MSHAMBULIAJI Mario Balotelli
alitarajiwa kuwasili England leo
mchana kwa ajili ya kufikia
makubaliano ya kujiunga na
Liverpool baada ya klabu hiyo
kufikia makubaliano na
wawakilishi wake.
Mpachika mabao huyo wa zamani
wa Manchester City yuko karibu
kusaini kikosi cha Brendan
Rodgers na amekwenda huko
kukamilisha dili hilo mara moja.
Baada ya kuwasili, Balotelli
alitarajiwa kwenda
kufanyiwa vipimo katika hospitali
ya klabu hiyo, Spire Liverpool
kabla ya kwenda kufanyiwa
vipimo zaidi vya afya katika
viwanja vya Melwood
vinavyotumika kwa mazoezi na
klabu hiyo.
Pamoja na hayo, mshambuliaji
huyo wa Italia hataweza
kuichezea Liverpool dhidi ya
klabu yake ya zamani,
Manchester City Jumatatu
usiku, katokana na muda wa
usajili kwa leo kupita.NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON |
0 comments:
Post a Comment