Thursday, October 09, 2014
 |
| MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la
Richard Osward (40) mkazi wa Tabata
Segerea, hivi karibuni alinusurika kuuawa
kwa kuchomwa moto na wananchi baada
ya kuhisiwa kuwa mwizi alipokutwa
alfajiri akiwa na mfuko ambao ndani yake
kulikuwa na bomba, huko Segerea.
Richard Osward aliyechomwa moto na
watu wenye hasira kali akidhaniwa kuwa
ni mwizi. Akizungumza kwa shida akiwa
katika wodi namba 23 iliyomo ndani ya
Jengo la Sewa Haji katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Richard alisema tukio
hilo lilimkuta akiwa ameongozana na
rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Moses na
kwamba walikuwa wakielekea Gerezani,
Kariakoo ambako wanajishughulisha na
ufundi wa magari. |
0 comments:
Post a Comment