Wednesday, September 24, 2014
 |
Nahodha wa Chelsea, John
Terry ameisaini jezi yake
ya mechi na kuituma kwa
mmoja wa mashabiki wa
Chelsea aliyefiwa na mama
yake.
Shabiki huyo alitumiwa
ujumbe na Terry kupitia
mtandao wa kijamii
akimuambia kuwa amemtumia
zawadi hiyo ya jezi
kumfariji.
Terry aliandika: Pole sana
taarifa za majonzi kuwa
mama yako amefariki dunia.
Ningependa kutuma moja ya
jezi zangu kwa ajili ya
mechi na kuweka saini
yangu ili ujue mimi na
Chelsea tuko pamoja nawe
katika kipindi hiki
kigumu.
Baadaye shabiki huyo
aitwaye Louise alituma
kwenye Instagram
akionyesha jezi hiyo baada
ya kuipokea. |
0 comments:
Post a Comment