Monday, September 22, 2014

STRAIKA AS ROMA APIGA BAO, APANDA JUKWAANI KUMKUMBATIA BIBI YAKE

Mshambuliaji wa AS Roma ya Italia, Alessandro Florenzi amepiga bao na haraka akapanda jukwaani na kwenda kumkumbatia bibi mwenye umri wa miaka 82. Ilikuwa ni mechi kati ya AS roma dhidi ya Cagliari na wakashinda kwa mabao 2-0, yote yakiwa yamepigwa na mshambuliaji huyo. Mara baada ya kufunga mshambuliaji huyo alipanda kasi kwenda juu ya jukwaa na kumkumbatia bibi huyo. Huo ulikuwa ni ushindi mwingine wa AS Roma baada ya kuwa imeiadhibu kwa mabao 5-1 timu ya CSKA Moscow katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Posted via Blogaway

0 comments:

Post a Comment