Wednesday, September 24, 2014
 |
LA LIGI
ARSENAL imefungwa mabao 2-1 na
Southamtpon katika Kombe la Ligi, maarufu
kama Capital One Cup usiku wa kuamkia leo
Uwanja wa Emirates.
Alexis Sanchez alitangulia kuwafungia
Gunners dakika ya 14 kwa mpira wa
adhabu, kabla ya Dusan Tadic kusawazisha
dakika sita baadaye kwa penalty, kufuatia
Tomas Rosicky kumchezea rafu Sadio
Mane.
Nathaniel Clyne akaifungia Southampton bao
la ushindi kwa shuti la umbali wa mita 30
dakika ya 40 katika mchezo ambao kiungo
anayetoka kwenye majeruhi wa Arsenal,
Abou Diaby alianza kwenye kikosi cha
kwanza kwa mara ya kwanza tangu Machi
2013.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Ospina, Bellerin/
Akpom dk86, Chambers, Hayden, Coquelin,
Rosicky, Diaby/Cazorla dk67, Campbell/
Oxlade-Chamberlain dk71, Wilshere, Podolski
na Sanchez.
Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Gardos,
Targett/Bertrand, Wanyama, Schneiderlin,
Mane/Long dk72, Davis, Tadic na Pelle. |
0 comments:
Post a Comment