Thursday, October 09, 2014
 |
| Kama kila siku huwa unaingia facebook,
whatsapp au instagram inawezekana ukawa
ulikutana na hii picha ya Askari Polisi ambao
walipigwa picha wakiwa wanakiss wakiwa
ndani ya sare za jeshi hilo.
Sasa taarifa mpya iliyotoka baada ya hii picha
kuzidi kusambaa ni kwamba Jeshi la Polisi
Kagera limechukua maamuzi ya kuwafukuza
kazi askari hawa wawili pamoja na mwingine
mmoja ambae ndio aliipiga hii picha kupitia
simu yake ya mkononi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Henry Mwaibambe
amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma
Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788,PC
Fadhili Linga mwenye namba G 2122 na PC
Veronica Nazaremo Mdeme na wote walikuwa
askari wa kikosi cha usalama barabarani
wilayani Missenyi. |
 |
| Kamanda Mwaibambe amezungumza na ITV na
kusema askari hao walitenda kosa hilo la
fedhea kwa kupiga picha kinyume na maadili
ya jeshi hilo mwaka 2012 wakiwa kazini na
kwamba PC Fadhili ndiye aliyehusika na kupiga
picha hizo kwa kutumia simu yake ya mkononi
na kuituma katika mitandao mbalimbali ya
kijamii kitendo ambacho ni kinyume cha
maadili kwa sababu mbalimbali.
Mwaibambe amekiri kuwa picha husika
inayoonekana kwenye mitandao ni picha halisi
ambayo haijachakachuliwa hivyo ni wazi kila
askari kujua maadili ya kijeshi yapo kisheria na
askari yeyote anafundishwa namna ya kuishi
katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polisi. |
0 comments:
Post a Comment