Thursday, September 04, 2014
 |
YANGA imesikia maneno ya straika wake wa
zamani, Emmanuel Okwi, aliyejiunga na Simba
na imemuahidi hatocheza mechi za Ligi Kuu
Bara labda mazoezi na mechi za kirafiki tu za
timu aliyojipeleka.
Mapema Okwi aliliambia gazeti hili kwamba
ana uhakika ataichezea Simba msimu ujao wa
ligi kuu utakaoanza Septemba 20 na
akawaambia mashabiki wa Yanga atawafanya
kitu kibaya katika mechi dhidi yao Oktoba 12
pale Uwanja wa Taifa. Lakini wakati Okwi
akiamini hivyo, Yanga imemjibu kuwa
asijidanganye hata kidogo kwani ataishia
kucheza mazoezi na mechi za kirafiki tu kwa
kuwa wana uhakika juu ya maeneo
yatakayowapa ushindi katika mgogoro wao.
Mmoja wa mabosi wa juu wa Yanga anayefanya
kazi kwa karibu na Mwenyekiti wa timu hiyo,
Yusuf Manji ameliambia Mwanaspoti kuwa
hawajashtuka hata kidogo juu ya kauli ya Okwi
kwani ana uhakika wa kisheria kuwa mchezaji
huyo ataitumikia Simba katika mechi za kirafiki
tu.
Atakavyonaswa Okwi
Bosi huyo alisema hawataki kulumbana na
Okwi wala Simba, lakini uongozi wao
umejikamilisha vya kutosha kuweza kuishinda
vita hiyo ambapo kwanza watatumia
mawasiliano ya Okwi alipozungumza na klabu
ya Wadigalde FC ya Misri ambayo mchezaji
huyo alitaja kiasi cha fedha Dola 60,000
ambazo Yanga ingepatiwa endapo ingekubali
kumuuza.
“Tumemsikia anachoongea tusubiri tuone kama
atacheza huko Simba, unajua Yanga tunafanya
kazi kwa mfumo bora, Okwi anatakiwa
kutambua kuwa tunayo barua pepe yake
ambayo alituarifu juu ya kutakiwa na hiyo timu
ya Misri tena akaenda mbali zaidi kwa kutaja
mpaka kiasi cha fedha kitakachotolewa na hiyo
timu anawezaje kukataa kwamba hakuzungumza
nao?” Alihoji.
“Pili akumbuke mkataba una kipengele
kinachosema mchezaji husika mkataba wake
utaanza kutumika pale tu atakapoanza
kuitumikia timu na kuhusu vibali vya kuchezea
hilo ni jukumu lake kuvifuatilia akivikosa
ataturudishia fedha zetu, alipokuja hapa
akazuiwa kucheza ni kosa letu au lake?”
Aliongeza eneo la tatu ambalo Yanga litawapa
ushindi ni kuwa Okwi hana nakala ya barua
ikionyesha klabu yao kutaka kuvunja mkataba.
“Nimemsikia siku aliyokuwa akitambulishwa
akidai tulivunja mkataba wake, anatakiwa
kutambua mkataba wake na klabu yetu
hatuwezi kuuvunja TFF bila ya kukutana naye,
wapi atatuonyesha kwamba tulimwandikia
tukitaka kuvunja mkataba wetu?” alihoji.
Phiri amtumia Okwi
Kocha wa Simba, Patrick Phiri amesema Okwi
ni mchezaji mahiri na tayari amemuweka katika
programu zake. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment