 |
| Na Princess Asia, JOHANNESBURG
KOCHA Mzungu anawanoa makipa wa
Simba SC katika kambi yao, Afrika Kusini
wakati kocha wa makipa wa Oman, Choke
Abeid anatarajiwa kutua wakati wowote
kuanza rasmi kazi ya ‘kuwafua’ makipa wa
timu hiyo, baada ya kutupiwa virago kwa
Iddi Pazi ‘Father’.
Pazi aliachwa Dar es Salaam wakati Simba
SC inaondoka jana na ingawa hajaambiwa
chochote, lakini ndiyo ametimuliwa- baada
ya uongozi kuamini viwango vya makipa
wao vimeshuka chini yake.
Simba SC imeanza mazoezi leo kwenye
viwanja vya
Hoteli ya Eden Vale Petra mjini
Johannesburg walipofikia na keshokutwa
watacheza mchezo wa kirafiki na wenyeji
Orlando Pirates mjini Johannesburg.
Simba ipo Afrika Kusini tangu jana kwa ajili
ya maandalizi yake ya mechi dhidi ya
watani wao wa jadi, Yanga SC, Oktoba 18,
mwaka huu Dar e Salaam.
Suleiman Matola aliyekuwa kocha Msaidizi
tangu wakati wa Mcroatia, Zdravko
Logarusic anaendelea kuwa Msaidizi wa
Mzambia, Patrick Phiri wakati Meneja
anaendelea Nico Nyagawa.
Katika mchezo na Pirates, Simba SC
itawakosa wachezaji wake walio timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Uganda,
The Cranes- ambao wanatarajiwa kujiunga
na wenao kuanzia Jumatatu.
Hata hivyo, mshambuliaji Mganda,
Emmanuel Okwi aliyekwenda kujiunga na
The Cranes yeye hatakwenda kabisa Afrika
Kusini, kwa sababu timu yake hiyo ya taifa
itakuwa na mechi ya kufuzu AFCON katikati
ya wiki.
Wachezaji wa Simba SC walioko Stars ni;
mabeki Miraji Adam na Joram Mgeveke na
viungo Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said
Ndemla na Haruna Chanongo ambao wote
watakwenda Afrika Kusini Jumatatu.
Simba SC itakuwa ikifanya mazoezi ya
nguvu hadi Oktoba 17 itakaporejea Dar es
Salaam, ikiwa ni siku moja kabla ya mechi
na watani.
Baada ya sare tatu mfululizo katika mechi
zake tatu za awali, 2-2 na Coastal Union,
1-1 mara mbili na Polisi Moro na Stand
United, Simba SC imepania kushinda mechi
ya kwanza Oktoba 18. |

 |
| Mzungu akiwanoa makipa wa Simba leo |
 |
| Simba SC wakijifua Afrika Kusini leo |
KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment