Friday, October 10, 2014

ROY KEANE AMTANDIKA FERGUSON, ASEMA AMEPATA MAMILIONI, JUKWAA, SANAMU LAKINI…

Vita ya maneno kati ya Roy Keane na Alex Ferguson sasa inazidi kuchanja mbuga.
Keane aliyekuwa nahodha wa Manchester United iliyopata mafanikio makubwa chini ya Ferguson, amesema kocha huyo ni muongo. Keane amesema hayo wakati akizizundua kitabu chake kipya cha Second Half. Hajapoteza maneno au kupepesa baada ya kusema aliamua kitabu hicho baada ya kusoma maneno mengi ya uongo ya Ferguson kwenye kitabu chake kilichochapishwa mwaka jana.
“Ajabu kabisa, Ferguson amepata mamilioni, amepata jukwaa na sanamu kwenye Uwanja wa Old Trafford, hayo yote ni mafanikio. “Sasa ni ajabu sana kama anafikia hatua ya kuwasema maneno mabaya watu waliomsaidia kupata hayo mafanikio. “Kwangu nimeona si mambo sahihi, hapaswi kufanya hivyo na hakuwa sahihi. “Hakika sikuwa nina mpango wa kutoa kitabu, lakini baada kitabu chake niliona lazima nifanye hivyo,” alisema Keane ambaye ni kocha msaidizi wa Aston Villa. Katika kitabu hicho cha Feguson (AMBACHO HUTAFSIRIWA KWA KISWAHILI NA GAZETI LA MICHEZO LA CHAMPIONI), ameeleza namna Keane alivyokuwa mkorofi na asiyewakubali wachezaji vijana.
Ameeleza kuwa Keane hakupenda wengine wafanikiwe na alijisahau baada ya yeye kumpa uhuru. Pia alieleza na kukiponda kitendo chake cha kuwasakama wachezaji wa Man United kwenye mahojiano yake na runinga ya klabu hiyo ya MUTV. Lakini Keane amesema yote hayo ni uzushi mtupu na ameyajibu kwenye kitabu chake hicho cha Second Half.

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

0 comments:

Post a Comment