Thursday, September 04, 2014
 |
MSHAMBULIAJI Radamel Falcao amesema
kwamba alikuwa kwenye mazungumzo na
Manchester United kwa miezi kadhaa kabla
ya uhamisho wake katika siku ya mwisho
ya kufunga pazia la usajili. Mshambuliaji
huyo wa Colombia alihusishwa kwa kiasi
kikubwa na kuhamia Real Madrid, kabla
uhamisho wake wa ghafla kuelekea Old
Trafford. Falcao, akizungumza jana wakati
akijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya
Brazil mjini Miami usiku wa Ijumaa
amesema: "Ninajivunia sana kuwa
Manchester United,". Tayari kwa kazi:
Radamel Falcao (katikati) akijifua na
Colombia mjini Miami jana "Tumekuwa
kwenye mazungomzo na klabu kwa miezi
fulani, na mwishowe, tulifikia makubaliano
na Monaco katika siku ya mwisho ya
kufunga pazia la usajili,". Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 28 alilazimika
kusubiri hadi Saa 7.30 Jumanne ili
kukamilisha uhamisho wake wa mkopo wa
msimu wa Pauni Milioni 6 kutoka Monaco
na kuthibitishwa na Ligi Kuu na kuwa
mchezaji wa United. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment