Tuesday, September 23, 2014
|
Mashabiki wa soka nchini
Ureno wamechangia kwenye
mitandao mbalimbali
wakionyesha kusikitishwa na
ugomvi wa nyota wao wawili.
Kocha Jose Mourinho wa
Chelsea na mshambulia
Cristiano Ronaldo wa Real
Madrid wameeleza hadharani
kuwa hawana urafiki tena.
Mashabiki hao wa soka
wameeleza wazi kusikitishwa
na hali hiyo huku
wakishindwa kugawanyika
wampede nani.
Baadhi wamesema Ureno yenye
watu milioni 11 na nyota
wachache wanaojulikana
zaidi duniani kama hao
wawili, hivyo hawakupaswa
kuwa maadui.
Kauli ya Mourinho kwamba
walitolewa kwenye nusu
fainali ya Ligi ya Mabingwa
mwaka 2012 baada ya Ronaldo
kukosa penalti na limekuwa
jambo ambalo linamuumiza
kila mara ilioonyesha
kumuudhi mshambuliaji huyo.
Ronaldo alijibu
mashambulizi kwa kusema
hayuko katika soka kutafuta
marafiki na hiyo ilikuwa
baada ya kuulizwa kama
uhusiano wake na Mourinho
ni mzuri.
Wawili hao walifanya kazi
pamoja Real Madrid tokea
mwaka 2010 hadi 2012
Mourinho alipoondoka na kwa
mambo yanavyokwenda
inaonekana uhusiano wao
haupo.
“Urafiki wetu haupo,
ulishakufa, si lahisi
kutuona tukiwa pamoja,”
Mourinho aliiambia moja ya
runinga marufu ya Ureno
wakati akifanyiwa
mahojiano. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment