Saturday, August 23, 2014
 |
Wakati wakongwe wao
wakitarajiwa kucheza
mechi ya kirafiki leo
jijini Dar es Salaam,
Real Madrid
imeshindwa kuonyesha
kuwa wanaweza baada
ya kuchapwa bao 1-0
na wapinzani wao
wakubwa Atletico
Madrid.
Kipigo hicho cha bao
1-0 katika mechi ya
pili ya Super Cup,
maana yake Atletico
wameibuka mabingwa
kwa jumla ya mabao
2-1 baada ya sare ya
1-1 katika mechi ya
kwanza ndani ya Camp
Nou.
Muuaji wa jana
alikuwa na Mario
Mandzukic ambaye
amejiunga na Atletico
akitokea Bayern
Munich ambaye
alifunga bao hilo
katika dakika ya 2
tu.
Pamoja na juhudi za
Kocha Carlo Ancelotti
kumuingiza Cristiano
Ronaldo katika
kipindi cha pili,
bado Madrid haikuweza
kupindua matokeo.
Kiungo Luca Modric
alilambwa kadi mbili
za njano na kuwa
nyekundu. NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON |
0 comments:
Post a Comment