Friday, October 10, 2014

HUSSEIN MACHOZI NAE KAACHIA NYIMBO INAITWA ""MDOGOMDOGO"" MTANDAO WA KENYA WAMPAMBANISHA NA DIAMOND

Mtandao wa GHAFLA wa Kenya umewaweka ulingoni nyota wa Tanzania Diamond Platnumz na Hussein Machozi kwa kupambanisha wimbo wa ‘Mdogo Mdogo’ wa Platnumz, na wimbo ‘mpya’ wa Machozi ambao bado haujatoka wenye jina hilo hilo ‘Mdogo Mdogo’. “Is This Beef in the Making??” Ndivyo umeuliza mtandao huo kwenye kichwa cha habari hiyo. “Hussein Machozi has chucked another tune dubbed Mdogo mdogo which surprisingly shares the same name with Diamond’s Mdogo mdogo barely 3 months after the latter dropped his. The BIG QUESTION could this be a drive to prove Diamond wrong? If you listen to this tune by Hussein Machozi its crystal clear that it is a big tune but do i say? “ Hivi ndivyo ilivyoandikwa na mtandao huo. GHAFLA wameongeza kuwa kuna tetesi kuwa Hussein Machozi na Diamond hawapikiki chungu kimoja. Iskilize ‘Mdogo Mdogo’ ya Hussein Machozi Diamond – Mdogo Mdogo

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

KAJALA YAMKUTA BAADA YA KUWEKA PICHA YA SIMU AMBAYO AIJATOKA SOKONI AKIDAI ANAYO

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

Kajala yamkuta baada ya kuweka picha simu ambayo bado haijatoka sokoni akidai anayo

Kupitia mtandao maarufu wa picha wa kijamii, mwanadada Kajala amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuweka picha ya simu aina ya samsung galaxy note 4 kwenye account yake kuwa anamiliki simu hiyo ilihali simu yenyewe ikiwa bado hata haijaanzwa kuuzwa sehemu yoyote duniani. Kupitia picha hiyo kajala aliambulia maneno kadhaa ya kashfa toka kwa watu mbalimbali wengi wao wakimtaka aache maisha ya kuigiza.

Baadhi ya maoni hayo ni:-

"Hahahaha watu ndo wanatoa pre order october 16 ndo ina launched we umeitoa wap wakat bado haijaanzwa kuuzwa!dah!kwel sasa naanza kumin maisha yako ni ya kuigiza nakufata mkumbo mumy...pole"

"Duh ... Simu aijatoka hiyo Pre Order imeanza USA & UK tarehe 19/09 lkn retail stores wanaanza kuuza tarehe 17/10 , hiyo pre order kwa watu ambao awataki kumiss ikitoka wanalipia kabisa ikitoka unaenda kuchukua , sasa hiyo umenunua wapi mwenzetu..."

"KAJALA ACHA UONGO HII CM LABDA MCHINA ORIGINAL HAIJATOKA MPKA KWA ORDER LOO MWANAMKE MZIMA MPKA LEO UNARINGISHIA CM PAULA NAE AFANYE NINI"

Wewe unaonaje kuhusu jambo hili la mastaa nchini kuishi maisha ya kuigiza kwa ajili ya kuonekana wapo juu kwa mashabiki wao?

ROY KEANE AMTANDIKA FERGUSON, ASEMA AMEPATA MAMILIONI, JUKWAA, SANAMU LAKINI…

Vita ya maneno kati ya Roy Keane na Alex Ferguson sasa inazidi kuchanja mbuga.
Keane aliyekuwa nahodha wa Manchester United iliyopata mafanikio makubwa chini ya Ferguson, amesema kocha huyo ni muongo. Keane amesema hayo wakati akizizundua kitabu chake kipya cha Second Half. Hajapoteza maneno au kupepesa baada ya kusema aliamua kitabu hicho baada ya kusoma maneno mengi ya uongo ya Ferguson kwenye kitabu chake kilichochapishwa mwaka jana.
“Ajabu kabisa, Ferguson amepata mamilioni, amepata jukwaa na sanamu kwenye Uwanja wa Old Trafford, hayo yote ni mafanikio. “Sasa ni ajabu sana kama anafikia hatua ya kuwasema maneno mabaya watu waliomsaidia kupata hayo mafanikio. “Kwangu nimeona si mambo sahihi, hapaswi kufanya hivyo na hakuwa sahihi. “Hakika sikuwa nina mpango wa kutoa kitabu, lakini baada kitabu chake niliona lazima nifanye hivyo,” alisema Keane ambaye ni kocha msaidizi wa Aston Villa. Katika kitabu hicho cha Feguson (AMBACHO HUTAFSIRIWA KWA KISWAHILI NA GAZETI LA MICHEZO LA CHAMPIONI), ameeleza namna Keane alivyokuwa mkorofi na asiyewakubali wachezaji vijana.
Ameeleza kuwa Keane hakupenda wengine wafanikiwe na alijisahau baada ya yeye kumpa uhuru. Pia alieleza na kukiponda kitendo chake cha kuwasakama wachezaji wa Man United kwenye mahojiano yake na runinga ya klabu hiyo ya MUTV. Lakini Keane amesema yote hayo ni uzushi mtupu na ameyajibu kwenye kitabu chake hicho cha Second Half.

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

BREAKING NEWS: SIMBA SC YAFUKUZA TENA KOCHA, MZUNGU AANZA KAZI AFRIKA KUSINI

Na Princess Asia, JOHANNESBURG KOCHA Mzungu anawanoa makipa wa Simba SC katika kambi yao, Afrika Kusini wakati kocha wa makipa wa Oman, Choke Abeid anatarajiwa kutua wakati wowote kuanza rasmi kazi ya ‘kuwafua’ makipa wa timu hiyo, baada ya kutupiwa virago kwa Iddi Pazi ‘Father’. Pazi aliachwa Dar es Salaam wakati Simba SC inaondoka jana na ingawa hajaambiwa chochote, lakini ndiyo ametimuliwa- baada ya uongozi kuamini viwango vya makipa wao vimeshuka chini yake. Simba SC imeanza mazoezi leo kwenye viwanja vya Hoteli ya Eden Vale Petra mjini Johannesburg walipofikia na keshokutwa watacheza mchezo wa kirafiki na wenyeji Orlando Pirates mjini Johannesburg. Simba ipo Afrika Kusini tangu jana kwa ajili ya maandalizi yake ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, Oktoba 18, mwaka huu Dar e Salaam. Suleiman Matola aliyekuwa kocha Msaidizi tangu wakati wa Mcroatia, Zdravko Logarusic anaendelea kuwa Msaidizi wa Mzambia, Patrick Phiri wakati Meneja anaendelea Nico Nyagawa. Katika mchezo na Pirates, Simba SC itawakosa wachezaji wake walio timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Uganda, The Cranes- ambao wanatarajiwa kujiunga na wenao kuanzia Jumatatu. Hata hivyo, mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyekwenda kujiunga na The Cranes yeye hatakwenda kabisa Afrika Kusini, kwa sababu timu yake hiyo ya taifa itakuwa na mechi ya kufuzu AFCON katikati ya wiki. Wachezaji wa Simba SC walioko Stars ni; mabeki Miraji Adam na Joram Mgeveke na viungo Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo ambao wote watakwenda Afrika Kusini Jumatatu. Simba SC itakuwa ikifanya mazoezi ya nguvu hadi Oktoba 17 itakaporejea Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja kabla ya mechi na watani. Baada ya sare tatu mfululizo katika mechi zake tatu za awali, 2-2 na Coastal Union, 1-1 mara mbili na Polisi Moro na Stand United, Simba SC imepania kushinda mechi ya kwanza Oktoba 18.
Mzungu akiwanoa makipa wa Simba leo
Simba SC wakijifua Afrika Kusini leo

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

Thursday, October 09, 2014

ULIONA PICHA HII YA POLISI WA TANZANIA ILIYOSAMBAA MITANDAONI? HATIMAYE MAAMUZI YAMETANGAZWA

Kama kila siku huwa unaingia facebook, whatsapp au instagram inawezekana ukawa ulikutana na hii picha ya Askari Polisi ambao walipigwa picha wakiwa wanakiss wakiwa ndani ya sare za jeshi hilo. Sasa taarifa mpya iliyotoka baada ya hii picha kuzidi kusambaa ni kwamba Jeshi la Polisi Kagera limechukua maamuzi ya kuwafukuza kazi askari hawa wawili pamoja na mwingine mmoja ambae ndio aliipiga hii picha kupitia simu yake ya mkononi. Kamanda wa Jeshi la Polisi Henry Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788,PC Fadhili Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme na wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Missenyi.
Kamanda Mwaibambe amezungumza na ITV na kusema askari hao walitenda kosa hilo la fedhea kwa kupiga picha kinyume na maadili ya jeshi hilo mwaka 2012 wakiwa kazini na kwamba PC Fadhili ndiye aliyehusika na kupiga picha hizo kwa kutumia simu yake ya mkononi na kuituma katika mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo ambacho ni kinyume cha maadili kwa sababu mbalimbali. Mwaibambe amekiri kuwa picha husika inayoonekana kwenye mitandao ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa hivyo ni wazi kila askari kujua maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari yeyote anafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polisi.

JOHARI NA CHUCHU HANS USURA WAZICHAPE TENA KISA PENZI LA RAY, ILIKUA HIVII…

Stori: Hamida Hassan na Imelda Mtema wa Global Publishers Mastaa wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans ambao wamekuwa katika bifu kwa muda mrefu kutokana na uhusiano wa kimapenzi na Vincent Kigosi ‘Ray’, hivi karibuni nusu wazichape kwa mara nyingine baada ya kurushiana matusi mazito ya nguoni
Tukio hilo lilijiri juzikati katika hoteli moja iliyopo Sinza jijini Dar. Chanzo cha uhakika kilichokuwa eneo la tukio kinavujisha kwamba, Ray alifika katika hoteli hiyo akiwa katika teksi na aliandamana na Chuchu. Inadaiwa Ray alifika hotelini hapo kwa ajili ya kuonana na mkurugenzi mwenza wa kampuni yao ya RJ, Johari, ambaye kwa wakati huo alikuwa akisimamia kambi ya projekti yao mpya. Baada ya Ray kushuka kwenye teksi na kuingia ndani ya hoteli hiyo huku Chuchu naye akishuka kwenye na kusimama nje akimwangalia mwandani wake anavyomsogelea Johari ambaye siku za nyuma alikuwa ndiye mwandani wake. Kitendo cha Chuchu kutokeza kuonesha alikuwa ameandamana na mkali huyo wa filamu kilimchukiza Johari ambaye kwa sauti iliyosikika vyema, alimuuliza Ray kwa nini alikwenda akiwa ameongozana na ‘malaya’ wake.
“Matusi yale yalimkera sana Chuchu, naye aliamua kumrudishia hali iliyosababisha kutokea kwa tafrani kubwa kwani watu walianza kujazana na kuwazuia wasichapane,” kilisema chanzo chetu. Baada ya habari hii kutua mezani, mapaparazi wetu waliingia kazini ili kuujua ukweli, mtu wa kwanza kuzungumza naye ni Johari ambaye siku za nyuma aliwahi kuzichapa na mpinzani wake huyo wakati akilitetea penzi lake lililokuwa likiyumba. Johari alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa mwigizaji huyo alikwenda kambini kwake kufanya fujo ambazo hata hivyo alishindwa kufafanua. Kwa upande wake, Chuchu alipoulizwa alisema: “Nimemvumilia sana Johari, amekuwa akinitukana kila kukicha nanyamaza, sasa nimechoka na kibaya zaidi siku hiyo alinitukania mama yangu, nimekuwa nikimvumilia kwa sababu alikuwa akinitukana mimi, sasa kumuingiza mama kwenye ugomvi wetu siwezi kumvumilia kamwe,” alisema Chuchu.

PERUZI KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI YOTE YA LEO ALHAMISI HAPA

Home » AyoTV » Jibu alilolitoa Jay Z akitembea baada ya kumsikia mtu wa pembeni akiuliza Jay Z ni nani? (video) Jibu alilolitoa Jay Z akitembea baada ya kumsikia mtu wa pembeni akiuliza Jay Z ni nani?


Rapper Jay Z na mke wake wapo Paris Ufaransa wiki hii ambapo wakati Jay akiwa kwenye matembezi huku akiwa amembeba mtoto wake ilitokea mmoja wa Watalii baada ya kumuona Jay akauliza ‘huyu ni nani? unajua jibu alilotoa mume huyu wa Beyonce?
Kabla ya Jay Z kujibu, mlinzi wake aliekua ametangulia mbele hatua chache huku Jay akifata kwa nyuma na timu yake alikua akizuia watu kupiga video ambapo huyu mtalii alikua akipiga video, akawa anashangaa imekuaje akatazwe kupiga video… swali lililoambatana na kuuliza huyu anaepita nani? Jay Z kwa kiburi na yeye akamjibu kwa kuuliza ‘wewe ni nani?‘

Japo inaonekana Jay Z alijibu kwa dharau, wataalamu wa mambo wanasema huenda kweli mtalii huyu hakuwa anajua anaepita ni nani manake alikua kwenye eneo la kitalii ambalo wengi wanaokuwepo hapo huchukua kumbukumbu kupitia camera zao.

Home » AyoTV » Jibu alilolitoa Jay Z akitembea baada ya kumsikia mtu wa pembeni akiuliza Jay Z ni nani? (video) Jibu alilolitoa Jay Z akitembea baada ya kumsikia mtu wa pembeni akiuliza Jay Z ni nani?

Home » AyoTV » Jibu alilolitoa Jay Z akitembea baada ya kumsikia mtu wa pembeni akiuliza Jay Z ni nani? (video)
Jibu alilolitoa Jay Z akitembea baada ya kumsikia mtu wa pembeni akiuliza Jay Z ni nani? (video)
Posted by: Millard Ayo October 8, 2014 AyoTV, Ent.
Rapper Jay Z na mke wake wapo Paris Ufaransa wiki hii ambapo wakati Jay akiwa kwenye matembezi huku akiwa amembeba mtoto wake ilitokea mmoja wa Watalii baada ya kumuona Jay akauliza ‘huyu ni nani? unajua jibu alilotoa mume huyu wa Beyonce?
Kabla ya Jay Z kujibu, mlinzi wake aliekua ametangulia mbele hatua chache huku Jay akifata kwa nyuma na timu yake alikua akizuia watu kupiga video ambapo huyu mtalii alikua akipiga video, akawa anashangaa imekuaje akatazwe kupiga video… swali lililoambatana na kuuliza huyu anaepita nani? Jay Z kwa kiburi na yeye akamjibu kwa kuuliza ‘wewe ni nani?‘

Japo inaonekana Jay Z alijibu kwa dharau, wataalamu wa mambo wanasema huenda kweli mtalii huyu hakuwa anajua anaepita ni nani manake alikua kwenye eneo la kitalii ambalo wengi wanaokuwepo hapo huchukua kumbukumbu kupitia camera zao.

MAMBO YA KISHAMBA AMBAYO MWANAUME WA SASA HUTAKIWA KUYAFANYA

1. Kufuata mkumbo, kutokuwa na maamuzi yako mwenyewe.

2. Kuongea lugha chafu, huwezi kumaliza sentensi bila matusi.

3. Kuvaa mlegezo.

4. Kunyoa panki, kiduku au kuacha afro.

5. Kuvaa viatu vya four angles au vyenye soli kubwa.

6. Kukimbia mimba au kutelekeza familia.

7. Kunywa pombe bila kipimo, kushinda bar bila sababu maalumu utadhani wewe kreti.

8. Kuvaa suruali za model au bwanga au kuvaa mayeno.

9. Kumpiga mwanamke awe mkeo, mpenzi wako au hata rafiki tu.

10. Kuwa na hulka ya kupigana, yani huwezi ku-solve tatizo kwa njia nyingine zaidi ya kuwaza kupigana.

11. Kuwa wa kwanza kulala na wa mwisho kuamka.

12. Kuvaa tshirts zenye maneno makubwa na mbaya zaidi yasiyo na maana.

13. Kulakula hovyo, hyo tabia tuwaachie wanawake

14. Kuvaa vitu oversize ili udumu nayo muda mrefu.

15. Kuvaa mikanda oversize, unakuta mkanda mkubwa had uajikunja ukiwa kwenye luks au una buckle kubwa.

16. Kuvaa tshirts zilizokatwa mikono.

17. Kuvaa boshori.

18. Kukaa vijiweni bila kuwa na shughuli ya maana kufanya.

19. Kuwaza starehe muda wote, weekend ikifika utasikia 'mwana bata wapi?'

20. Kuhonga vimada huku wanao hawana viatu au uniform za shule zimechakaa kupitiliza!! Na mbaya zaidi unawalaza hadi njaa we unakula raha na vimada tu by Ligogoma

21. Kuendekeza michepuko ilhali umeoa tena mke mrembo kweli kweli by Ligogoma

22. Kutojiwekea malengo ya kiuchumi, unaishi tu kama ndege.

23. Kuacha mindevu hovyohovyo bila KUNYOA

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

MWANAMKE MCHARUKO ATIMULIWA UKUMBINI...KISA KUSHOBOKEA WAUME ZA WATU!

Haijakaa poa! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwimbaji ambaye ni Prezidaa wa Bendi ya Mikumi Sound, Joshua Malekela amelazimika kumtimua mwanamke mmoja ukumbini, kisa kikielezwa ni mcharuko. Tukio hilo la aina yake lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa Black Poiny uliopo maeneo ya Iringa Road, Msamvu mjini hapa ambapo bendi hiyo ilikuwa ikishusha burudani. Mlinzi akimuondoa mcharuko(jina halikufahamika) kutoka ukumbini.Kabla ya kutimuliwa, mwanamke huyo ambaye jina halikupatikana, alikuwa akicheza ovyo na kuparamia waume za watu.Pia kabla ya kutolewa, mwanamke huyo alionekana akikwidwa na shabiki wa bendi hiyo akimshutumu kujipendekeza kwa mumewe kwa kumlazimisha akacheze naye sebene huku akimwaga ‘lazi’ hadharani.

MASKINI KIJANA HUYU, ANUSURIKA KUUAWA KWA KUCHOMWA MOTO AKIDHANIWA NI MWIZI!

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard Osward (40) mkazi wa Tabata Segerea, hivi karibuni alinusurika kuuawa kwa kuchomwa moto na wananchi baada ya kuhisiwa kuwa mwizi alipokutwa alfajiri akiwa na mfuko ambao ndani yake kulikuwa na bomba, huko Segerea. Richard Osward aliyechomwa moto na watu wenye hasira kali akidhaniwa kuwa ni mwizi. Akizungumza kwa shida akiwa katika wodi namba 23 iliyomo ndani ya Jengo la Sewa Haji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Richard alisema tukio hilo lilimkuta akiwa ameongozana na rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Moses na kwamba walikuwa wakielekea Gerezani, Kariakoo ambako wanajishughulisha na ufundi wa magari.

DIAMOND AMTAJA MWIMBAJI KUTOKA TANZANIA ANAYEMKUBALI

Diamond Platnumz amemtaja Vanessa Mdee kama muimbaji anayemkubali zaidi na ambaye anaona atafika mbali zaidi.Akiongea , Diamond amesema hata jukwaani, Vanessa ni msanii anayejituma sana. “Unajua wasanii wa kike wote wa hapa nyumbani ninawakubali ila namkubali sana Vanessa.

POMBE NOMA SANA AISEE: TAZAMA ILIVYOMFANYA HUYU MDADA INAYESEMEKANA NI MKE WA MTU!

Huyu amenaswa na camera akiwa hoi bin taabani hajitambui kabisa maskini! Just imagine ni mkeo inakuaje na fikiria upande wa pili wa vijana wa mjini wakimkuta ni nini kitajiri! Kunywa kistaarabu!

ANGALIA MOTO ULIVYOTEKETEZA NYUMBA YA VICTOR COSTA, MKEWE ALIA UMASIKINI

Mke wa beki wa zamani wa Simba, Victor Costa Nampoka amelia na kusema umasikini unaendelea kuwamaliza hasa baada ya nyumba yao kuteketea na moto. Jasmin Badar ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba, amesema anaona anatumbukia tena kwenye vita ya kujikomboa baada ya nyumba hiyo eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam kuteketea.
“Umasikini huu jamani, kama unavyoiona, nyumba yote imeteketea, kweli inatia uchungu sana,” alisema Jasmini ambaye alishinda kwa kishindo kwenye uchaguzi wa Simba.
Masaibu hayo yameikuta familia ya Costa wakati akiwa mkoani Shinyanga na timu yake ya sasa ya Mwadui FC. Costa amesema chanzo cha moto huo ni kibatari kilichowashwa baada ya umeme kukatika na baadaye moto wa kibatari kushika kwenye pazia na kwa kuwa watu hawakuwepo ndani, moto ule ulisambaa. Costa aliongeza kuwa moto huo umeteketeza kila kitu kilichokuwa ndani ya nyumba na hakuna kilichosalimika.

CRD SALEHALLY.COM

MBEYA CITY YAZIPIGA BAO 'LAINII' SIMBA NA YANGA SC...CHEKI KITU HIKI!

Mbeya City wamezidi kupiga hatua kwenye vitu kadhaa ambavyo vingeweza kufanywa na klabu kongwe za Yanga na Simba. Sasa wamekuwa wakivifanya wao kama vile utaratibu wa kuuza jezi ambao unaiwezesha klabu kuingiza fedha nyingi. Safari hii wametengeneza bahasha ambazo zina nembo ya klabu na mdhamini wao mkuu. Huenda hii inaweza isiwe ni biashara au faida, lakini ni sehemu ya kuonyesha kiasi gani wanaidhamini taasisi yao. Si taasisi za kiserikali au binafsi nje ya mpira ndiyo zinaweza kufanya hivyo pekee. Hata Mbeya City.

UNAAMBIWA ILI NIPIGO LINGINE KUBWA SANA WALIOPATA ARSENAL MSIMU HUU

KLABU ya Arsenal imepata pigo baada ya kiungo wake, Mesut Ozil kuumia na anatakiwa nje kwa kipidi chote kilichobaki kumaliza mwaka 2014. Kiungo huyo alikwenda kufanyiwa vipimo vya MRI katika goti lake na Chama cha Soka Ujerumani kimethibitisha atakuwa nje kwa miezi mitatu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hakufanya mazoezi na timu yake ya taifa ya Ujerumani mjini Frankfurt baada ya kuanza kulalamika juu ya hali yake. Mesut Ozil atakuwa nje kwa kipindi chote kilichobaki mwaka 2014 baada ya Chama cha Soka Ujerumani kuthibitisha kuumia kwake goti Ozil hajaonyesha dalili kubwa za maumivu katika miezi ya karibuni na amecheza mechi tisa msimu huu, akifunga bao moja. Taarifa ya Arsenal imesema: "Ozil alilalamika kuwa na maumivu ya goti la kushoto baada ya mechi na klabu ikakishauri Chama cha Soka Ujerumani kumfanyia uchunguzi atakapojiunga na kikosi cha timu ya taifa. "Klabu itamfanyia uchunguzi wa kina na ni mapema sana kusema Ozil atakuwa nje kwa muda mrefu kiasi gani". Ozil, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 42.5 mwaka jana, amekuwa akikandiwa kwa kucheza chini ya kiwango akiwa na jezi ya Arsenal. Habari za kuumia kwake zinazokuja mwezi wa pili ndani ya msimu mpya, ni pigo kwa kochaa Arsene Wenger ambaye sasa idadi ya majeruhi inaongezeka katika timu yake, Ozil akkungana na Aaron Ramsey, Mathieu Debuchy, Olivier Giroud pamoja na Mikel Arteta.

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

HALIMA MDEE NA WENZAKE WAPATA DHAMANA

Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee. Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wenzake 8 leo wamepata dhamana katika Mahakama ya Kisutu, Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014. Siku ya jana washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Kaluyenda na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu, Kangola aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi, Penina Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari. Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf iliyowataka watawanyike. Shtaka la pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika kinyume na sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

Wednesday, October 08, 2014

Vitu 8 vya kufanya kila asubuhi ili uweze kufikia Mafanikio kimaisha

Haya Msomaji wa mdadisiblog sikiliza nikuambie ni nini hasa mambo ya kufanya kila asubuhi ili uweze kupata mafanikio zaidi kimaisha. Binafsi hivi karibuni nimesoma makala katika moja ya magazeti nnayoyapenda na yalionyesha orodha za watu waliofanikiwa na wanachokifanya mara kwa mara. Kisha, nikaanza kutafiti zaidi kidogo na kupata mambo kadhaa muhimu ambayo yaliendana kwa watu hao. Hapa kwa haraka nitakushirikisha vitu  8 vya kufanya kila asubuhi:-

1. Amka Mapema

Jambo la kwanza la kufanya ukitaka kufanikiwa ni kuhakikisha unaamka mapema sana asubuhi. Watu waliofanikiwa huamka  kuanzia saa 10:30 hadi 11:30 asubuhi. Hapa nawalenga wale wanaoamka saa mbili asubuhi hadi saa tatu.Ukiamka mapema utaweza kupata kifungua kinywa mapema saa 01:30 asubuhi na kuwa na siku ndefu. Watu wengi wenye mafanikio huamka mapema.

2. Fanya Mazoezi

Mbali na kuamka mapema kufanya mazoezi ni jambo la muhimu pia na sio tu kufanya mazoezi bali kufanya mazoezi mapema asubuhi. Watu waliofanikiwa hufanya mazoezi asubuhi si kwa kupunguza miili yao tu bali kujipa afya ya akili katika kupambana na mambo aliyopanga kufanya katika siku hiyo.

3. Pata Kifungua kinywa (Breakfast)

Wote tunajua breakfast ni kitu muhimu ila je, Unajua kama watu waliofanikiwa huhakikisha wanapata breakfast kama jambo la msingi sana? Siongelei chai na maandazi nnaongelea chai nzito yenye vitu kama matunda au juice pamoja na maziwa/mayai ili kupata protini. Hii ni zawadi kubwa unayoweza kuupatia ubongo wako ili kuweza kuurahisishia kazi.

Hakikisha unapata breakfast masaa machache baada ya kuamka na kama jana yake usiku ulichelewa kula basi haishauriwi upate breakfast mapema.

4. Jipatie muda wa kuwa katika ukimywa

Sababu kubwa ya kuamka mapema ni kujipatia wasaa wa kuwa katika hali ya ukimywa. Unapoamka na kufanya mazoezi ni kujipa muda tosha na kuupa ubongo wako fursa ya kuwaza kuhusu mambo yako tu wala si kelele za watoto ndani ya nyumba au watu wengine.

Fikiria kuhusu majukumu yako ya siku hiyo na vitu unavyohitaji kufanya na kama itakusaidia unaweza kuandika chini. Kila siku zinapoenda utajikuta unazoea wasaa huu wa kuwa kimya hata kujiongezea muda wa jambo hili.

5.  Jipange

Kitu kingine ambacho kinafanana kwa watu waliofanikiwa ni pale wanapojipanga jinsi watavyoitumia siku yao. Kila asubuhi panga jinsi ya kutumia siku yako anza na kupanga vifaa vyako vya kazi, panga muda utaotumia kufanya kila jambo ikiwemo kula chakula cha mchana. Tandika kitanda chako na acha nyumba yako katika hali ya usafi. Kila mara unapoacha kufanya baadhi ya mambo haya taarifa za kukuletea mawazo (stress) hutumwa katika ubongo wako.
Ukijipanga utafurahia siku yako na kufanya mambo mengi zaidi kwa umakini unaohitajika.

6.  Achana na mambo ya siku iliyopita.

Kitu muhimu kila asubuhi ni kutoamka ukijilaumu kwa maamuzi na vitu ulivyovikosa jana. Kama uligombana na mtu jana, au mwajiri wako alisema kitu cha kukuudhi, au haukupata ile nyongeza ya mshahara uliyotarajia. Acha mambo ya aina hii. Kama ulimkosea mtu, hakikisha unamuomba msamaha. Achana na yaliyopita na weka akili yako kwa mambo ya leo.

Kila mtu aliyefanikiwa anaianza siku yake kwa kuwa na tabia mpya, mipango mipya na nguvu mpya na sio kujilaumu. Tabia hii itakupa uwezo wa kufanikiwa kwa siku husika.

7. Kuwa na Imani

Anza siku kwa kujitamkia maneno ya kujikumbusha kuwa una uwezo wa kuimaliza siku hii kwa kuchukua fursa zote zitakazo jitokeza, kufanya maamuzi sahihi na kuwa mvumilivu. Fanya Sara kulingana na Imani yako kwa Mungu.

8. Soma

Ikiwa ni habari kwenye gazeti, soma barua pepe, au soma kurasa chache za kitabu unachokipenda. Kusoma asubuhi ni kuzuri kwa mazoezi ya akili yako.

Nikki Mbishi awashirikisha Jaydee, Songa na One kwenye ‘Kupanda na Kushuka’

Rapper wa Tamaduni Muzik, Nikki Mbishi anatarajia kuachia wimbo mpya ‘Kupanda na Kushuka’ aliowashirikisha Lady Jaydee, Songa na One the Incredible. Nikki amesema ameamua kuwashirikisha wasanii hao ili kupata kitu tofauti kama muziki unavyohitaji. “Unajua muziki sometimes unahitaji vitu fulani fulani ili uwe mzuri zaidi na hii ni kawaida ya muziki ulivyo. Kwahiyo tukaona tukifanya kitu kwa pamoja kitakuwa safi tukaingia studio za Man Walter tukafanya wimbo ‘Kupanda na Kushuka’, ni wimbo ambao unaelezea maisha ya kawaida kupanda na kushuka kwa maisha, leo umepata kesho umelala njaa lakini ni maisha. Wimbo utatoka hivi karibuni pamoja na video,” alisema Mbishi.