Kama ulikuwa unadhani Liverpool wamemaliza kazi baada ya kuwa hatua chache za kumnasa mtukutu Mario Barwuah Barotelli nakupa pole tena sana.
Mchapo uko hivi Liverpool iko tayari kumpa mshambuliaji Mcameroun Samweli Eto'o mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengere cha kuongeza mmoja zaidi.
Tayari kifuta jasho cha £75,000 kwa wiki kiko mezani Anfield,bonuses + michuano ya ligi ya mabingwa atake nini zaidi huyu swahiba wa Mourinho na Guardiola?
Mara kadhaa Eto'o amenukuliwa akisema bado anataka kubaki England bado ana muda zaidi wa kucheza ligi kubwa na yenye ushindani... Marekani bado mapema sana kwake.......
Bado ana deni na nafsi yake anataka amfunge Pellegrini ampe pole,amfunge Mourinho amcheke. |
0 comments:
Post a Comment