Wednesday, September 24, 2014
 |
Nyuki bana, nao wana yao.
Katika mechi ya Ligi Kuu
Bara, Jumapili iliyopita
wakati Mtibwa Sugar
ikiivaa Yanga,
waliwakimbiza wachezaji wa
Mtibwa.
Wachezaji hao walikuwa
wanashangilia bao
lililofungwa na mwenzao
Mussa Hassan Mgosi, ghafla
nyuki hao wakaibuka na
wachezaji hao wakalazimika
kutimua mbio. |
 |
Cameraman wa Azam FC na mwenzake, pia walilazimika kuacha kazi yao na kutimua mbio baada ya lundo hilo la nyuki kuungana nao wakati wakishangilia.
Hata hivyo halikuwa tukio la muda mrefu, nyuki hao ‘walichukua za time’.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara iliisha kwa Mtibwa Sugar kushinda kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri. |
Picha na salehjembe
0 comments:
Post a Comment