Wednesday, September 24, 2014
 |
KLABU ya Liverpool imeifunga
Middlesbrough kwa penalti 14-13 katika
Raundi ya Tatu ya Kombe la Ligi, maarufu
kama Capital One Cup kufuatia sare ya 2-2
ndani ya dakika 120 Uwanja wa Anfield.
Kinda Jordan Rossiter alianza kuwafungia
Wekundu hao baada ya kupewa nafasi ya
kwanza kuchezea kikosi cha kwanza, kabla
ya Adam Reach kuwasawazishia wageni
akimalizia pasi ya Grant Leadbitter.
Mchezo huo ulihamia kwenye muda wa
nyongeza kufuatia timu kumaliza zikiwa
zimefungana 1-1 baada ya dakika 90.
Suso akafunga bao lake la kwanza tangu
ajiunge na Liverpool kuwapatia bao la
kuongoza Wekundu hao, lakini Kolo Toure
akacheza rafu ndani ya boksi na Patrick
Bamford akaenda kusawazisha dakika za
lala salama na katika penalty Liverpool
ikashinda 14-13 baada ya Albert Adomah
kupoteza mkwaju wa Boro.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet,
Manquillo, Toure, Sakho, Enrique, Rossiter/
Williams dk79, Lucas, Sterling, Lallana,
Markovic na Lambert/Balotelli dk74.
Middlesbrough; Blackman, Fredericks, Ayala,
Omeru, Friend, Adomah, Clayton, Leadbitter,
Reach, Tomlin na Kike/Wildschut dk76. |

0 comments:
Post a Comment