Saturday, August 23, 2014

ANGALIA TANZANIA ELEVEN WANAVYOPIGA BATA NDANI YA SAPPHIRE COURT KABLA YA KUIVAA MADRID LEO

NSAJIGWA, NYENGE NA MASATU.
KIKOSI CHA TANZANIA ELEVEN WAKIJIACHIA KWA MISOSI YA NGUVU KWA MGAHAWA WA HOTELI YA SAPPHIRE COURT YA JIJINI DAR ES SALAAM AMBAKO WAMEWEKA KAMBI KUJIWINDA DHIDI YA WAKONGWE WA REAL MADRID AMBAO WATAWAVAA LEO KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR KATIKA MECHI YA KIRAFIKI INAYOSUBIRIWA KWA HAMU KUBWA NA MASHABIKI
LUNYAMILA NA ATHUMANI CHINA.
IDDI MOSHI MNYAMWEZI NA MAXIME.
CHINA

Credit salley ally

Haya ndo matokeo ya mechi kati ya ATLETICO MADRID VS REALMADRID, super cup

Wakati wakongwe wao wakitarajiwa kucheza mechi ya kirafiki leo jijini Dar es Salaam, Real Madrid imeshindwa kuonyesha kuwa wanaweza baada ya kuchapwa bao 1-0 na wapinzani wao wakubwa Atletico Madrid. Kipigo hicho cha bao 1-0 katika mechi ya pili ya Super Cup, maana yake Atletico wameibuka mabingwa kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza ndani ya Camp Nou. Muuaji wa jana alikuwa na Mario Mandzukic ambaye amejiunga na Atletico akitokea Bayern Munich ambaye alifunga bao hilo katika dakika ya 2 tu. Pamoja na juhudi za Kocha Carlo Ancelotti kumuingiza Cristiano Ronaldo katika kipindi cha pili, bado Madrid haikuweza kupindua matokeo. Kiungo Luca Modric alilambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu. NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON

MSAFARA WA MWISHO WA REAL MADRID ULIVYOTUA DAR, LEO TAIFA PATAPENDEZA

Magwiji wa Real wakisubiri usafiri kuelekea Bahari Beach
Watu walijitokeza kuwapokea
Wanaelekea kwenye basi la Azam FC kwa safari ya hotelini
Msafara wa mwisho wa Real Madrid baada ya kuwasili Dar es Salaam jana jioni tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya magwiji wa Tanzania Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Friday, August 22, 2014

KARIBU TANGA: MAHABA NAMNA HII KWANINI MTU UCHEPUKE?!!!!....HAPO NDIO MAANDALIZI YA FOOD...

BALOTELLI ATUA LIVERPOOL KUKAMILISHA USAJILI WAKE

MSHAMBULIAJI Mario Balotelli alitarajiwa kuwasili England leo mchana kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kujiunga na Liverpool baada ya klabu hiyo kufikia makubaliano na wawakilishi wake. Mpachika mabao huyo wa zamani wa Manchester City yuko karibu kusaini kikosi cha Brendan Rodgers na amekwenda huko kukamilisha dili hilo mara moja. Baada ya kuwasili, Balotelli alitarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo katika hospitali ya klabu hiyo, Spire Liverpool kabla ya kwenda kufanyiwa vipimo zaidi vya afya katika viwanja vya Melwood vinavyotumika kwa mazoezi na klabu hiyo. Pamoja na hayo, mshambuliaji huyo wa Italia hataweza kuichezea Liverpool dhidi ya klabu yake ya zamani, Manchester City Jumatatu usiku, katokana na muda wa usajili kwa leo kupita.NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON

FAHAMU KIWANGO KIPYA ANACHOLIPWA DIAMOND KWA SHOW MOJA YA MZIKI HAPA TANZANIA

Tangu mwaka juzi tulifahamu kuwa Diamond Platinumz ndiye msanii wa Tanzania anaelipwa kiasi kikubwa cha pesa, na mwaka jana ikaelezwa kuwa bila milioni 10 au 8 za Kitanzania humpati kwenye show yako. Lakini kiwango kipya kilichotajwa jana kitawapa kizunguzungu zaidi hasa mapromota wenye mitaji midogo wenye ndoto za kufanya kazi na mwimbaji huyo. Kwa mujibu wa, Babu Tale ambaye ni meneja wake, hivi sasa kiwango cha chini anachochaji kwa show moja hapa nchini ni $15,000 (sawa na shilingi Milioni 25 za Tanzania). “Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola e15,000.” Babu Tale aliiambia Bongo5. Kwa mujibu wa Babu Tale, wanachaji kiasi cha hadi dola 25,000 kwa show moja za nje ya nchi (ikiwemo Marekani). “Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya.” Alisema wakati akikanusha tuhuma kuwa Diamond anauza dawa za kulevya. Kwa mahesabu ya haraka haraka, shows 15 mara dola 25,000 ni sawa na $375,000 (Sawa na shilingi za Tanzania 625,687,500). Yesss! Ni zaidi ya Milioni mia sita ishirini na tano za kitanzania. Kama ni kweli, basi Diamond anastahili kweli kuitwa Dangote wa Bongo Flava. Bado michongo inaendelea kumiminika ambapo hivi karibuni meneja wa Trey Songz alimtumia ujumbe kuwa atakapokuwa na nafasi amshitue waongee.

Kutana na vichekesho vya Peter Msechu na Baba Levo baada ya kukosa show.

Peter Msechu na Baba Levo ni wasanii kutoka mkoa wa Kigoma na wote wawili wana sifa ya kuwa wachekeshaji sana. Wasanii wengi wanajua kwamba ukipanda tour bus na wawili hawa basi ni kama unaangalia show ya comedy njia nzima ya safari. Peter Msechu amekuwa ana post vichekesho mbalimbali, kutana na hivi viwili kuhusiana na kazi yao baada ya kukosa show.

FIGO: NJOONI MUONE VITU VYANGU KESHO TAIFA, KAREMBEU ASEMA ATAMPA MAPANDE YA KUMWAGA AWABURUZE WATANZANIA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM MWANASOKA bora wa zamani wa dunia, Luis Figo ameahidi burudani nzuri ya soka kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati magwiji wa Real Madrid ya Hispania watakapomenyana na magwiji wa Tanzania katika mchezo wa kirafiki. Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu katika hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam, mshindi huyo wa Ballon d’Or mwaka 2000, aliyestaafu Mei 31 mwaka 2009, amesema kwamba Watanzania watafurahia kazi yake uwanjani kesho. Figo aliyepiga tuzo mbili mfululizo mwaka 2000, Mwanasoka Bora Ulaya na Dunia, amewaomba wapenzi wa soka Tanzania kujitokeza kwa wingi kesho kushuhudia burudani. “Ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, nimekwishatembea nchi kadhaa Afrika, nimefurahi kuja hapa, naipenda Afrika. Natarajia mchezo mzuri kesho, hata kwa wapinzani wetu pia, kitu muhimu ni kwamba FIFA imefurahia tukio hili,”alisema Figo. Kwa upande wake, mwanasoka bora wa Oceania mara mbili 1995 na 1998, Christian Karembeu aliyeshinda Kombe la Dunia na Ufaransa mwaka 1998, amesema kwamba atampa pasi nyingi kesho Figo afanye vitu vyake. Beki wa zamani wa kimataifa wa Hispania, Fernando Sanz Duran ni miongoni mwa wanasoka watatu waliowika Real Madrid muongo uliopita waliofika jana usiku, ambaye pia alikuwepo kwenye mkutano wa leo. “Nimefurahi kuja Tanzania, ni mara yangu ya kwanza, Watanzania watarajie burudani nzuri kutoka kwetu na wapinzani wetu,”alisema Sanz huku akimgusa begani, kocha Msaidizi wa Magwiji wa Tanzania, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’. Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa England, Michael Owen aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi Kombe la Dunia mwaka 1998 Ufaransa, anatarajiwa kuwasili katika kundi la mwisho la Magalactico hao jioni ya leo. Mkurugenzi wa makampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), Farough Baghozah ambao ndiyo wanawaleta magwiji hao nchini, amesema maandalizi yote yamekamilka na Watanzania wajitokeze kwa wingi Taifa kesho. Magalactito wa Real wamefikia katika hoteli ya Ladger Plaza, Bahari Beach wakati timu ya Tanzania imeweka kambi Kariakoo, Dar es Salaam kikiendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa. Kikosi hicho kinaundwa na makipa maarufu waliowahi kuwika nchini, Mwameja Mohamed na Manyika Peter, mabeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu, Abubakar Kombo, George Masatu, Habib Kondo, Viungo Athumani China, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo. Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka, Madaraka Suleiman na Akida Makunda. Benchi ka Ufundi, ni Kocha Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ na Wasaidizi Freddy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, Daktari Mwanandi Mkwankemwa na viongozi Mtemi Ramadhani, Hassan Mnyenye, Omar Gumbo na Hamisi Kisiwa. Katika ziara hiyo, pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania Agosti 23, pia watafanya utalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.

Aunt Ezekiel ajibu kauli ya Diamond kuhusu marafiki wa Wema ‘wapenda anasa’

Muigizaji wa filamu nchini, Aunt Ezekiel ambaye ni rafiki wa karibu wa mpenzi wa Diamond Platnumz, Wema Sepetu amezungumzia kauli ya Diamond aliyotoa hivi karibuni kuwa mpenzi wake ana marafiki wapenda starehe na anasa. Aunt ameiambia Bongo5 kuwa Wema ni mtu mzima anajua baya na jema. “Diamond alivyoongea pale hakunitaja jina, kwahiyo nikisema kwamba aliongea kwa sababu yangu nitakuwa muongo. Yeye aliongea kwa niaba ya watu ambao wako na Wema, hata kama angekuwa amenitaja jina sidhani kama angeongea kwamba yule mtu anafundishwa,” amesema Aunt. “Wema ni mtu mzima anaishi mwenyewe na ana maisha yake sidhani kama ni mtu wa kufundishwa. Wema ni mtu ambaye ana maamuzi yake, watu hawajui kuna wakati wa kazi na kuna wakati wa kuspend maisha. Kwahiyo mimi na muda wangu wa kazi na nina muda wangu waku spend.” “Sihitaji kuangalia kuna mtu anafuatilia maisha yangu kwamba eti nakuwaga na Wema. Hawanisaidii chochote. Nachotakiwa kuangalia nafanya kazi zangu na maisha yangu yanaenda mbele na sitaangalia watu wanasema nini. Mimi nina kazi zangu. Sijui kama Wema kama anahitajika kubadilika kwa sababu Diamond ndiyo anajua mapungufu ya Wema na Wema anajua ya Diamond.” Kwa upande mwingine muigizaji huyo amesema anakuja na filamu yake mpya iitwayo ‘Mwajuma Nipe’. CREDIT BONGO5

TB JOSHUA ATUMA MSAADA WA CHUPA 4000 ZA MAJI YA UPAKO KUPONYA EBOLA

Nabii maarufu ndani na nje ya bara la Afrika TB Joshua wa kanisa la All nations (Scoan) la nchini Nigeria ametuma chupa 4000 za maji ya upako pamoja na dola za kimarekani 50,000 nchini Sierra Leon ili kusaidia kutibu ugonjwa wa ebola ambao umeikamata nchi hiyo. Nabii Joshua amesema kupitia tovuti ya kanisa lake kwamba maji hayo yamesafirishwa kwa ndege maalumu ya kukodi ambayo gharama yake pia ni dola 50,000 na kufanya gharama kamili dola 100,000 (laki moja) kwa msaada alioutoa akishirikiana na wadau wa Emanuel TV ya kanisa lake. Katika taarifa yake kupitia tovuti hiyo nabii TB Joshua amesema Mungu mwenye nguvu atajidhihirisha uweza wake kupitia maji hayo ya upako ambayo yametolewa kwa watu waliokumbwa na ebola. "Sio maji ndiyo ya ponyayo wagonjwa ila ni Yesu mwenyewe, lazima mtu anayemuombea mwingine na yule anayeombewa wawe na imani. lazima imani iwe hai ili kupata uponyaji kwasababu ndiyo husababisha uponyaji na sio maji ya upako" amekaririwa nabii Joshua. Watu waliotumia maji hayo ya upako wamekiri kuwa na imani nayo kutokana na wengi kufunguliwa na miujiza mingi kutendeka kutoka hali ya kutokuwa na uwezo wa kuzaa na hatimaye kupata mtoto lakini pia maji hayo yamekuwa kinga ya risasi kupenya kwenye gari kama mtu mmoja kutoka nchini Ghana alivyopona mikononi mwa majambazi waliokuwa wakishambulia kwa risasi gari lake yeye akiwemo ndani bila mafanikio. Na mdadisiblog/festosaimon

DJ FETTY WA CLOUDS NOMA SANA ATWAGANA NGUMI LIVE LIVE CLUB

Stori: Musa Mateja MTANGAZAJI wa Clouds Redio na TV, Fatuma Hassan ‘DJ Fetty’, juzikati alijikuta akitwangana makonde na mrembo mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja baada ya kupishana kauli kwenye ukumbi mmoja wa starehe pande za Kahama, Shinyanga. Katika tukio hilo, Fetty aliyekuwa kwenye ‘tour’ ya Serengeti Fiesta alizama ukumbini hapo usiku na baada ya muda mfupi paparazi wetu alishangaa kumuona akizichapa na mrembo huyo ikidaiwa walizinguana, hata hivyo waliamuliwa kabla mambo hayajawa mabayaw. Ziara ya Tamasha la Fiesta kesho itahamia Tanga ambapo wasanii kibao wataangusha burudani ndani ya Uwanja wa Mkwakwani

SASA CAF YAICHARUKIA YANGA MCHANA KWEUPE

Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limewataka Yanga ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kuwa na kiwanja chao cha mazoezi. Yanga ambayo ipo kisiwani Pemba kwa ajili ya kambi yake ya kujiandaa na mikikimikiki ya msimu mpya, inatarajiwa kuwakilisha taifa katika Kombe la Shirikisho Afrika, lakini imekuwa haina uwanja wa kudumu wa kufanyia mazoezi. Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura amesema agizo hilo la Caf limezitaka timu zote za hapa nchini ambazo zitashiriki mashindano ya kimataifa kuwa na viwanja rasmi vya mazoezi ambavyo vitaweza kutumika muda wowote. “Tumepewa agizo na Caf juu ya kuziambia timu za Azam na Yanga ambazo zitaiwakilisha nchi yetu kwenye mashindano ya kimataifa kuwa na viwanja vyake rasmi vya mazoezi na kama timu haitakamilisha agizo hilo, inaweza ikaondolewa kushiriki mashindano hayo,” alisema Wambura. Ulipotafutwa uongozi wa Yanga kulizungumzia hilo, haukupatikana.

UNASEMA PHIRI MPOLE, SOMA HAPA UONE ANAPOKUWA KAZINI

Kocha wa Simba SC, Mzambia, Patrick Phiri, amewapa masharti mapya wachezaji wake ikiwemo kuwapiga marufuku kukaa chini muda wa mazoezi, hata kama wakiambiwa wapumzike. Hilo limejiri hivi karibuni wakati Simba ilipokuwa ikiendelea na mazoezi kisiwani Zanzibar kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kiislamu, Chukwani ambapo Phiri alikataza wachezaji waliokuwa pembeni wakipumzika wakisubiri ratiba nyingine, kukaa chini wakiwa kwenye mchakato wa mazoezi. Katika mazoezi hayo, wachezaji wa Simba waligawiwa katika vikosi vitatu ambapo viwili vilikuwa uwanjani, kile kingine ndipo wachezaji wake wakaamua kukaa chini kuwasubiri wenzao. Bila kuchelewa, Phiri alipoliona tukio hilo, alilazimika kuwafuata wachezaji hao na kuwaambia kuwa hawatakiwi kukaa chini wakati wakiwa kwenye programu ya mazoezi, badala yake wanatakiwa kusimama hata kama wakiwa wanapumzika au wanakunywa maji. “Hamtakiwi kukaa chini kama hivyo, kama ukiwa kwenye programu ya mazoezi ya kitimu kama hivi unatakiwa kupumzika kwa kusimama na hata ukinywa maji hupaswi pia kukaa chini, hili lisijirudie tena,” alisikika Phiri akiwaonya wachezaji wake hao. Na mdadisiblog/festosaumon

Shakira atuhumiwa ku- copy na ku-paste wimbo

Sehemu kidogo ya wimbo wa Loca (Spanish version) kutoka kwa mwimbaji Shakira ilikuwa ni kazi ya mtungaji mwingine wa nyimbo anaitwa Ramon Arias Vazquez.

Jaji Alvin Hellerstein alisema toleo la wimbo “Loca” la lugha ya kihispania 2010 lilikiuka haki za umiliki za wimbo wa mwimbaji Ramon Arias Vazquez.

Wimbo huo ulikuwemo kwenye albam yake ya mwaka 2010 ‘Sale el Sol’ na uamuzi unatarajiwa kuelekeza fidia atakayolipwa kwa mlalamikaji

IMEJULIKANA KUMBE KAVUMBAGU ANATUMIA VIDONGE

Straika wa Azam FC, Mrundi, Didier Kavumbagu ameweka wazi kuwa, anatumia vidonge maalum kuongeza virutubisho vya mwili ambavyo vinamsaidia kuwa mwepesi na kumudu programu za kocha wake. Kavumbagu ambaye alikipiga Yanga misimu miwili kwa mafanikio aliyasema hayo hivi karibuni ambapo alikiri kuwa vidonge hivyo vinaongeza virutubisho muhimu mwilini, pia kuulainisha mwili kuwa tayari kwa ajili ya mazoezi magumu ya kimichezo na si vinginevyo. “Nimefanya vizuri katika mazoezi kwa kuwa ninapata muda mwingi wa kupumzika na kula chakula katika muda mwafaka, pia kuna rafiki yangu yupo Ulaya amenitumia vidonge f’lani vya vitamin ambavyo nikimeza vinaufanya mwili uwe huru na kuwa tayari kwa ajili ya mazoezi. “Ni vidonge vya kawaida ambavyo mwanamichezo yeyote anaweza kutumia bila ya kupata madhara, hata Didier Drogba wa Chelsea anavitumia sana,” alisema Kavumbagu. Alipotafutwa Daktari wa Azam, Mwanandi Mwankenwa juu ya ufafanuzi wa vidonge hivyo, alisema: “Navifahamu vidonge hivyo, vinatumiwa na wachezaji wengi wa Azam, siyo yeye tu, hata (John) Bocco na wengine pia wanatumia, havina madhara kiafya.” SOURCE: CHAMPIONI

KOCHA JULIO ATOA KALI YA MWAKA BAADA YA KUMNASA KIBAO MWANDISHI WA HABARI

Kocha msaidizi wa timu ya wachezaji wa zamani wa Tanzania Eleven, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, juzi alitoa kituko kwa kumchapa kofi mwandishi ambaye (siyo wa Championi) alikuwa akimrekodi bila idhini yake baada ya kumaliza mazoezi yanayofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar. Julio alifanya kitendo hicho baada ya kugundua anarekodiwa pasipo mwenyewe kujua, jambo ambalo lilimkera, hivyo kuchukua uamuzi huo kama alivyofanya staa wa Argentina, Diego Maradona hivi karibuni. Julio alizungukwa na kundi kubwa la mashabiki ambapo alikuwa akipiga nao soga mbalimbali. Wakati mazungumzo yamekolea, kocha huyo alimpokonya simu kijana aliyekuwa karibu yake na kuitupa mbali na kisha kumpiga kibao na kumsindikizia na maneno yake yalee ya mbwembwe. “Haiwezekani we ufike unirekodi tu mimi wakati nipo kwenye mazungumzo binafsi,” alisema Julio na kuungwa mkono na wale aliokuwa akizungumza nao. SOURCE: CHAMPIONI

HII TABIA SASA NI BALAA...WADADA WANAZIDI KUJINANILIUUU..WAKATI WANAUME KIBAO HAWANA WAPENZI!!!!

Swali tuwafanyeje!!!

WANAWAKE WENGI NAMNA HII.....KAMA WEWE NDIO HAKIMU HUYU JAMAA UNGEMPA ADHABU GANI?

Jamaa aliebambwa anamla uroda
Mbuzi!!!!

BAADA YA LIVERPOOL KUMSAJILI BALOTEL JANA JIONI HUU NDO USAJILI MWINGINE MKUBWA UNAOFUATA

Kama ulikuwa unadhani Liverpool wamemaliza kazi baada ya kuwa hatua chache za kumnasa mtukutu Mario Barwuah Barotelli nakupa pole tena sana. Mchapo uko hivi Liverpool iko tayari kumpa mshambuliaji Mcameroun Samweli Eto'o mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengere cha kuongeza mmoja zaidi. Tayari kifuta jasho cha £75,000 kwa wiki kiko mezani Anfield,bonuses + michuano ya ligi ya mabingwa atake nini zaidi huyu swahiba wa Mourinho na Guardiola? Mara kadhaa Eto'o amenukuliwa akisema bado anataka kubaki England bado ana muda zaidi wa kucheza ligi kubwa na yenye ushindani... Marekani bado mapema sana kwake....... Bado ana deni na nafsi yake anataka amfunge Pellegrini ampe pole,amfunge Mourinho amcheke.