Sunday, August 31, 2014

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA LEO JUMAPILI

Chelsea wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa QPR Loic Remy, 27, baada ya Fernando Torres, 30, kwenda AC Milan (Telegraph), kiungo wa Manchester United Tom Cleverly, 25, anafikiria kwenda Aston Villa kwa pauni milioni 7, baada ya kuzungumza na nahodha wa zamani wa Man Utd Roy Keane ambaye sasa ni meneja msaidizi Villa Park (Daily Mirror), meneja mpya wa Crystal Palace Neil Warnock anataka kumchukua beki wa QPR Armand Traore, 24, kwa pauni milioni 2.5 (Sun), Arsenal wamepata matumaini makubwa ya kumchukua winga Alessio Cerci, 27, baada ya rais wa Torino, Urbano Cairo kusema mchezaji huyo atauzwa kwa bei stahiki (Daily Star), Manchester United wanataka kumsajili beki Timothy Fosu Mensah, 16, kutoka Ajax (Daily Express), uhamisho wa beki Marcos Rojo, 24, kwenda Manchester United uko hatarini kutokana na kutopata bado kibali cha kufanya kazi na pia wakala wa tatu wa uhamisho aliyepo kwenye mkataba wake (Sun), West Ham wanakaribia kukamilisha uhamisho wa Alex Song, 26, kutoka Barcelona kwa mkopo (Daily Mail), Birmingham City wanataka kumchukua Hatem Ben Arfa, 27, kutoka Newcastle kwa mkopo (Newcastle Chronicle), Manchester United wanahitaji kutoa pauni milioni 5 zaidi kuweza kumsajili Arturo Vidal kutoka Juventus huku klabu hizo mbili zikiendelea na mazungumzo kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu (Tuttosport), Benfica wanajiandaa kutoa pauni milioni 7.9 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Joel Campbell (O Jogo), Manchester United wamekubali kutoa pauni milioni 14.2 na Ajax kumchukua Daley Blind (De Telegraaf), Chelsea wako tayari kuongeza juhudi kumfuatilia mshambuliaji wa Roma Mattia Destro kufuatia kuondoka kwa Fernando Torres (Daily Mirror). Zimesalia moja mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu.

Baada ya kuondoka kwa Torres – huyu ndio mshambuliaji mpya aliyesajiliwa na Chelsea

Usiku wa jana mshambuliaji wa kimataifa wa Spain Fernando Torres alikamilisha usajili wake wa mkopo wa miaka miwili kutoka Chelsea kwenda AC Milan. Huku yakiwa hajapita hata masaa 24 tangu Torres aondoke, Jose Mourinho amekamilisha usajili wa mbadala wa Torres, mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Loic Remy. Remy ambaye alifeli vipimo vya afya alipokuwa akikaribia kujiunga na Liverpool mwanzoni mwa dirisha la usajili, amejiunga na Chelsea kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 10 kutoka QPR. Remy anachukua nafasi ya Torres na kuungana na Didier Drogba katika kumsaidia Diego Costa. Wakati huo huo Alex Song amejiunga na West Ham kwa mkopo kutoka FC Barcelona.

Lady Jaydee ajibu habari ya gazeti la udaku kuwa na uhusiano na ‘Dogo Dogo’

Lady Jaydee ameamua kujibu habari iliyoandikwa kwenye gazeti la udaku la Risasi kuhusu kuwa na uhusiano na aliyewahi kuwa mtuma salamu maarufu kwenye redio, Meddy Ahmed aka ‘Mtoto wa Vitoto’. Kwenye habari hiyo, Risasi wanadai kuwa Jaydee ambaye anadaiwa kuachana na mume wake Gadner G Habash ameonekana mara kadhaa na Mtoto wa Vitoto na kwamba amewahi kuonekana akiwa na gari lake. Kupitia Instagram, Jaydee ameandika: Kuna habari za kuniudhi Ila hii imenichekesha. Kwahiyo mtoto wa vitoto ndio bwana angu???? Basi sawa nashukuru naona mmenianzia tena sasa picha za February Na nilizi post mwenyewe humu insta leo ndio mmeziona? Ukweli mnaujua mmeamua tu kuzingua ,,, wangapi wameshapiga picha na hiyo Range? Duuuh! !!!!! Shkamoooni Moyo wangu chuma. Pigeni mawe mpk mchoke Kama ambavyo mmekuwa mkifanya miaka yote na bado nipo hapa hapa.”

Saturday, August 30, 2014

EPL: Matokeo ya Chelsea vs Everton yapo hapa

Mechi ya mwisho ya Premier League leo hii ilikuwa kati ya vijana wa Jose Mourinho Chelsea dhidi ya vijana wa Roberto Martinez Everton. Mchezo huo wa kuvutia uliopigwa kwenye dimba la Goodson Park umeisha kwa Chelsea kupata ushindi mzito na mkubwa kuliko wowote kwenye premier league msimu huu. Magoli ya mapema ya Diego Costa na Ivanovic yaliwaweka Chelsea mbele kwa 2-1 mpaka timu zilipoenda mapumziko – Kevin Mirallas aliifungia Everton goli la kwanza dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kuisha. Kipindi cha pili Everton walirudi kwa kasi wakijaribu kusawazisha lakini kwenyw dakika ya 67, Coleman akajifunga na kuiongezea Chelsea uongozi, lakini Naismith akapunguza pengo dakika 2 baadae, kabla ya Nemanja Matic kuongeza goli la 4 kwa Chelsea. Samuel Eto’o akicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Everton akafunga bao la 3 dk 76, lakini dakika 2 baadae Ramirez akapiga mkwaju wa 5 na Diego Costa kwa mara nyingine tena akafunga mahesabu kwa Chelsea kwa kufunga goli la 6 kwenye dakika 90. Hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa yakisomeka 6-3.

Baada ya kuondoka kwa Torres – huyu ndio mshambuliaji mpya aliyesajiliwa na Chelsea

Usiku wa jana mshambuliaji wa kimataifa wa Spain Fernando Torres alikamilisha usajili wake wa mkopo wa miaka miwili kutoka Chelsea kwenda AC Milan. Huku yakiwa hajapita hata masaa 24 tangu Torres aondoke, Jose Mourinho amekamilisha usajili wa mbadala wa Torres, mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Loic Remy. Remy ambaye alifeli vipimo vya afya alipokuwa akikaribia kujiunga na Liverpool mwanzoni mwa dirisha la usajili, amejiunga na Chelsea kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 10 kutoka QPR. Remy anachukua nafasi ya Torres na kuungana na Didier Drogba katika kumsaidia Diego Costa. Wakati huo huo Alex Song amejiunga na West Ham kwa mkopo kutoka FC Barcelona.

Posted via Blogaway


Posted via Blogaway

MATOKEO YA MECHI YA MAN CITY vs STOKE CITY HAYA HAPA

Mabingwa wa England, Manchester City wameanza kuonja joto ya jiwe wa Ligi Kuu England baada ya leo kulala kwa bao 1-0. Stoke City ambao waliinyanyasa Man City msimu uliopita, leo ‘wameifanyia mbaya’ kwa kuichapa kwa bao 1-0 tu. Mame Diouf ndiye alikuwa shujaa wa Stoke City waliokuwa nyumbani baada ya kuwapangua viungo na mabeki wa wageni wao kabla ya kupachika bao akipiga mpira uliompita kipa Joe Hart katikati ya miguu yake, unaweza kusema topo. Juhudi za Man City kutaka kuchomoa 'kashfa' hiyo ziligonga mwamba.

Posted via Blogaway

FERGUSON LEO AMEUDHIKA MNO MAN UNITED MECHI YA TATU HAKUNA USHINDI

Maudhi matupu: Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson (mbeke) akiwa na David Gill na Sir Bobby Charlton wakitazama mchezo wa timu hiyo leo ikilazimishwa sare ya 0-0 na Burnley. United imekuwa ikisuasua tangu kustaafu kwa Ferguson mwaka jana. Makocha wawili wamekwishapewa timu, David Moyes aliyetimuliwa mwishoni mwa msimu uliopita na Ryan Giggs akakaimu kumalizia msimu, kabla ya msimu huu kuajiriwa Louis Van Gaal ambaye leo amefikisha mechi ya tatu bila ushindi, sare mbili ugenini, nyingine 1-1 na Sunderland na kufungwa moja nyumbani na Swansea City 2-1.

Posted via Blogaway

AKILI ZA USIKU:KAMA HUYU NI MDOGO WAKO AU NDUGU YAKO LEO HII UNGEMWAMBIA NINI KUHUSU TABIA HII

BARUA YA FIFA ILIYOMPELEKA OKWI YANGA HII HAPA, JE INAWEZA KUMPELEKA SIMBA PIA?

HII ILIKUWA NI BARUA KUTOKA FIFA KWENDA TFF AMBAYO ILIKUWA INAENDELEA NAMNA AMBAVYO TFF INAVYOWEZA KULISHUGHULIKIA SUALA LA OKWI HUKU IKIELEZA ANAWEZA KUCHEZA YANGA KWA KUWA SUALA LAKE LA MADAI DHIDI YA ETOILE DU SAHEL NI TOFAUTI. KUPITIA BARUA HII, TFF IKAMUIDHINISHA OKWI KUCHEZA YANGA WAKATI HUO SIMBA ILIKUWA IKIENDELEA KUIDAI ETOILE DOLA 300,000 ZA MAUZO. SWALI, FIFA INAWEZA KUINGILIA SUALA HILI KAMA YANGA ITASHITAKI NA JE, ITACHUKUA UAMUZU WA KUMUIDHINISHA OKWI ACHEZE SIMBA WAKATI ANAENDELEA KUDAIANA NA YANGA AMBAYO INAMDAI NA YEYE AMEELEZA KUWA ANAIDA?

BAADA YA MAN U KUMSAJIRI DI MARIA HUU NDIO USAJILI UNAOFUATA

Kilabu ya Manchester United ya Uingereza imekubaliana na kilabu ya Uholanzi Ajax Amsterdam kutoa kitita cha pauni millioni 13.8 kumnunua mlinzi wa timu hiyo Daley Blind.

Blind ambaye ana umri wa miaka 24 alikuwa katika kikosi cha Kombe la dunia cha Uholanzi chini ya mkufunzi Louis Van Gaal. Anaweza kucheza kama beki wa kushoto pamoja na ngome ya kati ya ulinzi.

Iwapo makubaliano hayo yatatiwa sahihi, huyo atakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na kilabu hiyo.

Kilabu ya Manchester tayari imetumia zaidi ya pauni millioni 130 katika msimu huu pamoja na kuvunja rekodi ya Uingereza kwa kusajili Angel Di Maria kwa kitita cha pauni 59.7 kutoa Real Madrid.

Old Trafford pia imemnunua beki wa kushoto Luke Shaw,mchezaji wa kungo cha kati Ander Herrera na Marcos Rojo.


Posted via Blogaway

MSOME VIZURI MANJI ALIVYOLONGA KUHUSU SUALA LA OKWI

Suala la Emmanuel Okwi kutangaza kuwa Yanga imevunja mkataba wake na sasa ataitumikia Simba, limezua sekeseke na sasa ni mtafutano kila kona, kama ni vita sasa hii ndiyo inaanza kukolea. Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, amefunguka kuwa wametoa siku saba kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoa majibu sahihi juu ya Simba kumtangaza Okwi kuwa mchezaji wao wakati bado kuna kesi inayoendelea baina ya Yanga na Okwi. Kuonyesha kuwa wapo ‘serious’ na hicho wanachokifanya, Manji amesema kuwa ikiwa TFF haitatoa majibu ya kueleweka kwao ndani ya siku saba, basi moja kwa moja watatua katika Shirikisho la Soka la Afrika (Caf), ikiwa pia hapo hakutaeleweka ndani ya siku saba, basi wataelekea Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa ajili ya suala hilo. Manji alionekana kutokuwa na utani kwenye kauli zake, alionekana kukerwa na kitendo cha Okwi kutua Simba na kusema kuwa Yanga imevunja mkataba wake, ndiyo maana ameamua kwenda kuichezea Simba. Waipa siku saba TFF “Tumepeleka barua TFF, leo (Ijumaa) asubuhi kutoa malalamiko kuhusiana na Simba kumsainisha Okwi wakijua wazi kuwa ana mkataba na sisi wa miaka miwili. “Hii ni barua yetu ya tatu baada ya mbili tulizopeleka mwezi wa tano na wa saba juu ya malalamiko kwa Okwi kutoitumikia Yanga kutofanyiwa kazi. Kutinga Fifa “Tumetoa siku saba kwa TFF kulitolea ufafanuzi suala hili na kutoa maamuzi juu ya kilichofanyika na iwapo maamuzi hayatatolewa ndani ya muda huo, tunatarajia kuwasilisha malalamiko yetu Fifa na ikishindikana tutaliwasilisha katika Mahakama ya Michezo nchini Uswisi (CAS). Simba hawajui sheria za soka “Viongozi wa Simba wameshindwa kufanya suala la uungwana kwa kufuata sheria za mpira kama zinavyoeleweka, wangekuja kuwauliza kwani hatukatai kuuza wachezaji ila sheria ifuatwe. “Mfano mzuri kina Frank Domayo na Didier Kavumbagu wamesajiliwa, hatujalalamika kwa kuwa walifuata utaratibu unaotakiwa. “Upande wangu naona ni jambo la kawaida kushirikiana, hata mimi nilimpongeza (Evans) Aveva alipochaguliwa kuwa rais kwani ndiyo mambo ya mpira yalivyo. Waongeza dau la fidia “Dau la awali kabla ya kusaini Simba tulitaka alipe fidia ya dola 200,000 (Sh milioni 320) lakini baada ya kuamka leo tumeongeza dola 500,000 (Sh milioni 800), kwa hiyo jumla ni dola 700,000 (Sh bilioni 1.12). Hii tutawadai Simba na Okwi mwenyewe. Wataka Okwi afungiwe maisha “Tumepeleka malalamiko TFF ikiwezekana mchezaji huyo afungiwe maisha, pamoja na wakala wake kutoshiriki masuala ya soka hapa Tanzania kutokana na ukiukwaji wa sheria alioufanya ikiwa ni wazi kuwa bado ana mkataba na klabu yake ya awali. Apendekeza Simba ishushwe daraja “Kutokana na kitendo walichokifanya Simba wasinione mbaya iwapo timu itashushwa daraja kutokana na kumsajili mchezaji aliyekuwa na mkataba kwa kutofuata sheria, iwapo walikuwa wanahitaji kumnunua wangekuja na kuzungumza nasi. “Kwani sisi huwa tunaachana vizuri na wachezaji wetu, mfano mzuri Fred Mbuna na Shadrack Nsajigwa ambaye kwa sasa amerudi kuja kufundisha Yanga, hii ni kutokana na kuachana vizuri. Atishia kuinunua Simba “Mimi nina uwezo wa kununua wachezaji wote wa Simba na nikawalipa mshahara na jambo hilo naliweza, ila tunachoangalia ni kufuata kanuni na sheria za soka. “Kwani hata sisi tungeweza kumchukua (Amissi) Tambwe kutokana na kumuona ni mchezaji mzuri na kumsajili Yanga lakini hatuwezi kufanya hivyo kwa kuwa tunatambua sheria na mchezaji huyo ana mkataba ambao tunauheshimu. “Hata hivyo Klabu ya Yanga ina mfuko mrefu kuliko Simba. Jina lake limo katika usajili TFF “Tumewasilisha majina sita ya wachezaji wa kimataifa akiwemo Okwi kwa kuwa hatukupata majibu yetu mapema kutoka TFF. “Iwapo wangetupatia taarifa mapema tungeamua kumuacha mchezaji mmoja, hata Jaja na kumwambia akakae kwa miezi sita kisha angerudi tena kucheza. “Siyo kwamba tunalalamika kuwa tunamhitaji mchezaji huyo kwani kuna wachezaji wengi na tunaweza kwenda kusajili sehemu mbalimbali duniani ila tunataka sheria ifuatwe. Okwi ataka kukutana na Manji “Okwi alikuja ofisi kwangu na kutaka kuonana na mimi lakini nikawa bize akaambiwa na katibu muhtasi wangu kuwa atapangiwa siku, kweli akapangiwa siku, hakutokea, akapigiwa simu hakupokea lakini alitumiwa meseji hakuweza kujibu wala kutokea tena. Akana kuvunja mkataba “Hatujawahi kuvunja mikataba na wachezaji wa Simba, kwani hata Juma Kaseja tulisubiri mkataba uishe ndiyo tukaingia naye mkataba… “…Ndiyo maana tulimsajili pia Kelvin Yondani baada ya mkataba wake kumalizika, hatukuvunja sheria. Waunda kamati ya sheria “Kesho (leo) tunatarajia kutangaza kamati yetu mpya ya sheria ambapo ilikuwa ni mpango wa muda mrefu, kwani tumeona ni muhimu kuwa na kamati hii na isifikiriwe kuwa imetokana na suala la Okwi,” alisema Manji.

Posted via Blogaway

LOVELY PHOTO:KAJALA AKIWA NA MTOTO WALE PAULA....SO BWITIFU!!!

Hii ndiyo siku Vanessa alipofunguka, kuhusu mahusiano yake yakimapenzi.

Msanii wa kike ambaye anazidi ku-make headlines hasa kwa historia yake ya kila nyimbo pale anapoi-release lazima ifanye vizuri, maarufu kama Vanessa Mdee au Veemoney finaly afunguka kuhusu maisha yake yakimahusiano. Mtu kama Vanessa ambaye ni maarufu kama ilivyo kwa wasanii wengi wa bongo, upande wake wa pili hasa wa kimahusiano umekuwa na utata, na kuzidi kuwafanya mashabiki wengi wazidi kujiuliza ni nani haswa anatoka na Vanessa mdee. Akiwa anahojiwa hapa utamsikia mwenyewe akiongelea rumors nyingi zilizowahi kusambaa kuwa yeye anatoka na baadhi ya watu maarufu na kufunguka kuwa, mara nyingi watu wanakuwa wanadadisi vitu, hasa pale wasipojuamwelekeo wako kwenye jambo fulani, hivyo kumfanya kila aonekanaye naye kuwa na ukaribu, kudhaniwa kuwa ndiye anayetoka naye. Msikilize hapa vanesa akipigwa swali lakizushi ndani ya studio za cocacola.

Vibe


Posted via Blogaway

wakati mkisubiria ya Diamond na Wema, huko Hollywood kimeshanuka.

Wakati watu wakizidi kusubiria tukio la kihistoria kwenye sanaa ya Bongo fleva na bongo movie, ndoa kati ya Diamond Platnumz na Wema Sepetu kufunga ndoa, huko Hollywood hiki ndicho kilichojiri. Ni baada ya miaka tisa ya mahusiano hatimaye imekuwa, huko hollywood weekend hii hii haya ndio yaliyo-make headlines, ni harusi kati ya ma- star wakubwa wawili Angeline Jolie na Brad Pitt, wawili hawa walififanya harusi ndogo iliyoalika wana ndugu tu wa karibu na marafiki, harusi iliyofanyika katika mji wa Chateau Miraval, Hii inakuwa ni ndoa ya pili kwa Brad Pitt na ya tatu sasa kwa Angeline Jolie.

Posted via Blogaway

Jikumbishe amri 10 za soka enzi zetu za utoto. Lazima ucheke!!!

Pamoja na sheria 17 za soka za FIFA kuwepo, enzi za utoto kulikuweko na sheria za soka ambazo ndizo zilizokuwa zinatambuliwa:-

1.Mwenye mpira ndiye anayeamua nani atacheza

2.Mtoto bonge ndiye golikipa

3.Wachezaji mahiri ndio wanaochaguliwa kwanza

4.Kukiwa na penati ruksa kubadilisha kipa

5.Ukipiga mpira kwa nguvu au kwa mandochi mwenye mpira ana ruhusa ya kukuonya au kukukataza usicheze

6.Usipochagia hela ya kujaza upepo utapigwa marufuku kucheza

7.Hakuna marefa wala malinzmeni, na mpira unachezwa mpaka kuzunguka goli
8.Kumkaba mwenye mpira faulo

9.Ukitoboa mpira unalipa

10.Mwenye mpira akikasirika au akiumia au akiitwa na mama yake ndio mwisho wa mechi


Posted via Blogaway

PICHA: COMMENT CHOCHOTE HAPA ...WANAENDANA HAWAENDANI?.....

Hussein Machozi aelezea ukweli wa habari ya kufumaniwa na mke wa mwanasiasa Kenya

Star wa bongo Hussein Machozi hatimaye amezungumzia tukio lililotokea mwezi uliopita na kupelekea vyombo vingi vya habari nchini Kenya kuripoti kuwa amekamatwa akizini na mke wa mwanasiasa maarufu mjini Mombasa, Kenya. Haya ndio maelezo ya hit maker wa ‘Kwaajili Yako’ kuhusu kilichotokea, alipozungumza na Millard Ayo kupitia Amplifaya ya Clouds FM jana (Agosti 28). “Ukweli ni kwamba hiyo story imekuzwa yaani imekuwa kubwa sana tofauti na jinsi mambo yalivyokuwa. Kama masaa 24 nilipewa sasa mbona bado nipo Kenya…Ile ishu ilikuwa hivi, tulikuwa tumekwenda kuingia deal hotelini kama tunavyokutanaga, sasa Yule mtu aliyekuwa ananipa deal alikuwa yupo pale hotelini akaniita twende tukaongee kupanga mikakati na kila kitu, lakini baadae kumbe alikuwa na beef sijui na mume wake au sio bana, kwahiyo mume wake alikuja pale kuanza kumletea fujo lakini mimi sikuwa kwenye uhusiano wowote, watu wakaleta fujo pale na nini mimi mbona nikaondoka fresh tu lakini hamna lolote ni kwamba tulikuwa tumekaa nae tunaongea mchakato wa biashara…hotelini kama maeneo ya kupumzika hivi kama sehemu ya mikutano hivi”.

 Asante kwa kutembelea blog hii na kalibu tena ila usisahau kubofya hapa ili ujiunge nasi 


Posted via Blogaway

Baada ya Okwi kutangaza kujiunga na Simba,hiki ndicho walichokifanya Yanga.

Zikiwa siku chache zimepita toka klabu ya Simba kumtangaza Emmanuel Okwi kama mchezaji wao rasmi wa klabu hiyo,taarifa nyingine iliyotolewa leo na uongozi wa Yanga ni kumshitaki Okwi. Klabu ya Young Africans imemshitaki Emmanuel Okwi kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kuingia mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili na Yanga.

Posted via Blogaway

HIVI NI UMAARUFU, PESA AU MAPENZI YA KWELI YANAYOWAFANYA WADADA HAWA KUMPENDA DIAMOND??? TUJUZE

Ni kawaida ya dada zetu hapa Tz,siyo wote ila ni baadhi yao kujigonga kwa mtu yeyote pale apatapo umaarufu,haijalishi alikuwa handsome au mtu wa kawaida,ni pale tu anapoanza kupata jina ndio unaona idadi ya watu wanaongezeka si tu wadada yani hadi idadi ya marafiki huongezeka pale mtu apatapo umaarufu,ila kwa Diamond Platnumz wamembatiza hadi jina na kumuita sukari ya warembo,Jina hili limetokana na jinsi wadada zetu wanavyompenda msanii huyu tena ile zaidi ya kimuziki. Aliyempa jina la sukari ya warembo hakukosea kabisa cause hivi sasa Diamond Platnumz si yule wa zamani wa mbagala tena ambaye kila mtu alikuwa anamdharau,pale kabla hata hajatoka kulinganisha na hivi sasa. ni mfululizo wa wadada walioteyari kuuza roho zao kupata attention kutoka kwa mwanamuziki huyu,ila swali la kujiuliza ni mapenzi ya kweli au ni umaarufu tu alionao ndio kinachotengeneza sukari hiyo,unaweza kusema labda ni zile Benjamins(money) alizonazo ndio zinaongeza utamu wa sukari hiyo..well,nobody seem to know the answer…ila mbali ya hayo yote mwisho wa siku ni kukubali tu the guy anaweza. Kati ya mwanamuziki anayeongoza kuwa na ladies skendo basi huyu raisi wa wasafi hawezi kusahaulika hata kwabahati mbaya,cause for the past year tumeweza kusikia that amedate na wadada kama watatu hivi,mbali na rumors zile za hapa na pale ambazo hazina uthibitisho kwamba ni kweli au si za kweli,he has been on and off to these ladies. Ni Raisi wa wasafi,Diamond Platnumz aliyeweza kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na kipaji chake cha kutoa hit tracks nzuri zilizoteka nyoyo za mashabiki wa kila rika na kila nchi hapa africa na nje ya africa, kokote kule wasikiapo track kali za mwanamuziki huyu,ni umaarufu uliotokana na juhudi alizonazo pamoja na kipaji chake mwenyewe ndicho kilichopelekea kupata umaarufu huu ndani ya muda mfupi tu.

Credit vibe


Posted via Blogaway

PERUZI KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI HAPA