Saturday, August 30, 2014
 |
| Zikiwa siku chache zimepita toka klabu ya
Simba kumtangaza Emmanuel Okwi kama
mchezaji wao rasmi wa klabu hiyo,taarifa
nyingine iliyotolewa leo na uongozi wa Yanga
ni kumshitaki Okwi.
Klabu ya Young Africans imemshitaki
Emmanuel Okwi kwenye Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa
shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) na
shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kuingia
mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado
ana mkataba wa miaka miwili na Yanga. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment