Straika wa Azam FC,
Mrundi, Didier
Kavumbagu ameweka
wazi kuwa, anatumia
vidonge maalum
kuongeza virutubisho
vya mwili ambavyo
vinamsaidia kuwa
mwepesi na kumudu
programu za kocha
wake.
Kavumbagu ambaye
alikipiga Yanga
misimu miwili kwa
mafanikio aliyasema
hayo hivi karibuni
ambapo alikiri kuwa
vidonge hivyo
vinaongeza
virutubisho muhimu
mwilini, pia
kuulainisha mwili
kuwa tayari kwa ajili
ya mazoezi magumu ya
kimichezo na si
vinginevyo.
“Nimefanya vizuri
katika mazoezi kwa
kuwa ninapata muda
mwingi wa kupumzika
na kula chakula
katika muda mwafaka,
pia kuna rafiki yangu
yupo Ulaya amenitumia
vidonge f’lani vya
vitamin ambavyo
nikimeza vinaufanya
mwili uwe huru na
kuwa tayari kwa ajili
ya mazoezi.
“Ni vidonge vya
kawaida ambavyo
mwanamichezo yeyote
anaweza kutumia bila
ya kupata madhara,
hata Didier Drogba wa
Chelsea anavitumia
sana,” alisema
Kavumbagu.
Alipotafutwa Daktari
wa Azam, Mwanandi
Mwankenwa juu ya
ufafanuzi wa vidonge
hivyo, alisema:
“Navifahamu vidonge
hivyo, vinatumiwa na
wachezaji wengi wa
Azam, siyo yeye tu,
hata (John) Bocco na
wengine pia
wanatumia, havina
madhara kiafya.”
SOURCE: CHAMPIONI |
0 comments:
Post a Comment