Muigizaji wa filamu nchini, Aunt
Ezekiel ambaye ni rafiki wa karibu
wa mpenzi wa Diamond Platnumz,
Wema Sepetu amezungumzia kauli
ya Diamond aliyotoa hivi karibuni
kuwa mpenzi wake ana marafiki
wapenda starehe na anasa.
Aunt ameiambia Bongo5 kuwa
Wema ni mtu mzima anajua baya
na jema.
“Diamond alivyoongea pale
hakunitaja jina, kwahiyo nikisema
kwamba aliongea kwa sababu
yangu nitakuwa muongo. Yeye
aliongea kwa niaba ya watu ambao
wako na Wema, hata kama
angekuwa amenitaja jina sidhani
kama angeongea kwamba yule mtu
anafundishwa,” amesema Aunt.
“Wema ni mtu mzima anaishi
mwenyewe na ana maisha yake
sidhani kama ni mtu wa
kufundishwa. Wema ni mtu
ambaye ana maamuzi yake, watu
hawajui kuna wakati wa kazi na
kuna wakati wa kuspend maisha.
Kwahiyo mimi na muda wangu wa
kazi na nina muda wangu waku
spend.”
“Sihitaji kuangalia kuna mtu
anafuatilia maisha yangu kwamba
eti nakuwaga na Wema.
Hawanisaidii chochote.
Nachotakiwa kuangalia nafanya
kazi zangu na maisha yangu
yanaenda mbele na sitaangalia
watu wanasema nini. Mimi nina
kazi zangu. Sijui kama Wema kama
anahitajika kubadilika kwa sababu
Diamond ndiyo anajua mapungufu
ya Wema na Wema anajua ya
Diamond.”
Kwa upande mwingine muigizaji
huyo amesema anakuja na filamu
yake mpya iitwayo ‘Mwajuma
Nipe’. CREDIT BONGO5 |
0 comments:
Post a Comment