Thursday, September 04, 2014
 |
Baada ya kunusurika kifo mwezi April mwaka
huu, Lucas Mkenda aka Mr Nice ameibuka na
kuzungumzia mipango yake mipya ya kazi yake
ya muziki ambayo ilisimama baada ya kupata
ajali mbaya ya bajaj iliyomsababisha kukaa
muda mrefu akisubiri kupona.
Nice ambaye ni mwimbaji na mwanzilishi wa
staili ya Takeu, amesema amefanya kazi mpya
na producer wake wa kwanza aliyemtoa aitwaye
Kameta.
“Napenda kuwajulisha marafiki zangu wote wa
Tanzania, wapenda muziki kwamba nimefanya
na rafiki yangu wa zamani Kameta producer
ambaye ndio wa kwanza kufanya kazi na
mimi” .Mr Nice aliiambia 255 ya XXL ya Clouds
Fm.
“Kilichokuja kunikwamisha ni baada ya kupata
ajali kwasababu unajua niliumia sana kama
ulisikia niliokuwepo nao wote walikufa mi
nikabahatika kusalia mwenyewe tu ikawa
kidogo imeniweka chini, unajua maswala ya
kuvunjika ukishavunjikavunjika tena sio kitu
cha siku mbili tatu.” Amesema Nice.
Nice ameongeza kuwa kabla mwaka huu
haujaisha tayari atakuwa ametoa kazi hiyo
mpya sababu anajipanga kufanya na video.
“Kabla ya mwezi desemba nitakuwa na kitu
ambacho ni very special ambacho nimewawish
wanawake wote wa Tanzania na dunia nzima,
lakini kwa sasa hivi nipo katika final recovery
ya tangu nipate ajali.”
Kameta ndiye producer aliyemtoa mr Nice na
kumtengenezea album yake ya kwanza
iliyokuwa na hits kama ‘Kikulacho’, ‘Kidalipo’ na
zingine. |
KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA ILI KILA NIKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI PUNDE NIZIPATAPO
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment