Friday, September 05, 2014
 |
BEKI mpya wa Manchester United, Marcos
Rojo anaweza kuichezea kwa mara ya kwanza
klabu yake hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya
England dhidi ya Queens Park Rangers Uwanja
wa Old Trafford Septemba 14 baada ya
kupatiwa hati ya kufanya kazi.
Rojo alisafiri hadi Lisbon Alhamisi ili
kukamilisha taratibu za kupata hati hiyo ya
kufanyia kazi England.
Kufanikiwa kwa mchezaji huyo kupata hati
hiyo ya kufanyia kazi ni faraja kwa kocha Louis
van Gaal, ambaye kikosi chake mina tatizo la
safu ya ulinzi. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment