Thursday, October 09, 2014
 |
| Stori: Hamida Hassan na Imelda Mtema wa
Global Publishers
Mastaa wa filamu Bongo, Blandina Chagula
‘Johari’ na Chuchu Hans ambao wamekuwa
katika bifu kwa muda mrefu kutokana na
uhusiano wa kimapenzi na Vincent Kigosi ‘Ray’,
hivi karibuni nusu wazichape kwa mara nyingine
baada ya kurushiana matusi mazito ya nguoni |
 |
| Tukio hilo lilijiri juzikati katika hoteli moja iliyopo
Sinza jijini Dar.
Chanzo cha uhakika kilichokuwa eneo la tukio
kinavujisha kwamba, Ray alifika katika hoteli hiyo
akiwa katika teksi na aliandamana na Chuchu.
Inadaiwa Ray alifika hotelini hapo kwa ajili ya
kuonana na mkurugenzi mwenza wa kampuni yao
ya RJ, Johari, ambaye kwa wakati huo alikuwa
akisimamia kambi ya projekti yao mpya.
Baada ya Ray kushuka kwenye teksi na kuingia
ndani ya hoteli hiyo huku Chuchu naye akishuka
kwenye na kusimama nje akimwangalia
mwandani wake anavyomsogelea Johari ambaye
siku za nyuma alikuwa ndiye mwandani wake.
Kitendo cha Chuchu kutokeza kuonesha alikuwa
ameandamana na mkali huyo wa filamu
kilimchukiza Johari ambaye kwa sauti iliyosikika
vyema, alimuuliza Ray kwa nini alikwenda akiwa
ameongozana na ‘malaya’ wake. |
 |
| “Matusi yale yalimkera sana Chuchu, naye
aliamua kumrudishia hali iliyosababisha kutokea
kwa tafrani kubwa kwani watu walianza kujazana
na kuwazuia wasichapane,” kilisema chanzo
chetu.
Baada ya habari hii kutua mezani, mapaparazi
wetu waliingia kazini ili kuujua ukweli, mtu wa
kwanza kuzungumza naye ni Johari ambaye siku
za nyuma aliwahi kuzichapa na mpinzani wake
huyo wakati akilitetea penzi lake lililokuwa
likiyumba.
Johari alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai
kuwa mwigizaji huyo alikwenda kambini kwake
kufanya fujo ambazo hata hivyo alishindwa
kufafanua.
Kwa upande wake, Chuchu alipoulizwa alisema:
“Nimemvumilia sana Johari, amekuwa akinitukana
kila kukicha nanyamaza, sasa nimechoka na
kibaya zaidi siku hiyo alinitukania mama yangu,
nimekuwa nikimvumilia kwa sababu alikuwa
akinitukana mimi, sasa kumuingiza mama kwenye
ugomvi wetu siwezi kumvumilia kamwe,” alisema
Chuchu. |
0 comments:
Post a Comment