| Usiku wa jana mshambuliaji wa kimataifa wa
Spain Fernando Torres alikamilisha usajili
wake wa mkopo wa miaka miwili kutoka
Chelsea kwenda AC Milan.
Huku yakiwa hajapita hata masaa 24 tangu
Torres aondoke, Jose Mourinho amekamilisha
usajili wa mbadala wa Torres, mshambuliaji
wa kimataifa wa Ufaransa Loic Remy.
Remy ambaye alifeli vipimo vya afya
alipokuwa akikaribia kujiunga na Liverpool
mwanzoni mwa dirisha la usajili, amejiunga na
Chelsea kwa ada ya uhamisho wa paundi
millioni 10 kutoka QPR.
Remy anachukua nafasi ya Torres na kuungana
na Didier Drogba katika kumsaidia Diego
Costa.
Wakati huo huo Alex Song amejiunga na West
Ham kwa mkopo kutoka FC Barcelona. |
0 comments:
Post a Comment