Stori: Musa Mateja
MTANGAZAJI wa Clouds Redio
na TV, Fatuma Hassan ‘DJ
Fetty’, juzikati alijikuta
akitwangana makonde na
mrembo mmoja ambaye jina
lake halikuweza kufahamika
mara moja baada ya
kupishana kauli kwenye
ukumbi mmoja wa starehe
pande za Kahama, Shinyanga.
Katika tukio hilo, Fetty
aliyekuwa kwenye ‘tour’ ya
Serengeti Fiesta alizama
ukumbini hapo usiku na
baada ya muda mfupi
paparazi wetu alishangaa
kumuona akizichapa na
mrembo huyo ikidaiwa
walizinguana, hata hivyo
waliamuliwa kabla mambo
hayajawa mabayaw.
Ziara ya Tamasha la Fiesta
kesho itahamia Tanga ambapo
wasanii kibao wataangusha
burudani ndani ya Uwanja wa
Mkwakwani |
0 comments:
Post a Comment