Thursday, October 09, 2014
 |
| Haijakaa poa! Katika hali isiyokuwa ya
kawaida, mwimbaji ambaye ni Prezidaa wa
Bendi ya Mikumi Sound, Joshua Malekela
amelazimika kumtimua mwanamke mmoja
ukumbini, kisa kikielezwa ni mcharuko.
Tukio hilo la aina yake lilijiri wikiendi
iliyopita kwenye Ukumbi wa Black Poiny
uliopo maeneo ya Iringa Road, Msamvu
mjini hapa ambapo bendi hiyo ilikuwa
ikishusha burudani.
Mlinzi akimuondoa mcharuko(jina
halikufahamika) kutoka ukumbini.Kabla
ya kutimuliwa, mwanamke huyo ambaye
jina halikupatikana, alikuwa akicheza ovyo
na kuparamia waume za watu.Pia kabla ya
kutolewa, mwanamke huyo alionekana
akikwidwa na shabiki wa bendi hiyo
akimshutumu kujipendekeza kwa mumewe
kwa kumlazimisha akacheze naye sebene
huku akimwaga ‘lazi’ hadharani. |
0 comments:
Post a Comment