Friday, September 05, 2014

RONALDINHO APATA MKATABA MPYA BAADA YA KUBWAGA MANYANGA ATLETICO MINEIRO

MWANASOKA bora wa zamani wa dunia, Ronaldinho Gaucho amepewa ofa ya kuendelea kucheza na klabu ya Basingstoke Town. Timu hiyo ya Ligi ya awali, (Conference South) imempa ofa ya mkataba nyota hiuyo wa zamani wa Barcelona na AC Milan ambaye yuko huru baada ya kuondoka Atletico Mineiro ya Brazil, kwa mujibu wa Basingstoke Gazette . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 pia amepewa ofa ya kusafiri hadi England na malazi kama sehemu ya mkataba huo.

Posted via Blogaway

0 comments:

Post a Comment