Friday, September 05, 2014

Jipya kuhusu Young Killer kumbe alishatoa mahali kimya kimya baada ya kupewa kitisho hiki.

Rappa kutoka 88.1 Mwanza ambaye msimu wa Serengeti Fiesta 2012 ulifanikiwa kumuwakia na kuwa mshindi wa kwanza kwenye mashindano ya Serengeti Super Nyota Young Killer leo amehusishwa tukio la kutoa mahali kimya kimya bila kumfahamisha mtu. Mezani kwa Soudy Brown,Young Killer ameulizwa kuhusu madai hayo ambayo inasemekana mzazi wa msichana anayetajwa kuishi nae Halimaty alimwambia Young Killer kuwa kama asipotoa mahali atampiga ‘Allah Badili’ Young Killer alipopigiwa na Soudy Brown kadai yuko kwenye ndege anajiandaa kwenda Musoma kwenye Serengeti Fiesta hivyo ametakiwa kuzima simu na kuahidi atampigia baadae simu Soudy Brown.source millardayo

Posted via Blogaway

RONALDINHO APATA MKATABA MPYA BAADA YA KUBWAGA MANYANGA ATLETICO MINEIRO

MWANASOKA bora wa zamani wa dunia, Ronaldinho Gaucho amepewa ofa ya kuendelea kucheza na klabu ya Basingstoke Town. Timu hiyo ya Ligi ya awali, (Conference South) imempa ofa ya mkataba nyota hiuyo wa zamani wa Barcelona na AC Milan ambaye yuko huru baada ya kuondoka Atletico Mineiro ya Brazil, kwa mujibu wa Basingstoke Gazette . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 pia amepewa ofa ya kusafiri hadi England na malazi kama sehemu ya mkataba huo.

Posted via Blogaway

HIKI NDO KITU KINACHO ENDELEA MAN UNITED KUHUSU MARCOS ROJO

BEKI mpya wa Manchester United, Marcos Rojo anaweza kuichezea kwa mara ya kwanza klabu yake hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Queens Park Rangers Uwanja wa Old Trafford Septemba 14 baada ya kupatiwa hati ya kufanya kazi. Rojo alisafiri hadi Lisbon Alhamisi ili kukamilisha taratibu za kupata hati hiyo ya kufanyia kazi England. Kufanikiwa kwa mchezaji huyo kupata hati hiyo ya kufanyia kazi ni faraja kwa kocha Louis van Gaal, ambaye kikosi chake mina tatizo la safu ya ulinzi.

Posted via Blogaway

SOMA ALICHOKISEMA NISHA BAADA YA SKENDO KUENEA KUA ANATOKA KIMAPENZI NA MCHEKESHAJI MASAI NYOTAMBOFU

Mchekeshaji maarufu hapa Tzee ambaye anamiondoko ya kimasai, Gillady Severina aka Masai Nyotambofu, ameteka sana soko la filamu hapa Bongo kwa upande wa Comedy kwa kufanya filamu kibao kama ‘Vyumba Vimejaa’, ‘Inye Ndembendembe’, ‘Pedeshe’ nk. Kwa chanzo chetu cha kuaminika kimebaini uhusiano uliopo baina ya Masai Nyotambofu na Salma Jab aka Nisha anayetamba sokoni na muvi ya ‘Zena Na Betina’, ‘Jike Dume’ nk, mara baada ya kuunasa Comment yake Instagram aliyopost kidume mwenye mbwembwe za kimasai. BK lilijaribu kumuuliza Nyotambofu ambye alijibu hivi, “No jamani mimi sina mahusiano yeyote na Nisha but mimi siku ile nilipost tu kuwataarifu watu juu ya kutoka kwa muvi yake Nisha iliyofahamika kwa jina ‘Zena Na Betina’ basi najua Nisha alitoa Coment hiyo kwasababu aliona kuwa mimi jinsi gani napenda mafanikio yake.” alisema Masai Nyotambovu

Thursday, September 04, 2014

HAYA NDO MAPYA ALIYOYAZUA OKWI LEO HII JAGWANI

YANGA imesikia maneno ya straika wake wa zamani, Emmanuel Okwi, aliyejiunga na Simba na imemuahidi hatocheza mechi za Ligi Kuu Bara labda mazoezi na mechi za kirafiki tu za timu aliyojipeleka. Mapema Okwi aliliambia gazeti hili kwamba ana uhakika ataichezea Simba msimu ujao wa ligi kuu utakaoanza Septemba 20 na akawaambia mashabiki wa Yanga atawafanya kitu kibaya katika mechi dhidi yao Oktoba 12 pale Uwanja wa Taifa. Lakini wakati Okwi akiamini hivyo, Yanga imemjibu kuwa asijidanganye hata kidogo kwani ataishia kucheza mazoezi na mechi za kirafiki tu kwa kuwa wana uhakika juu ya maeneo yatakayowapa ushindi katika mgogoro wao. Mmoja wa mabosi wa juu wa Yanga anayefanya kazi kwa karibu na Mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuf Manji ameliambia Mwanaspoti kuwa hawajashtuka hata kidogo juu ya kauli ya Okwi kwani ana uhakika wa kisheria kuwa mchezaji huyo ataitumikia Simba katika mechi za kirafiki tu. Atakavyonaswa Okwi Bosi huyo alisema hawataki kulumbana na Okwi wala Simba, lakini uongozi wao umejikamilisha vya kutosha kuweza kuishinda vita hiyo ambapo kwanza watatumia mawasiliano ya Okwi alipozungumza na klabu ya Wadigalde FC ya Misri ambayo mchezaji huyo alitaja kiasi cha fedha Dola 60,000 ambazo Yanga ingepatiwa endapo ingekubali kumuuza. “Tumemsikia anachoongea tusubiri tuone kama atacheza huko Simba, unajua Yanga tunafanya kazi kwa mfumo bora, Okwi anatakiwa kutambua kuwa tunayo barua pepe yake ambayo alituarifu juu ya kutakiwa na hiyo timu ya Misri tena akaenda mbali zaidi kwa kutaja mpaka kiasi cha fedha kitakachotolewa na hiyo timu anawezaje kukataa kwamba hakuzungumza nao?” Alihoji. “Pili akumbuke mkataba una kipengele kinachosema mchezaji husika mkataba wake utaanza kutumika pale tu atakapoanza kuitumikia timu na kuhusu vibali vya kuchezea hilo ni jukumu lake kuvifuatilia akivikosa ataturudishia fedha zetu, alipokuja hapa akazuiwa kucheza ni kosa letu au lake?” Aliongeza eneo la tatu ambalo Yanga litawapa ushindi ni kuwa Okwi hana nakala ya barua ikionyesha klabu yao kutaka kuvunja mkataba. “Nimemsikia siku aliyokuwa akitambulishwa akidai tulivunja mkataba wake, anatakiwa kutambua mkataba wake na klabu yetu hatuwezi kuuvunja TFF bila ya kukutana naye, wapi atatuonyesha kwamba tulimwandikia tukitaka kuvunja mkataba wetu?” alihoji. Phiri amtumia Okwi Kocha wa Simba, Patrick Phiri amesema Okwi ni mchezaji mahiri na tayari amemuweka katika programu zake.

FALCAO AIZUNGUMZIA MAN UNITED KWA MARA YA KWANZA SOMA HAPA ALICHOSEMA

MSHAMBULIAJI Radamel Falcao amesema kwamba alikuwa kwenye mazungumzo na Manchester United kwa miezi kadhaa kabla ya uhamisho wake katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili. Mshambuliaji huyo wa Colombia alihusishwa kwa kiasi kikubwa na kuhamia Real Madrid, kabla uhamisho wake wa ghafla kuelekea Old Trafford. Falcao, akizungumza jana wakati akijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil mjini Miami usiku wa Ijumaa amesema: "Ninajivunia sana kuwa Manchester United,". Tayari kwa kazi: Radamel Falcao (katikati) akijifua na Colombia mjini Miami jana "Tumekuwa kwenye mazungomzo na klabu kwa miezi fulani, na mwishowe, tulifikia makubaliano na Monaco katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili,". Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alilazimika kusubiri hadi Saa 7.30 Jumanne ili kukamilisha uhamisho wake wa mkopo wa msimu wa Pauni Milioni 6 kutoka Monaco na kuthibitishwa na Ligi Kuu na kuwa mchezaji wa United.

Posted via Blogaway

EXCLUSIVE : MAMBO MATANO ALIYOSEMA DIAMOND BAADA YA KUKOSWAKOSWA KUPOKEA KIPONDO CHA MASHABIKI WA UJERUMANI.

siku tatu zilizopita stori kubwa kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa zimeenea kuhusiana na fujo zilizotokea Ujerumani kwenye show aliyokwenda kufanya Diamond Platnumz huko Stuttgart. Hizi hapa chini ni kauli za Diamond mwenyewe 1.‘Mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa tatizo lilikua nini, siamini kama tatizo lilikua ni hela, balance iliyokua imebaki ni balance ndogo kama EURO 3500 hivi ambazo ni zaidi ya milioni 7 za Tanzania, ninavyojua Mapromoter wengi wa nje wakifanya show huwa wanauza na vinywaji wenyewe na wanapata hela nyingi sana kwenye vinywaji kuliko hata viingilio so nahisi labda walivuta muda ili waendelee kuuza vinywaji zaidi’ 2. ‘Walichelewa kunipeleka kwenye show, walinifata kwenye mida ya saa tisa usiku na wakawa hawana hela yangu iliyobaki, nikawaambia siendi kokote mpaka wamalize kunilipa, walikua na EURO 1500 wakati nilikua nawadai 3500 nikawaambia lazima wanipe hela yote, wakaifata ndio tukaenda kwenye show’. ‘Tukafika kwenye show saa10 kasoro, kweli hata ningekua mimi shabiki ningekasirika ningefanya vurugu, wengine walilipa zaidi ya laki moja na wametoka kwenye miji na nchi jirani, niliwaambia wanipeleke nikafanye show ndani ya ukumbi japo tulikuta watu wengi sana nje lakini Mapromota walikua waogawaoga kunipeleka ndani’ 4. ‘Nikakuta watu wengi na vurugu nje, nikamwambia promota atupeleke ndani tungefika kwenye stage ingetulia baada ya sisi kuimba manake ni vitu tunakutana navyo kwenye muziki lakini promota walikua waogawaoga, askari wa Ujerumani karibu gari 7 wakaja pale lakini mtiti ukawa mkubwa’ 5. ‘So dakika ya mwisho tukaona hapashukiki ndio wakaturudisha hotelini, kiukweli nimesikitishwa sana manake nilikua nimejipanga vizuri na ilikua ni mara yangu ya kwenda kuperform pale Stuttgart, imenisikitisha manake watu walikua kuniona alafu mwisho ikashindikana kuwafikishia walichokitarajia 6. ’‘Nafikiri October tutakua na show nyingine na itafanyika kulekule, nilikua nazungumza na uongozi wangu kwamba wanataka show nyingine na tayari wameshatuma hiyo hela ya show nyingine’

SHABIKI HUYU WA YANGA APO JANA ALITOA KALI YA MWAKA MAPEMA MAPEMA KUHUSU JAJA

Jaja akishangilia baada ya kufunga na chini akipongezwa na wenzake
Toa Jaja huyooo; Shabiki aliyenyoosha mkono alipiga yowe la kutaka Geilson Santana Santos 'Jaja' atolewe kipindi cha kwanza. Lakini Mbrazil huyo ndiye aliyeifungia bao pekee Yanga SC leo dakika ya 58.

Posted via Blogaway

KWA MARA YA KWANZA RONALDO AZUNGUMZIA KUHUSU KULUDI MAN UNITED

MWANASOKA Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo amesema kwamba Manchester United ni klabu ambayo ipo moyoni make na anatamani siku moja are jee kucheza tena. Mchezaji huyo wa Real Madrid na Ureno ameweka wazi "MaipendaI Manchester," na kuongeza; "Kila mmoja anajua hilo — nimesema hivyo mara nyingi. Manchester ipo moyoni mwangu. Nimeacha marafi wengi huko, mashabiki wanavutia sana na ninatamani siku moja ningerudi,".

Posted via Blogaway

New AUDIO | Hemedy PHD Ft. Bela Combo - Far Away | Download hapa

Hemedy PHD amechia wimbo mpya amemshirikisha Mwanadada Bela Combo wimbo unaitwa “Far Away” Studio Sei Records Video teyali wamesha Shoot itatoka hivi karibu
amefanya na Kwetu Studio BOFYA HAPA KUDOWNLOAD NGOMA HII 

Posted via Blogaway

MAN UNITED IKIWA NA FALCAO, INAWEZA KUPANGWA HIVI AU HIVI...

KOCHA LOUIS VAN GAAL ANAWEZA KUIPANGA
MAN UNITED NAMNA HII KATIKA MIFUMO
MIWILI TOFAUTI HUKU RAMADEL FALCAO AKIONGOZA MASHAMBULIZI KWA
KUSHIRIKIANA NA NAODHA WAYNE ROONEY NA
ROBIN VAN PERSIE.

Posted via Blogaway

PERUZI KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI MBALIMBALI YA LEO ALHAMISI HAPA

Dakika 3 za Wema Sepetu akizungumzia yote yanayosemwa ikiwemo isue ya kuajiriwa na Kajala.

Kupitia mitandao na magazeti siku chache zilizopita ilitoka stori ambayo ilidai Kajala anaelekea kumuajiri Wema Sepetu,leo Wema kapatikana na kakubali kuongelea isue hizo zote ikiwemo hiyo ya Kajala. Kupitia You heard ya XXL ya Clouds Fm Soudy Brown alianza kwa kutaka kufahamu kama kweli Kajala anaweza kumuajiri yeye [Wema],Wema Sepetu akamjibu>>’Inawezekana,kila kitu kinawezekana Soudy’ Kuhusu mshahara ambao anataka kulipwa na Kajala,Wema Sepetu amejibu>>’Kwa Kajala mi sihitaji mshahara hata bure nitafanya kazi kwa Kajala,shughuli yoyote nitafanya Soudy’ Soudy Brown alipomuuliza kuhusu fununu za Meninah kutoka na Diamond,Wema amejibu>>’Mimi sijui Soudy bwana na wala sijali’. Bonyeza play kusikiliza.

 PLAY HAPA KUSIKILIZA 

Source millardayo

Posted via Blogaway

BAADA YA MR NICE KUNUSULIKA KIFO HAJA NA HII KUBWA KULIKO

Baada ya kunusurika kifo mwezi April mwaka huu, Lucas Mkenda aka Mr Nice ameibuka na kuzungumzia mipango yake mipya ya kazi yake ya muziki ambayo ilisimama baada ya kupata ajali mbaya ya bajaj iliyomsababisha kukaa muda mrefu akisubiri kupona. Nice ambaye ni mwimbaji na mwanzilishi wa staili ya Takeu, amesema amefanya kazi mpya na producer wake wa kwanza aliyemtoa aitwaye Kameta. “Napenda kuwajulisha marafiki zangu wote wa Tanzania, wapenda muziki kwamba nimefanya na rafiki yangu wa zamani Kameta producer ambaye ndio wa kwanza kufanya kazi na mimi” .Mr Nice aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm. “Kilichokuja kunikwamisha ni baada ya kupata ajali kwasababu unajua niliumia sana kama ulisikia niliokuwepo nao wote walikufa mi nikabahatika kusalia mwenyewe tu ikawa kidogo imeniweka chini, unajua maswala ya kuvunjika ukishavunjikavunjika tena sio kitu cha siku mbili tatu.” Amesema Nice. Nice ameongeza kuwa kabla mwaka huu haujaisha tayari atakuwa ametoa kazi hiyo mpya sababu anajipanga kufanya na video. “Kabla ya mwezi desemba nitakuwa na kitu ambacho ni very special ambacho nimewawish wanawake wote wa Tanzania na dunia nzima, lakini kwa sasa hivi nipo katika final recovery ya tangu nipate ajali.” Kameta ndiye producer aliyemtoa mr Nice na kumtengenezea album yake ya kwanza iliyokuwa na hits kama ‘Kikulacho’, ‘Kidalipo’ na zingine.

  KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA ILI KILA NIKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI PUNDE NIZIPATAPO  

Posted via Blogaway

Diamond Platnumz azungumza kwa mara ya kwanza kuhusu fujo zilizotokea Ujerumani

Pamoja na kwamba mapromoter Wanigeria walioandaa show ya Diamond iliyoshindwa kufanyika weekend iliyopita mjini Stuttgart, Ujerumani baada ya kutokea vurugu kubwa, upande wa Diamond Platnumz amesema kwake haoni kama tukio hilo limemchafua kwa namna yoyote na badala yake anaona limempa ‘kiki’. “Sidhani kwasababu karibuni asilimia tisini walijua nini kinachoendelea hawakujua kabisa tatizo lilikuwa kwa msanii…hiki kitu kiko wazi na hata promota nasikia amezungumza kuwaambia kwamba halikuwa tatizo la msanii” amesema Diamond kupitia 255 ya Clouds Fm. Diamond amesema kuwa baada ya tukio hilo asubuhi yake vyombo vingi vya habari vya Ujerumani viliandika habari hiyo ambayo kwa upande wake hiyo ni faida. “mi nachokiona sana sana naona busta tu kwasababu asubuhi yake iliandikwa katika blog kibao za Ujerumani magazeti ya Ujerumani, katika vitu viiingi vya Ujerumani viliandika kama ilitokea hivi na hivi na hivi afu kila ikiandikwa itamuandika Diamond wanaweka picha ya Diamond. So kwa namna moja ama nyingine Mwenyezi Mungu alitumia njia ile kufanya watu wa Ujerumani kama kuna mtu anaitwa Diamond wajue kuna mtu anaitwa Diamond”. Hata hivyo kwa upande mwingine Platnumz amesema alijisikia vibaya pamoja na kwamba alilipwa pesa yote lakini kama msanii kuna kitu muhimu alichokikosa. “Kiukweli nilijiskia vibaya kwasababu msanii hakuna kitu unachokifurahia kwanza kama show ijae kwasababu show ikijaa kwanza ni credit, ni cv kubwa sana unajua unavyopost ile picha umejaza unawatengenezea promoters wengine kuona kama huyu mtu anakubalika”.
Uharibifu uliotokana na vurugu hizo

  KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA ILI KILA NIKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI PUNDE NIZIPATAPO  

Posted via Blogaway

JAJA, JAJA, JAJA…YANGA WAWAAA, WAKENYA CHALI TAIFA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM BAO pekee la Mbrazil Genilson Santana Santos ‘Jaja’ limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Thika United ya Kenya katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Jaja alifunga dakika ya 58 kwa pasi ya Simon Msuva na hilo linakuwa bao la pili kwa Jaja tangu ajiunge na Yanga SC miezi miwili iliyopita, akiwa amecheza mechi yake ya nne leo. Jaja aliingia ‘mzima mzima’ pembezoni mwa lango la Thika kuhakikisha anaiunganishia nyavuni krosi ya Msuva kwa vyovyote na akafanikiwa akimuacha kipa Mganda, Hamza Muwonge anaokota mpira nyavuni. Kwa furaha ya bao hilo, Jaja ambaye alikuwa akizomewa na mashabiki wa Simba SC kila alipokosea alitoka nje ya Uwanja kushangilia bao hilo, kwa shangwe za aina zote alizoweza. Yanga SC haikucheza vizuri kipindi cha kwanza na zaidi ilitegemea kupitisha mashambulizi yake pembeni walipokuwa wakiteleza kwa awamu Simon Msuva, Haruna Niyonzima na Andrey Coutinho. Coutinho alikaribia kufunga mara mbili kwa mipira ya adhabu aliyopiga kutoka nje kidogo ya eneo la penalti, wakati Jaja hakuwa na madhara kabisa kipindi cha kwanza. Nafasi nzuri zaidi kwa Thika ilikuwa dakika ya 20 wakati shuti la Moses Odhiambo lilipodakwa na kipa Deo Munishi ‘Dida’- zaidi ya hapo, safu ya ulinzi ya Yanga SC leo ilicheza vizuri. Kipindi cha pili, kocha Mbrazil Marcio Maximo alianza na mabadiliko katika safu ya kiungo akimpumzisha Hassan Dilunga na kumuingiza Hamisi Thabit, ambaye alikwenda kuibadilisha timu. Angalau Yanga wakaanza kucheza mpira, pasi zilionekana kutembea uwanjani na mashabiki wakaanza kushangilia ‘chama lao’. Ni Hamisi Thabit ambaye alimpasia mpira mzuri Msuva, aliyemtoka beki wa Thika hadi nje kidogo ya eneo la penalti alipomtilia krosi Jaja, aliyefunga bao hilo pekee. Refa Hashim Abdallah aligoma kutoa penalti dakika ya 62 baada Coutinho kuangushwa kwenye eneo la hatari, wakati Said Bahanuzi aliyetokea benchi alichelewa kuunganisha krosi nzuri ya Niyonzima dakika ya 80. Huo unakuwa mchezo wa nne kwa Maximo tangu aanze kazi Yanga SC Julai mwaka huu na amefanikiwa kushinda mechi zote, 1-0 dhidi ya Chipukizi Uwanja wa Gombani, Pemba kabla ya kushinda 2-0 mara mbili dhidi ya Shangani na KMKM Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Hassan Dilunga/Hamisi Thabit dk46, Haruna Niyonzima/Omega Seme dk73, Genilson Santana ‘Jaja’/Said Bahanuzi dk87, Andery Coutinho/Nizar Khalfan dk60 na Simon Msuva/Hussein Javu dk70.

  KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA ILI KILA NIKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI PUNDE NIZIPATAPO  

Posted via Blogaway