Monday, September 22, 2014
 |
Gharama za kuunganisha umeme wa
majumbani zitatolewa bure kuanzia mwezi
Machi mwakani baada ya ujenzi wa bomba
la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam,
kukamilika kwa asilimia 90.
Aidha gharama za matumizi ya umeme wa
majumbani na viwandani zitapungua
kwa kiasi kikubwa baada ya mtambo huo
kuanza kufanyakazi.
Msemaji Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini, alisema hayo jana alipotembelea
mtambo huo Kinyerezi akiwa na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es
Salaam, Ramadhani Madabida, Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya mkoa na Waandishi
wa habari.
Alisema kuwa gharama za watumiaji wa
umeme kwa Tanzania ziko chini kwa
asilimia tano ukilinganisha na nchi za
Uganda (asilimia 24) na Burundi (asilimia
20).
“Mtambo wa kusafirishia umeme wa gesi
ambao ukubwa wake ni kama ule wa
Ubungo umekamilika kwa asilimia 90.
Alisema kuwa serikali imeajiri
wafanyakazi Watanzania kwa asilimia 95,
na ifikapo Januari vijana 60, watapelekwa
nchini China kwa masomo ili wapate ujuzi
wakuendesha mitambo hiyo.
Mhandisi anayesimamia mradi huo,
Saimoni Gilma, alisema mradi huo
umetumia Dola za Marekani milioni 103,
ambazo zote zimelipwa na Serikali ya
Tanzania.
Alisema ujenzi wa miundombinu ya
mitambo hiyo umekamilika
kinachosubiriwa ni kuletwa kwa mitambo
hiyo kutoka bandarini.
Aidha, nyumba za wafanyakazi,
watakaoendesha mitambo hiyo
zimekamilika kwa ajili ya kuanza kazi.
Alifafanua kuwa mabomba ya gesi
yaliotandazwa aridhini kutoka Mtwara
hadi Dar es Salaam ni transfoma 200. Na
yatawekewa ulinzi mkali ikiwa ni pamoja
na ulinzi wa helikopta itakayokuwa
inazunguka usiku na mchana.
Alisema kuwa gharama za kuweka umeme
majumbani zitagharamiwa na nchi ya
Japan na Finland, wananchi watatakiwa
kutoa sehemu ya viwanja vyao au
mashamba ili kupisha bomba hilo kupita. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment