBWA, CAMERAMAN WA AZAM TV

Nyuki bana, nao wana yao. Katika mechi ya Ligi Kuu Bara, Jumapili iliyopita wakati Mtibwa Sugar ikiivaa Yanga, waliwakimbiza wachezaji wa Mtibwa. Wachezaji hao walikuwa wanashangilia bao lililofungwa na mwenzao Mussa Hassan Mgosi, ghafla nyuki hao wakaibuka na wachezaji hao wakalazimika kutimua mbio.
Cameraman wa Azam FC na mwenzake, pia walilazimika kuacha kazi yao na kutimua mbio baada ya lundo hilo la nyuki kuungana nao wakati wakishangilia. Hata hivyo halikuwa tukio la muda mrefu, nyuki hao ‘walichukua za time’. Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara iliisha kwa Mtibwa Sugar kushinda kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri.

Picha na salehjembe

HII YAPA NDO SIKU MAALUM YA WACHEZAJI FRANK DOMAYO NA JOHN BOCCO WATAKAYO RUDI RASMI UWANJANI

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM KIUNGO Frank Domayo ataanza mazoezi mepesi Oktoba 1, mwaka huu baada ya kumaliza muda wa mapumziko kufuatia kufanyiwa upasuaji wa nyama za paja. Domayo aligundulika kuchanika vibaya nyama za paja, baada tu ya kusajiliwa na Azam FC Juni mwaka huu, kufuatia kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC. Kufuatia hali hiyo, alipelekwa Afrika Kusini alikofanyiwa opersheni na kutakiwa kupumzika kwa miezi mitatu- na sasa yuko tayari kuanza jaribio la kurejea uwanjani. “Nitaanza mazoezi tarehe moja, najisikia vizuri kabisa kwa sasa, kama mambo yatakwenda vizuri natarajia kuanza kucheza labda kuanzia mwishoni mwa mwa mwezi ujao,”amesema.
Aidha, winga Joseph Kimwaga akiyekwenda kufanyiwa upasuaji pamoja na Domayo, naye ameanza mazoezi mepesi tangu mwishoni mwa wiki. Kimwaga aliumia goti mwaka jana katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu baada ya kuibuka vizuri kikosi cha kwanza cha Azam kufuatia kupandishwa kutoka akademi. Amekuwa nje kwa muda wote akijaribu kutibiwa hapa nyumbani bila mafanikio kabla ya kupelekwa Afrika Kusini, naye sasa anajaribu kurudi tena uwanjani. Umaarufu wa Kimwaga ulikuja baada ya kuifungia Azam FC bao la tatu katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita. Kwa upande mwingine, mshambuliaji John Raphael Bocco aliyeumia katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya El Merreikh ya Sudan mwezi uliopita, naye anatarajiwa kuanza mazoezi mapema wiki ijayo. Tayari majeruhi mwingine wa muda mrefu wa Azam FC, Waziri Salum ameanza mazoezi tangu mwishoni mwa wiki.

HIKI NDO KILICHOIUA MAN UNITED DHIDI YA LECESTER

Hali imeonekana kuwa nzurio kutokana na Manchester United kuendelea kuboronga na safu yake ya ulinzi kuwa nyanya. Mechi iliyopita Man United imefungwa mabao 5-3 na Leicester City ikiwa ni bada ya kuongeza kwa mabao 3-1. Picha unayoiona, inaonyesha kiasi gani safu yake ya ulinzi inacheza shaghalabagala. Wachezaji hawakai katika sehemu zao. Angalia aliyewekewa namba 2, huyo ni Blackett ambaye ameamua kubaki nyuma peke yake bila ya kuangalia wenzake wamejipanga vipi. Ukiachana na hivyo, katika picha hiyo kuna wachezaji saba wa Man United na watatu tu wa Leicester City lakini bado waliweza kuleta madhara. Kitu kikubwa cha tatu, katika wachezaji saba wa Man United, hakuna hata mmoja aliyemkaba mchezaji mmoja tu kati ya watatu wa Leicester City. Hayo ndiyo sehemu ya madudu ya safu ya ulinzi ya Man United.

TERRY ATUMA JEZI YAKE YA MECHI KWA SHABIKI ALIYEFIWA NA MAMA YAKE

Nahodha wa Chelsea, John Terry ameisaini jezi yake ya mechi na kuituma kwa mmoja wa mashabiki wa Chelsea aliyefiwa na mama yake. Shabiki huyo alitumiwa ujumbe na Terry kupitia mtandao wa kijamii akimuambia kuwa amemtumia zawadi hiyo ya jezi kumfariji. Terry aliandika: Pole sana taarifa za majonzi kuwa mama yako amefariki dunia. Ningependa kutuma moja ya jezi zangu kwa ajili ya mechi na kuweka saini yangu ili ujue mimi na Chelsea tuko pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu. Baadaye shabiki huyo aitwaye Louise alituma kwenye Instagram akionyesha jezi hiyo baada ya kuipokea.

HIVI NDO JINSI ARSENAL ILIVONG'OLEWA KWENYE KOMBE LA LIGI NA SOUTHAMPTON UWANJA WA EMIRATES

LA LIGI ARSENAL imefungwa mabao 2-1 na Southamtpon katika Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Emirates. Alexis Sanchez alitangulia kuwafungia Gunners dakika ya 14 kwa mpira wa adhabu, kabla ya Dusan Tadic kusawazisha dakika sita baadaye kwa penalty, kufuatia Tomas Rosicky kumchezea rafu Sadio Mane. Nathaniel Clyne akaifungia Southampton bao la ushindi kwa shuti la umbali wa mita 30 dakika ya 40 katika mchezo ambao kiungo anayetoka kwenye majeruhi wa Arsenal, Abou Diaby alianza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tangu Machi 2013. Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Ospina, Bellerin/ Akpom dk86, Chambers, Hayden, Coquelin, Rosicky, Diaby/Cazorla dk67, Campbell/ Oxlade-Chamberlain dk71, Wilshere, Podolski na Sanchez. Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Gardos, Targett/Bertrand, Wanyama, Schneiderlin, Mane/Long dk72, Davis, Tadic na Pelle.

CPL: MATOKEO YA LIVERPOOL vs MIDDLESBROG HAYA HAPA

KLABU ya Liverpool imeifunga Middlesbrough kwa penalti 14-13 katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Anfield. Kinda Jordan Rossiter alianza kuwafungia Wekundu hao baada ya kupewa nafasi ya kwanza kuchezea kikosi cha kwanza, kabla ya Adam Reach kuwasawazishia wageni akimalizia pasi ya Grant Leadbitter. Mchezo huo ulihamia kwenye muda wa nyongeza kufuatia timu kumaliza zikiwa zimefungana 1-1 baada ya dakika 90. Suso akafunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na Liverpool kuwapatia bao la kuongoza Wekundu hao, lakini Kolo Toure akacheza rafu ndani ya boksi na Patrick Bamford akaenda kusawazisha dakika za lala salama na katika penalty Liverpool ikashinda 14-13 baada ya Albert Adomah kupoteza mkwaju wa Boro. Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Toure, Sakho, Enrique, Rossiter/ Williams dk79, Lucas, Sterling, Lallana, Markovic na Lambert/Balotelli dk74. Middlesbrough; Blackman, Fredericks, Ayala, Omeru, Friend, Adomah, Clayton, Leadbitter, Reach, Tomlin na Kike/Wildschut dk76.

Goodnews: Huyu ndio msanii staa wa kimataifa anaekuja Fiesta Dar 2014.

Wakati Tour ya Fiesta ikiwa inazunguka kwenye mikoa mbalimbali Tanzania ambapo weekend hii ni Mbeya na Songea, ametangazwa msanii wa kimataifa ambae ni rasmi atapanda kwenye stage ya Fiesta Dar es salaam October 2014 Leaders Club Kinondoni. Rapper T.I ndio msanii wa kimataifa kwenye stage ya Fiesta October 18 2014 akiwa ni mkali ambae kwa sasa anamiliki chati za muziki kwa single yake ya No Mediocre

Tuesday, September 23, 2014

UGOMVI WA MOURINHO, RONALDO WAWAMUIMIZA MASHABIKI URENO

Mashabiki wa soka nchini Ureno wamechangia kwenye mitandao mbalimbali wakionyesha kusikitishwa na ugomvi wa nyota wao wawili. Kocha Jose Mourinho wa Chelsea na mshambulia Cristiano Ronaldo wa Real Madrid wameeleza hadharani kuwa hawana urafiki tena. Mashabiki hao wa soka wameeleza wazi kusikitishwa na hali hiyo huku wakishindwa kugawanyika wampede nani. Baadhi wamesema Ureno yenye watu milioni 11 na nyota wachache wanaojulikana zaidi duniani kama hao wawili, hivyo hawakupaswa kuwa maadui. Kauli ya Mourinho kwamba walitolewa kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2012 baada ya Ronaldo kukosa penalti na limekuwa jambo ambalo linamuumiza kila mara ilioonyesha kumuudhi mshambuliaji huyo. Ronaldo alijibu mashambulizi kwa kusema hayuko katika soka kutafuta marafiki na hiyo ilikuwa baada ya kuulizwa kama uhusiano wake na Mourinho ni mzuri. Wawili hao walifanya kazi pamoja Real Madrid tokea mwaka 2010 hadi 2012 Mourinho alipoondoka na kwa mambo yanavyokwenda inaonekana uhusiano wao haupo. “Urafiki wetu haupo, ulishakufa, si lahisi kutuona tukiwa pamoja,” Mourinho aliiambia moja ya runinga marufu ya Ureno wakati akifanyiwa mahojiano.

Posted via Blogaway

YANGA SC WAPEWA SHARTI MOJA TU WAKITEKELEZA WANALAMBA MILIONI 155

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM YANGA SC wamepewa sharti moja tu na Bodi ya Ligi, ambalo wakitekeleza watapatiwa Sh. Milioni 155. Sharti gani hilo? Msimu uliopita Yanga SC walisusia fedha za haki ya matangazo ya Televisheni ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinazotolewa na Azam Media Limited kwa sababu wao walikuwa wanapinga kampuni hiyo kupewa Mkataba huo. Lakini jitihada zao za kuipinga Azam Media kurusha Ligi Kuu zilishindikana kutokana na ukweli kwamba walitoa ofa nzuri ambayo hakukuwa na kampuni iliyofikia hata nusu yake. Yanga SC wakajaribu kutaka kuzuia Azam kurusha mechi zao, hilo nalo likashindikana kwa kuwa ile si Ligi Kuu ya Yanga SC, ni Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayomilikiwa na waliosaini Mkataba na Azam Media Limited, TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) na Bodi ya Ligi. Ilikuwa rahisi wao kujiondoa kwenye Ligi wakacheze ligi ambayo haina Mkataba na Azam Media, kuliko kuizuia kampuni hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kutekeleza mkataba wao na TFF na bodi ya Ligi. Yanga SC wakagomea fedha za mgawo wa haki ya matangazo Sh. Milioni 100 za msimu uliopita, ambazo Azam Media walizikabidhi kwa bodi ya Ligi. Na bodi ya Ligi imezipeleka wapi fedha hizo? “Fedha za Yanga SC zipo, tumeziweka katika akaunti maalum, za msimu uliopita na msimu huu, wakizihitaji wakati wowote waziandikie barua ya kuziomba, tuwapatie,”amesema Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga. Maana yake- kama Yanga SC wanazihitaji fedha hizo wanaweza kuzipata ndani ya wiki moja- iwapo wataandika barua na fedha zitahamishiwa kwenye akaunti yao, au kupewa hundi moja kwa moja. Azam Media Limited waliingia Mkataba wa haki za matangazo ya Televisheni ya Ligi Kuu mwaka jana na TFF kwa pamoja na bodi ya ligi hiyo, wakitoa Sh. Milioni 100 kwa kila klabu, wakati mwaka huu kuna ongezeko la asilimia 10, na kufanya dau la Milioni 110. Tayari kwa msimu huu kila timu, kati ya 14 zilizopo kwenye ligi hiyo imekwishaptiwa Sh. Milioni 55, wakati Sh. Milioni 55 nyingine zitatolewa sambamba na mzuguko wa pili wa Ligi Kuu mapema mwakani.

Posted via Blogaway

Monday, September 22, 2014

KIBADENI AELEZA MZIMU WA MAFISANGO UNAVYOMSUMBUA OKWI

Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni, amesema mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, anateswa na mzimu wa marehemu, Patrick Mafisango kwa kuwa ndiye aliyekuwa akimchezesha. Okwi amesajiliwa na Simba katika dakika za mwisho lakini alikuwa hajaonyesha ubora wake kwenye mechi za kirafiki alizocheza kabla ya jana kuivaa Coastal. Kibadeni amesema Okwi anahitaji ajipange ipasavyo ili aweze kupata nafasi ya kucheza Simba na kumpata mtu wa kumchezesha kama ilivyokuwa kwa Mafisango ambaye ndiye aliyekuwa msaada mkubwa kwake. “Okwi ninayemjua mimi si huyu wa sasa kwani kiwango chake kimeshuka mno, hivyo anahitaji kujipanga ipasavyo kwa kuonyesha juhudi za hali ya juu ili aweze kupata nafasi katika kikosi cha kwanza. “Zamani wakati anaichezea timu hiyo alikuwa na mtu wa kumchezesha, marehemu Mafisango, hivyo kwa sasa anahitaji mtu mwingine aweze kumchezesha na kuwa katika kiwango kizuri kama cha awali,” alisema Kibadeni.

Posted via Blogaway

STRAIKA AS ROMA APIGA BAO, APANDA JUKWAANI KUMKUMBATIA BIBI YAKE

Mshambuliaji wa AS Roma ya Italia, Alessandro Florenzi amepiga bao na haraka akapanda jukwaani na kwenda kumkumbatia bibi mwenye umri wa miaka 82. Ilikuwa ni mechi kati ya AS roma dhidi ya Cagliari na wakashinda kwa mabao 2-0, yote yakiwa yamepigwa na mshambuliaji huyo. Mara baada ya kufunga mshambuliaji huyo alipanda kasi kwenda juu ya jukwaa na kumkumbatia bibi huyo. Huo ulikuwa ni ushindi mwingine wa AS Roma baada ya kuwa imeiadhibu kwa mabao 5-1 timu ya CSKA Moscow katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Posted via Blogaway

CHEKI PICHA KIBAO ZA KUMNANGA VAN GAAL BAADA YA MAN UNITED KUCHAPWA 5-3

BAADA YA MAN UNITED KUCHAPWA MABAO 5-3 YA LEICESTER ILIYOPANDA DARAJA LIGI ENGLAND, PICHA KIBAO ZA KUMBEZA KOCHA LOUIS VAN GAAL NA NYINGINE ZA VICHEKESHO KAMA HIZI. CHEKI HIZI HAPA NI BAADHI YAKE.

Posted via Blogaway

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI MBURULAA AVAA NGUO ZA AIBU

Fashion Police: Checkout What A Gospel Singer Wore To Church This Gospel singer was allowed to wear an outfit that exposes her body during a church service at the riverside church in New York. Apparently, the Pastor at the church didn't see anything wrong with the half naked gospel singerand so instead of advising her to wear something decent, he was rather clapping his hands to welcome her on stage.

Posted via Blogaway

GHARAMA ZA KUUNGANISHA UMEME WA MAJUMBANI BURE KUANZIA MWAKANI

Gharama za kuunganisha umeme wa majumbani zitatolewa bure kuanzia mwezi Machi mwakani baada ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, kukamilika kwa asilimia 90. Aidha gharama za matumizi ya umeme wa majumbani na viwandani zitapungua kwa kiasi kikubwa baada ya mtambo huo kuanza kufanyakazi. Msemaji Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, alisema hayo jana alipotembelea mtambo huo Kinyerezi akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa na Waandishi wa habari. Alisema kuwa gharama za watumiaji wa umeme kwa Tanzania ziko chini kwa asilimia tano ukilinganisha na nchi za Uganda (asilimia 24) na Burundi (asilimia 20). “Mtambo wa kusafirishia umeme wa gesi ambao ukubwa wake ni kama ule wa Ubungo umekamilika kwa asilimia 90. Alisema kuwa serikali imeajiri wafanyakazi Watanzania kwa asilimia 95, na ifikapo Januari vijana 60, watapelekwa nchini China kwa masomo ili wapate ujuzi wakuendesha mitambo hiyo. Mhandisi anayesimamia mradi huo, Saimoni Gilma, alisema mradi huo umetumia Dola za Marekani milioni 103, ambazo zote zimelipwa na Serikali ya Tanzania. Alisema ujenzi wa miundombinu ya mitambo hiyo umekamilika kinachosubiriwa ni kuletwa kwa mitambo hiyo kutoka bandarini. Aidha, nyumba za wafanyakazi, watakaoendesha mitambo hiyo zimekamilika kwa ajili ya kuanza kazi. Alifafanua kuwa mabomba ya gesi yaliotandazwa aridhini kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ni transfoma 200. Na yatawekewa ulinzi mkali ikiwa ni pamoja na ulinzi wa helikopta itakayokuwa inazunguka usiku na mchana. Alisema kuwa gharama za kuweka umeme majumbani zitagharamiwa na nchi ya Japan na Finland, wananchi watatakiwa kutoa sehemu ya viwanja vyao au mashamba ili kupisha bomba hilo kupita.

Posted via Blogaway

Diamond au Alikiba? Mr Blue aeleza yupi anayependa kufanya naye ngoma

Kihistoria, Diamond na Alikiba ni wadogo zake Mr Blue. Wakati Mr Blue anatamba na ngoma zake ikiwemo Mapozi, hakuna aliyekuwa akiwafahau wawili hao. Na kuna wakati Blue aliwahi kusimulia namna alivyokerwa na tabia ya Diamond ya kutembea na ex wake akiwe Wema na Najma. Hata Hivyo rapper huyo wa Pesa, amesema anawakubali wote Alikiba na Diamond na wote ni washkaji. “Unajua mie wale wote washkaji zangu nawala sina tatizo nao kwahiyo nipo tayari kufanya kazi na yeyote yule ambaye atakuwa tayari si unajua hii kazi na kazi mkishirikiana pamoja ndo inakuwa nzuri zaidi,” Blue ameiambia Bongo5. Akizungumzia kuhusu video, rapper huyo amesema anatarajia kutoa video mbili kwa pamoja.”Nimeshaulizwa sana kuhusu natoa video lini. Jibu sasa lipo tayari kwa mashabiki wangu. Nitaachia video mbili hivi karibuni na hizo video nimefanya zote na Adam Juma. Video ya Pesa ipo tayari na namalizia kushoot video ya Mapenzi pia kwahiyo muda wowote nitaziachia.” Kwa upande mwingine Kabasyer amesema kama akitaka kurudi shule basi atasomea tu muziki na utayarishaji.credit bongo5

Posted via Blogaway

ANGALIA PICHA YA MWANAMKE MMOJA ALIYENASWA AKIFANYA MAPENZI NA WANAUME WAWILI HUKO MBAGALA

Kijiji kilichogunduliwa Mbagala Zakhem, jijini Dar, wasichana na wavulana walinaswa wakifanya vitendo vya ngono kwenye moja ya mabanda ambayo yametengenezwa maalumu kwa shughuli hiyo. Operesheni hiyo ilifanywa na waandish kwa kushirikiana na jeshi la polisi Jumamosi iliyopita usiku ambapo ilifanikiwa kuwanasa baadhi ya vijana akiwemo mwanamke mmoja aliyekutwa akifanya ngono na wanaume wawili (walio pichani). Hata hivyo, kundi la watu kama wanane wakiwa na nguo mikononi walitimua mbio baada ya kuona polisi wamevamia chumba kimoja kilichotengenezwa kwa uzio wa vipande vya magunia chakavu na makaratasi walichokuwa wakikitumia kufanyia ngono. Aidha, wana usalama walifanikiwa kuwakamata watu watatu, wanaume wawili pamoja na mwanamke aliyejitambulisha kwa jina moja la Semeni waliyekuwa wakifanya naye mapenzi. Baada ya kuwatia mbaroni watu hao na kuwafanyia upekuzi, walikutwa na kondomo na vipisi vya bangi. Maafande walipomhoji Semeni alisema vijana hao walimlipa shilingi 5,000 kila mmoja na mmiliki wa eneo hilo aliyemtaja kwa jina moja la Babu walimlipa shilingi 2,000. Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, aliwapongeza polisi kwa kufanikiwa kuwakamata baadhi ya vijana hao. “Kwa kweli sehemu hii ni kama kijiji cha ngono maana hata wanafunzi huchukuliwa na kuingizwa kwenye vibanda hivi kwa ajili ya kufanya ufuska, tunashukuru kwa kuamua kukisambatisha,” alisema jamaa huyo aliyeomba hifadhi ya jina

Posted via Blogaway

WEMA SEPETU NA DIAMOND PLATNUMZ: DONDOO MUHIMU KUHUSU MAHUSIANO YAO

When the president wa wasafi classic meet his first lady wema sepetu kila kitu seems to go as planned and fans expectations huwa zipo high.Diamond seems to be well atleast when he is with Wema,and fans wa hawa celebrity hapa bongo huwa siku zoke hukaa mkao wa kula kusikilizia suprises zozote watakazotoka nazo.Kama unakumbuka walivyorudiana mara ya pili wakati haukupita waliweza ku-post on I.G (instagram) some private moment wakiwa pamoja,fans wengi hupenda hii couple.This is known to be most popular celeb couple of all time ambayo imeweza kutokea na ikitokea kuwa mambo yameenda kushoto kidogo,the news do tend to travel fast na huwa inatokea mlipuko wa habari kuhusu wawili hao when they do fall apart kitu ambacho ni sawa na pale wanapoamua kurudiana, huwa ni news ya wiki nzima hapa Bongo na kushangaza zaidi ni east africa nzima huwa inaongelea hii couple,hii inaongeza popularity kwao as celebs na hivyo hata mtu mgeni aliyeingia hapa TZ huwa yuko curious kuulizia about the life of this two Celebz and we all know that popularity means business these days. Jina la Diamond Platmuz mbali ya kuwa popular in music industry,limekuwa jina ambalo vijana wengi hapa nchini wamekuwa na mtu wakumuangalia na kila mtu kutaka kuwa kama yeye,the way anavyo dress,anavyo nyoa na hata pozz tu sawa na wema sepetu kila mtu amekuwa anamu-admire kwa jinsi tu alivyo especialy young ladies,unaweza kusema wawili hawa ndio moja ya most influencial couples wa hapa bongo,its like brad pit na Jolie wa hapa Bongo. They say Celeb couple huwa hawawezi kukaa katika relation muda mrefu,this is one of the reason Diamond and Wema ya ku-date ili waweze kuwa-prove wrong watu wengi wanaoamini huo msemo, mbali ya kuachana na na kurudiana mara kwa mara wawili hawa wamekuwa na drama zakutosha,as celebz they always do ila kwa hawa inaoneana kama bado mapenzi yao yapo pale pale no matter how many times they break up,the record says they are back together and its official now.

Posted via Blogaway