| Suala la Emmanuel Okwi
kutangaza kuwa Yanga
imevunja mkataba wake na
sasa ataitumikia Simba,
limezua sekeseke na sasa ni
mtafutano kila kona, kama
ni vita sasa hii ndiyo
inaanza kukolea.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf
Manji, amefunguka kuwa
wametoa siku saba kwa
Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kutoa majibu sahihi
juu ya Simba kumtangaza
Okwi kuwa mchezaji wao
wakati bado kuna kesi
inayoendelea baina ya Yanga
na Okwi.
Kuonyesha kuwa wapo
‘serious’ na hicho
wanachokifanya, Manji
amesema kuwa ikiwa TFF
haitatoa majibu ya
kueleweka kwao ndani ya
siku saba, basi moja kwa
moja watatua katika
Shirikisho la Soka la
Afrika (Caf), ikiwa pia
hapo hakutaeleweka ndani ya
siku saba, basi wataelekea
Shirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa) kwa ajili
ya suala hilo.
Manji alionekana kutokuwa
na utani kwenye kauli zake,
alionekana kukerwa na
kitendo cha Okwi kutua
Simba na kusema kuwa Yanga
imevunja mkataba wake,
ndiyo maana ameamua kwenda
kuichezea Simba.
Waipa siku saba TFF
“Tumepeleka barua TFF, leo
(Ijumaa) asubuhi kutoa
malalamiko kuhusiana na
Simba kumsainisha Okwi
wakijua wazi kuwa ana
mkataba na sisi wa miaka
miwili.
“Hii ni barua yetu ya tatu
baada ya mbili tulizopeleka
mwezi wa tano na wa saba
juu ya malalamiko kwa Okwi
kutoitumikia Yanga
kutofanyiwa kazi.
Kutinga Fifa
“Tumetoa siku saba kwa TFF
kulitolea ufafanuzi suala
hili na kutoa maamuzi juu
ya kilichofanyika na iwapo
maamuzi hayatatolewa ndani
ya muda huo, tunatarajia
kuwasilisha malalamiko yetu
Fifa na ikishindikana
tutaliwasilisha katika
Mahakama ya Michezo nchini
Uswisi (CAS).
Simba hawajui sheria za
soka
“Viongozi wa Simba
wameshindwa kufanya suala
la uungwana kwa kufuata
sheria za mpira kama
zinavyoeleweka, wangekuja
kuwauliza kwani hatukatai
kuuza wachezaji ila sheria
ifuatwe.
“Mfano mzuri kina Frank
Domayo na Didier Kavumbagu
wamesajiliwa,
hatujalalamika kwa kuwa
walifuata utaratibu
unaotakiwa.
“Upande wangu naona ni
jambo la kawaida
kushirikiana, hata mimi
nilimpongeza (Evans) Aveva
alipochaguliwa kuwa rais
kwani ndiyo mambo ya mpira
yalivyo.
Waongeza dau la fidia
“Dau la awali kabla ya
kusaini Simba tulitaka
alipe fidia ya dola 200,000
(Sh milioni 320) lakini
baada ya kuamka leo
tumeongeza dola 500,000 (Sh
milioni 800), kwa hiyo
jumla ni dola 700,000 (Sh
bilioni 1.12). Hii
tutawadai Simba na Okwi
mwenyewe.
Wataka Okwi afungiwe maisha
“Tumepeleka malalamiko TFF
ikiwezekana mchezaji huyo
afungiwe maisha, pamoja na
wakala wake kutoshiriki
masuala ya soka hapa
Tanzania kutokana na
ukiukwaji wa sheria
alioufanya ikiwa ni wazi
kuwa bado ana mkataba na
klabu yake ya awali.
Apendekeza Simba ishushwe
daraja
“Kutokana na kitendo
walichokifanya Simba
wasinione mbaya iwapo timu
itashushwa daraja kutokana
na kumsajili mchezaji
aliyekuwa na mkataba kwa
kutofuata sheria, iwapo
walikuwa wanahitaji
kumnunua wangekuja na
kuzungumza nasi.
“Kwani sisi huwa tunaachana
vizuri na wachezaji wetu,
mfano mzuri Fred Mbuna na
Shadrack Nsajigwa ambaye
kwa sasa amerudi kuja
kufundisha Yanga, hii ni
kutokana na kuachana
vizuri.
Atishia kuinunua Simba
“Mimi nina uwezo wa kununua
wachezaji wote wa Simba na
nikawalipa mshahara na
jambo hilo naliweza, ila
tunachoangalia ni kufuata
kanuni na sheria za soka.
“Kwani hata sisi tungeweza
kumchukua (Amissi) Tambwe
kutokana na kumuona ni
mchezaji mzuri na kumsajili
Yanga lakini hatuwezi
kufanya hivyo kwa kuwa
tunatambua sheria na
mchezaji huyo ana mkataba
ambao tunauheshimu.
“Hata hivyo Klabu ya Yanga
ina mfuko mrefu kuliko
Simba.
Jina lake limo katika
usajili TFF
“Tumewasilisha majina sita
ya wachezaji wa kimataifa
akiwemo Okwi kwa kuwa
hatukupata majibu yetu
mapema kutoka TFF.
“Iwapo wangetupatia taarifa
mapema tungeamua kumuacha
mchezaji mmoja, hata Jaja
na kumwambia akakae kwa
miezi sita kisha angerudi
tena kucheza.
“Siyo kwamba tunalalamika
kuwa tunamhitaji mchezaji
huyo kwani kuna wachezaji
wengi na tunaweza kwenda
kusajili sehemu mbalimbali
duniani ila tunataka sheria
ifuatwe.
Okwi ataka kukutana na
Manji
“Okwi alikuja ofisi kwangu
na kutaka kuonana na mimi
lakini nikawa bize
akaambiwa na katibu muhtasi
wangu kuwa atapangiwa siku,
kweli akapangiwa siku,
hakutokea, akapigiwa simu
hakupokea lakini alitumiwa
meseji hakuweza kujibu wala
kutokea tena.
Akana kuvunja mkataba
“Hatujawahi kuvunja
mikataba na wachezaji wa
Simba, kwani hata Juma
Kaseja tulisubiri mkataba
uishe ndiyo tukaingia naye
mkataba…
“…Ndiyo maana tulimsajili
pia Kelvin Yondani baada ya
mkataba wake kumalizika,
hatukuvunja sheria.
Waunda kamati ya sheria
“Kesho (leo) tunatarajia
kutangaza kamati yetu mpya
ya sheria ambapo ilikuwa ni
mpango wa muda mrefu, kwani
tumeona ni muhimu kuwa na
kamati hii na isifikiriwe
kuwa imetokana na suala la
Okwi,” alisema Manji. |
0 comments:
Post a Comment