Thursday, September 04, 2014
 |
MSHAMBULIAJI Radamel Falcao amesema
kwamba alikuwa kwenye mazungumzo na
Manchester United kwa miezi kadhaa kabla ya
uhamisho wake katika siku ya mwisho ya
kufunga pazia la usajili.
Mshambuliaji huyo wa Colombia alihusishwa
kwa kiasi kikubwa na kuhamia Real Madrid,
kabla uhamisho wake wa ghafla kuelekea Old
Trafford.
Falcao, akizungumza jana wakati akijiandaa na
mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil mjini Miami
usiku wa Ijumaa amesema: "Ninajivunia sana
kuwa Manchester United,".
Tayari kwa kazi: Radamel Falcao (katikati)
akijifua na Colombia mjini Miami jana
"Tumekuwa kwenye mazungomzo na klabu kwa
miezi fulani, na mwishowe, tulifikia
makubaliano na Monaco katika siku ya mwisho
ya kufunga pazia la usajili,".
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28
alilazimika kusubiri hadi Saa 7.30 Jumanne ili
kukamilisha uhamisho wake wa mkopo wa
msimu wa Pauni Milioni 6 kutoka Monaco na
kuthibitishwa na Ligi Kuu na kuwa mchezaji wa
United. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment