Tangu mwaka juzi tulifahamu
kuwa Diamond Platinumz
ndiye msanii wa Tanzania
anaelipwa kiasi kikubwa cha
pesa, na mwaka jana
ikaelezwa kuwa bila milioni 10
au 8 za Kitanzania humpati
kwenye show yako.
Lakini kiwango kipya
kilichotajwa jana kitawapa
kizunguzungu zaidi hasa
mapromota wenye mitaji
midogo wenye ndoto za
kufanya kazi na mwimbaji
huyo.
Kwa mujibu wa, Babu Tale
ambaye ni meneja wake, hivi
sasa kiwango cha chini
anachochaji kwa show moja
hapa nchini ni $15,000 (sawa
na shilingi Milioni 25 za
Tanzania).
“Tuna show Marekani show
kumi na tano (15), show kumi
na tano dola elfu ngapi? Na
kwa hapa Tanzania hatufanyi
show chini ya dola e15,000.”
Babu Tale aliiambia Bongo5.
Kwa mujibu wa Babu Tale,
wanachaji kiasi cha hadi dola
25,000 kwa show moja za nje
ya nchi (ikiwemo Marekani).
“Tunalipwa milioni 20 show
moja, tunalipwa dola elfu
25,000 show moja, hii ni zaidi
ya madawa ya kulevya.”
Alisema wakati akikanusha
tuhuma kuwa Diamond
anauza dawa za kulevya.
Kwa mahesabu ya haraka
haraka, shows 15 mara dola
25,000 ni sawa na $375,000
(Sawa na shilingi za Tanzania
625,687,500).
Yesss! Ni zaidi ya Milioni mia
sita ishirini na tano za
kitanzania.
Kama ni kweli, basi Diamond
anastahili kweli kuitwa
Dangote wa Bongo Flava.
Bado michongo inaendelea
kumiminika ambapo hivi
karibuni meneja wa Trey
Songz alimtumia ujumbe kuwa
atakapokuwa na nafasi
amshitue waongee. |
0 comments:
Post a Comment