Friday, August 22, 2014

UNASEMA PHIRI MPOLE, SOMA HAPA UONE ANAPOKUWA KAZINI

Kocha wa Simba SC, Mzambia, Patrick Phiri, amewapa masharti mapya wachezaji wake ikiwemo kuwapiga marufuku kukaa chini muda wa mazoezi, hata kama wakiambiwa wapumzike. Hilo limejiri hivi karibuni wakati Simba ilipokuwa ikiendelea na mazoezi kisiwani Zanzibar kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kiislamu, Chukwani ambapo Phiri alikataza wachezaji waliokuwa pembeni wakipumzika wakisubiri ratiba nyingine, kukaa chini wakiwa kwenye mchakato wa mazoezi. Katika mazoezi hayo, wachezaji wa Simba waligawiwa katika vikosi vitatu ambapo viwili vilikuwa uwanjani, kile kingine ndipo wachezaji wake wakaamua kukaa chini kuwasubiri wenzao. Bila kuchelewa, Phiri alipoliona tukio hilo, alilazimika kuwafuata wachezaji hao na kuwaambia kuwa hawatakiwi kukaa chini wakati wakiwa kwenye programu ya mazoezi, badala yake wanatakiwa kusimama hata kama wakiwa wanapumzika au wanakunywa maji. “Hamtakiwi kukaa chini kama hivyo, kama ukiwa kwenye programu ya mazoezi ya kitimu kama hivi unatakiwa kupumzika kwa kusimama na hata ukinywa maji hupaswi pia kukaa chini, hili lisijirudie tena,” alisikika Phiri akiwaonya wachezaji wake hao. Na mdadisiblog/festosaumon

0 comments:

Post a Comment