Wednesday, September 24, 2014
 |
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KIUNGO Frank Domayo ataanza mazoezi
mepesi Oktoba 1, mwaka huu baada ya
kumaliza muda wa mapumziko kufuatia
kufanyiwa upasuaji wa nyama za paja.
Domayo aligundulika kuchanika vibaya
nyama za paja, baada tu ya kusajiliwa na
Azam FC Juni mwaka huu, kufuatia kumaliza
Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC.
Kufuatia hali hiyo, alipelekwa Afrika Kusini
alikofanyiwa opersheni na kutakiwa
kupumzika kwa miezi mitatu- na sasa yuko
tayari kuanza jaribio la kurejea uwanjani.
“Nitaanza mazoezi tarehe moja, najisikia
vizuri kabisa kwa sasa, kama mambo
yatakwenda vizuri natarajia kuanza kucheza
labda kuanzia mwishoni mwa mwa mwezi
ujao,”amesema. |
 |
Aidha, winga Joseph Kimwaga akiyekwenda
kufanyiwa upasuaji pamoja na Domayo,
naye ameanza mazoezi mepesi tangu
mwishoni mwa wiki.
Kimwaga aliumia goti mwaka jana katika
mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu baada ya
kuibuka vizuri kikosi cha kwanza cha Azam
kufuatia kupandishwa kutoka akademi.
Amekuwa nje kwa muda wote akijaribu
kutibiwa hapa nyumbani bila mafanikio kabla
ya kupelekwa Afrika Kusini, naye sasa
anajaribu kurudi tena uwanjani.
Umaarufu wa Kimwaga ulikuja baada ya
kuifungia Azam FC bao la tatu katika ushindi
wa 3-2 dhidi ya Yanga SC katika mchezo
wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara msimu uliopita.
Kwa upande mwingine, mshambuliaji John
Raphael Bocco aliyeumia katika Robo Fainali
ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati
dhidi ya El Merreikh ya Sudan mwezi
uliopita, naye anatarajiwa kuanza mazoezi
mapema wiki ijayo.
Tayari majeruhi mwingine wa muda mrefu
wa Azam FC, Waziri Salum ameanza
mazoezi tangu mwishoni mwa wiki. |
0 comments:
Post a Comment