Saturday, August 30, 2014
 |
| Star wa bongo Hussein Machozi hatimaye
amezungumzia tukio lililotokea mwezi uliopita
na kupelekea vyombo vingi vya habari nchini
Kenya kuripoti kuwa amekamatwa akizini na
mke wa mwanasiasa maarufu mjini Mombasa,
Kenya.
Haya ndio maelezo ya hit maker wa ‘Kwaajili
Yako’ kuhusu kilichotokea, alipozungumza na
Millard Ayo kupitia Amplifaya ya Clouds FM
jana (Agosti 28).
“Ukweli ni kwamba hiyo story imekuzwa yaani
imekuwa kubwa sana tofauti na jinsi mambo
yalivyokuwa. Kama masaa 24 nilipewa sasa
mbona bado nipo Kenya…Ile ishu ilikuwa hivi,
tulikuwa tumekwenda kuingia deal hotelini
kama tunavyokutanaga, sasa Yule mtu
aliyekuwa ananipa deal alikuwa yupo pale
hotelini akaniita twende tukaongee kupanga
mikakati na kila kitu, lakini baadae kumbe
alikuwa na beef sijui na mume wake au sio
bana, kwahiyo mume wake alikuja pale kuanza
kumletea fujo lakini mimi sikuwa kwenye
uhusiano wowote, watu wakaleta fujo pale na
nini mimi mbona nikaondoka fresh tu lakini
hamna lolote ni kwamba tulikuwa tumekaa nae
tunaongea mchakato wa biashara…hotelini
kama maeneo ya kupumzika hivi kama sehemu
ya mikutano hivi”. |
Asante kwa kutembelea blog hii na kalibu tena ila usisahau kubofya hapa ili ujiunge nasi
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment