Lady Jaydee ameamua kujibu habari
iliyoandikwa kwenye gazeti la udaku la Risasi
kuhusu kuwa na uhusiano na aliyewahi kuwa
mtuma salamu maarufu kwenye redio, Meddy
Ahmed aka ‘Mtoto wa Vitoto’.
Kwenye habari hiyo, Risasi wanadai kuwa
Jaydee ambaye anadaiwa kuachana na mume
wake Gadner G Habash ameonekana mara
kadhaa na Mtoto wa Vitoto na kwamba
amewahi kuonekana akiwa na gari lake.
Kupitia Instagram, Jaydee ameandika:
Kuna habari za kuniudhi Ila hii imenichekesha.
Kwahiyo mtoto wa vitoto ndio bwana angu????
Basi sawa nashukuru naona mmenianzia tena
sasa picha za February Na nilizi post
mwenyewe humu insta leo ndio mmeziona?
Ukweli mnaujua mmeamua tu kuzingua ,,,
wangapi wameshapiga picha na hiyo Range?
Duuuh! !!!!! Shkamoooni Moyo wangu chuma.
Pigeni mawe mpk mchoke Kama ambavyo
mmekuwa mkifanya miaka yote na bado nipo
hapa hapa.” |
0 comments:
Post a Comment