Thursday, September 04, 2014
 |
siku tatu zilizopita stori kubwa kwenye
mitandao ya kijamii zilikuwa zimeenea
kuhusiana na fujo zilizotokea Ujerumani
kwenye show aliyokwenda kufanya
Diamond Platnumz huko Stuttgart.
Hizi hapa chini ni kauli za Diamond
mwenyewe
1.‘Mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa
tatizo lilikua nini, siamini kama tatizo
lilikua ni hela, balance iliyokua imebaki ni
balance ndogo kama EURO 3500 hivi
ambazo ni zaidi ya milioni 7 za Tanzania,
ninavyojua Mapromoter wengi wa nje
wakifanya show huwa wanauza na vinywaji
wenyewe na wanapata hela nyingi sana
kwenye vinywaji kuliko hata viingilio so
nahisi labda walivuta muda ili waendelee
kuuza vinywaji zaidi’
2. ‘Walichelewa kunipeleka kwenye show,
walinifata kwenye mida ya saa tisa usiku na
wakawa hawana hela yangu iliyobaki,
nikawaambia siendi kokote mpaka
wamalize kunilipa, walikua na EURO 1500
wakati nilikua nawadai 3500 nikawaambia
lazima wanipe hela yote, wakaifata ndio
tukaenda kwenye show’. ‘Tukafika kwenye
show saa10 kasoro, kweli hata ningekua
mimi shabiki ningekasirika ningefanya
vurugu, wengine walilipa zaidi ya laki moja
na wametoka kwenye miji na nchi jirani,
niliwaambia wanipeleke nikafanye show
ndani ya ukumbi japo tulikuta watu wengi
sana nje lakini Mapromota walikua
waogawaoga kunipeleka ndani’
4. ‘Nikakuta watu wengi na vurugu nje,
nikamwambia promota atupeleke ndani
tungefika kwenye stage ingetulia baada ya
sisi kuimba manake ni vitu tunakutana
navyo kwenye muziki lakini promota
walikua waogawaoga, askari wa Ujerumani
karibu gari 7 wakaja pale lakini mtiti
ukawa mkubwa’
5. ‘So dakika ya mwisho tukaona
hapashukiki ndio wakaturudisha hotelini,
kiukweli nimesikitishwa sana manake
nilikua nimejipanga vizuri na ilikua ni mara
yangu ya kwenda kuperform pale Stuttgart,
imenisikitisha manake watu walikua
kuniona alafu mwisho ikashindikana
kuwafikishia walichokitarajia
6. ’‘Nafikiri October tutakua na show
nyingine na itafanyika kulekule, nilikua
nazungumza na uongozi wangu kwamba
wanataka show nyingine na tayari
wameshatuma hiyo hela ya show nyingine’ |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment