Kocha msaidizi wa
timu ya wachezaji wa
zamani wa Tanzania
Eleven, Jamhuri
Kihwelo ‘Julio’,
juzi alitoa kituko
kwa kumchapa kofi
mwandishi ambaye
(siyo wa Championi)
alikuwa akimrekodi
bila idhini yake
baada ya kumaliza
mazoezi yanayofanyika
kwenye Uwanja wa
Karume jijini Dar.
Julio alifanya
kitendo hicho baada
ya kugundua
anarekodiwa pasipo
mwenyewe kujua, jambo
ambalo lilimkera,
hivyo kuchukua uamuzi
huo kama alivyofanya
staa wa Argentina,
Diego Maradona hivi
karibuni.
Julio alizungukwa na
kundi kubwa la
mashabiki ambapo
alikuwa akipiga nao
soga mbalimbali.
Wakati mazungumzo
yamekolea, kocha huyo
alimpokonya simu
kijana aliyekuwa
karibu yake na
kuitupa mbali na
kisha kumpiga kibao
na kumsindikizia na
maneno yake yalee ya
mbwembwe.
“Haiwezekani we ufike
unirekodi tu mimi
wakati nipo kwenye
mazungumzo binafsi,”
alisema Julio na
kuungwa
mkono na wale
aliokuwa akizungumza
nao.
SOURCE: CHAMPIONI |
0 comments:
Post a Comment