Shirikisho la Soka
Afrika (Caf)
limewataka Yanga
ambao ni wawakilishi
wa Tanzania kwenye
michuano ya Kombe la
Shirikisho kuwa na
kiwanja chao cha
mazoezi.
Yanga ambayo ipo
kisiwani Pemba kwa
ajili ya kambi yake
ya kujiandaa na
mikikimikiki ya msimu
mpya, inatarajiwa
kuwakilisha taifa
katika Kombe la
Shirikisho Afrika,
lakini imekuwa haina
uwanja wa kudumu wa
kufanyia mazoezi.
Ofisa Habari wa
Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF),
Boniface Wambura
amesema agizo hilo la
Caf limezitaka timu
zote za hapa nchini
ambazo zitashiriki
mashindano ya
kimataifa kuwa na
viwanja rasmi vya
mazoezi ambavyo
vitaweza kutumika
muda wowote.
“Tumepewa agizo na
Caf juu ya kuziambia
timu za Azam na Yanga
ambazo zitaiwakilisha
nchi yetu kwenye
mashindano ya
kimataifa kuwa na
viwanja vyake rasmi
vya mazoezi na kama
timu haitakamilisha
agizo hilo, inaweza
ikaondolewa kushiriki
mashindano hayo,”
alisema Wambura.
Ulipotafutwa uongozi
wa Yanga
kulizungumzia hilo,
haukupatikana. |
0 comments:
Post a Comment