Monday, September 22, 2014



 |
Kijiji kilichogunduliwa Mbagala Zakhem, jijini
Dar, wasichana na wavulana walinaswa
wakifanya vitendo vya ngono kwenye moja ya
mabanda ambayo yametengenezwa maalumu
kwa shughuli hiyo.
Operesheni hiyo ilifanywa na waandish
kwa kushirikiana na jeshi la polisi Jumamosi
iliyopita usiku ambapo ilifanikiwa kuwanasa
baadhi ya vijana akiwemo mwanamke mmoja
aliyekutwa akifanya ngono na wanaume wawili
(walio pichani).
Hata hivyo, kundi la watu kama wanane
wakiwa na nguo mikononi walitimua mbio
baada ya kuona polisi wamevamia chumba
kimoja kilichotengenezwa kwa uzio wa vipande
vya magunia chakavu na makaratasi
walichokuwa wakikitumia kufanyia ngono.
Aidha, wana usalama walifanikiwa kuwakamata
watu watatu, wanaume wawili pamoja na
mwanamke aliyejitambulisha kwa jina moja la
Semeni waliyekuwa wakifanya naye mapenzi.
Baada ya kuwatia mbaroni watu hao na
kuwafanyia upekuzi, walikutwa na kondomo na
vipisi vya bangi.
Maafande walipomhoji Semeni alisema vijana
hao walimlipa shilingi 5,000 kila mmoja na
mmiliki wa eneo hilo aliyemtaja kwa jina moja
la Babu walimlipa shilingi 2,000.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo,
aliwapongeza polisi kwa kufanikiwa
kuwakamata baadhi ya vijana hao.
“Kwa kweli sehemu hii ni kama kijiji cha ngono
maana hata wanafunzi huchukuliwa na
kuingizwa kwenye vibanda hivi kwa ajili ya
kufanya ufuska, tunashukuru kwa kuamua
kukisambatisha,” alisema jamaa huyo
aliyeomba hifadhi ya jina |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment