Tuesday, October 21, 2014

HUYU NDO MCHEZAJI ALIYEFARIKI AKIJARIBU KUSHANGILIA BAO KAMA MIROSLAV KLOSE

MWANASOKA amefariki dunia baada ya kuanguka vibaya aliporuka samasoti kushangilia bao katika mchezo wa Ligi Kuu ya jimbo la Mizoram nchini India. Peter Biaksangzuala amefariki akiwa hospitali Jumapili baada ya kuangukia kichwa chake aliporuka samasoti kushangilia bao aliloifungia Bethlehem Vengthlang FC - klabu yenye maskani yake Kaskazini Mashariki kwa jimbo la Mizoram. Mchezaji huyo aliyekuwa ana umri wa miaka 23 alifunga bao hilo dakika ya 62 kuisawazishia timu yake dhidi ya Chanmari West FC Jumanne katika mchezo wa Ligi na akataka kushangilia kwa staili ya mfungaji bora wa kihistoria wa Kombe la Dunia, Miroslav Klose.
Biaksangzuala alikosea katika kuruka kwake na akapigiza kichwa chini, kabla ya kupatiwa huduma ya kwanza uwanjani na kisha kutolewa nje kwa machela. Biaksangzuala alikimbizwa katika hospitali ya Aizawl Civil ambako vipimo vya CT vilionyesha amepata madhara makubwa kwa undani na mara moja akahamishiwa chumba cha wagonjwa walio chini ya uangalizi maalum. Chanzo kimesema: "Alijaribu kushangilia kama Mjerumani Klose, lakini akakosea kwa bahati mbaya. Alikaa hospitali kwa siku tano, lakini madaktari hawakufanikiwa kuokoa uhai wake,". Taarifa nchini India zinasema kwamba Biaksangzuala alichangia macho yake wakati akiwa amelazwa hospitali. Kwa ajili ya kumbukumbu ya kiungo huyo, Bethlehem Vengthlang FC imeamua kuipumzisha jezi namba 21 na Chama cha Soka Mizoram kimetoa taarifa
Peter Biaksangzuala (aliyezungushiwa duara kulia) amefariki dunia baada ya kuumia akishangilia bao
Biaksangzuala akikimbia kwenda kushangilia bao lake dhidi ya Chanmari West FC

EPL: HIKI NDO KILICHOIPATA MANCHESTER UNITED DHIDI YA WEST BROM USIKU HUU

BROM, SESSEGNON 'ALIYETIWA MFUKONI' TAIFA AWATIA KIMOJA, SARE 2-2 BAO la dakika ya 87 la kiungo Daley Blind limeinusuru Manchester United kulala mbele ya West Brom Albion baada ya kupata sare ya 2-2 ugenini katika mchezo wa Ligi Kuu England usiku huu. Blind alifunga bao zuri kutoka umbali wa mita 23, likiwa bao lake la kwanza tangu ajiunge na Mashetani hao Wekundu msimu huu. Stephane Sessegnon aliyeshindwa kufurukuta mbele ya Tanzania, Taifa Stars akiichezea Benin ikifungwa 4-1 katika mchezo wa kirafiki Oktoba 12 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, leo aliifungia WBA bao la kwanza dakika ya nane akimalizia krosi ya Andre Wisdom. Marouane Fellaini aliyetokea benchi dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Ander Herrera, aliisawazishia Manchester United dakika ya 48 akimalizia pasi ya Angel di Maria. Mzaliwa wa Burundi, Saido Berahino akaifungia bao lililoelekea kuwa la ushindia West Brom dakika ya 66 akimalizia pasi ya Chris Brunt, kabla ya Blind ‘kuchomoa’ dakika za lala salama. Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Rafael, Jones, Rojo, Shaw, Blind, Herrera/Fellaini dk46, Januzaj, Mata/Falcao dk72, Di Maria/Ashley Young dk76, Van Persie West Brom: Myhill, Wisdom, Lescott, Dawson, Pocognoli, Gardner, Brunt, Morrison, Dorrans, Sessegnon/Youssuf Mulumbu dk86 na Berahino.

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MSANII DAVIDO ALIVYOKUA AKIONDOKA TANZANIA!

Msanii Kutoka Nigeria, Adedeji Adelek maarufu kama ‘Davido' Ameweza kuwashukuru Watanzania kwa mapokezi waliyompatia pia pamoja na kushare jukwaa moja na Msanii kutoka Marekani T.I amesema hayo kupitia ukurasa wa Istragram pindi alivyokuwa anaondoka nchini Tanzania.
"Kwa heri Tanzania 26464! it was great sharing the stage with trouble man 31...thank you Clouds fm for napkin it possible and bless my brother @diamondplatnumz for welcoming me well" Aliandika DavidoLicha ya kwamba Aliweza kupikwa Mikwara na baadhi ya Vyombo vya Habari vya hapa nchi kuziiwa kufanya show hiyo.

Monday, October 20, 2014

BAADA YA KUFANYIWA KITU MBAYA KATIKA FIESTA 2014 DIAMOND PLATINUM AHAMUA KUWANYAMAZISHA WANAFKI KWA NJIA HII

Ommy Dimpoz atoboa siri ya picha anayoonekana akishuka kwenye treni ‘tusiamini kila tukionacho mtandaoni’

Baada ya kusambaa kwa picha ya Ommy Dimpoz anayoonekana akiwa kama kijana wa kijijini aliyetua mjini Dar es Salaam na watu wengi kuhisi ni picha yake ya zamani aliyopigwa wakati anatua Dar (kitu ambacho si kweli), ameamua kuelezea hisia zake. Akiweka picha nyingine kwenye Instagram lakini awamu hii akiwa na Vanessa Mdee (ambayo inaonesha kuwa ni moja ya kazi zake zitakazokuja), Ommy amesema amejifunza mengi kutokana na jinsi watu walivyoiongelea picha hiyo.
Ommy na Vanessa Mdee “Wiki iliyopita nimejifunza mambo mengi sana baada ya ile picha niliyodandia treni kusambaa kwenye mitandao kuna watu waliongelea km utani,kuna watu walinikebehi,wengine waliweka kwenye mitandao na kunitusi kabisa,”ameandika Ommy. “Ila nilichogundua Sio kila tunachokiona kwenye mitandao kina ukweli tujaribu kuwa wachunguzi,tuache mambo ya kucopy na kupaste jambo la mwisho kabisa siri ya Maisha anaijua mungu usimdharau mtu kwa muonekano unayemuona mshamba eti amekukuta mjini kesho ndo huyo huyo atakayekupa ajira tupendane tusidharauliane……Asante @vanessamdee kwa kupokea na fuko langu.”

TEAM DIAMOND YAZUNGUMZIA SUALA LA KUZOMEWA KWA DIAMOND KWENYE FIESTA

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amesema haoni kama wameathirika na kundi la watu waliomzomea msanii huyo wakati akitumbuiza Jumamosi hii kwenye show ya Serengeti Fiesta, Leaders Club jijini Dar es Salaam. Tale amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa walikuwa na taarifa kuhusu mpango huo hata kabla ya show na hivyo walijiandaa. “Tulikuwa tumemjenga kisaikolojia, kwahiyo hiyo ni sehemu ya kazi na mashabiki ingekuwa wanapiga kelele kama tumekosea show kweli, lakini sio hivyo. Show ilikuwa sawa,” amesema Tale. “Tunachojua sisi msanii wetu anafanya vizuri na sasa hivi nguvu zetu tumeelekeza katika tuzo. Wananchi wakaze kumpigia kula katika tuzo Channel O na MTV, sie sasa hivi tunasonga mbele, tunachojua chema chajiuza, kibaya chajitembeza.”

DOWNLOAD NGOMA MPYA YA MOMUSIC ~SIMAMA

MILIONI 58 ZAFUTA BAO TATU ZA WAZI SIMBA

MATAJIRI wa Simba wamefurahishwa na matokeo ya suluhu waliyopata dhidi ya Yanga na kusema bila kambi yao ya nchini Afrika Kusini wangeweza kufungwa si chini ya mabao 3-0 na Yanga. Kabla ya matokeo hayo ya juzi Jumamosi pale Uwanja wa Taifa, Simba ilikuwa Afrika Kusini ambako iliweka kambi ya siku nane kujiandaa na mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao ulimalizika suluhu. Akizungumza na Mwanaspoti, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji ‘KD’, alisema kikosi chao kilikuwa katika hali mbaya ya kuweza kupoteza vibaya mechi dhidi ya Yanga na wasingefanya jitihada hizo wangejikuta wanapata kipigo cha aibu. Dewji ambaye ndiye aliyekuwa mmoja wa waratibu wa kambi hiyo, alisema Yanga kabla ya mchezo huo walikuwa katika morali nzuri kuliko Simba. Alisema kambi na gharama mbalimbali walizoziingia zimewagharimu zaidi ya Dola 350,000 ambazo ni sawa na Sh58 milioni. “Hatukuwa katika hali nzuri, tulilazimika kutumia akili hiyo ya haraka kuinusuru klabu kupata kipigo cha aibu maana tuliangalia timu yetu kulinganisha na Yanga na kubaini endapo tusingeandaa ile kambi tungeweza kupata kipigo cha aibu cha si chini ya bao 3-0,”alisema Dewji. Matokeo hayo yamewakera mabosi wa Yanga waliokuwa wanataka ushindi kuziba kelele za Simba huku wachezaji kilio chao ni kukosa Sh80 milioni walizoahidiwa endapo wangeshinda huku Simba nao wakikosa Sh100 milioni ambazo wangepewa kama wangeishinda Yanga. “Tulipambana sana hasa sisi mabeki, lakini tatizo lilikuwa mbele katika umaliziaji tu, tulikuwa tunalala na fedha uongozi ulituletea Sh80 milioni taslimu na ukatuhoji nani akabidhiwe lakini ndiyo hivyo tumechemsha,” alisema kwa huzuni beki mmoja wa Yanga.

CRD:Mwanaspoti

HILI NI PIGO LINGINE KUBWA LILILOIPATA TASNIA YA FILAMU TANZANIA MCHANA WA LEO

Mdogo wa aliyekuwa muigizaji na muongozaji wa filamu marehemu George Otieno ‘Tyson’ aitwaye Benson Okumu Otieno 'Benii' enzi za uhai wake.

Mdogo wa aliyekuwa muigizaji na muongozaji wa filamu marehemu George Otieno ‘Tyson’ aitwaye Benson Okumu Otieno 'Benii' amefariki dunia ghafla katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar mchana leo. Msiba upo Sinza Vatican

Benii alikuwa muigizaji na muongozaji wa filamu mbalimbali nchini. Mipango ya mazishi ya kumpeleka kwao Kenya
GPL

HESHIMA: WEMA SEPETU APIGWA BAO NA FLORA MVUNGI NA MUMEWE H.BABA!

HESHIMA! Wanandoa, muigizaji Flora Mvungi ‘H.Mama’ na mwanamuziki Hamis Ramadhan ‘H.Baba’ wamemfunika mwigizaji Wema Sepetu kwa kupanga ghorofa. Mjengo wa wanandoa, muigizaji Flora Mvungi ‘H.Mama’ na mwanamuziki Hamis Ramadhan ‘H.Baba’ Akizungumzia mjengo huo walioupanga maeneo ya Mbezi-Jogoo, jijini Dar, H. Mama alisema yeye na mume wake wameamua kupanga nyumba hiyo si kwa sababu ya kumfunika mtu bali wanapenda kuwa huru na kuishi vizuri.
Flora Mvungi ‘H.Mama’ akiwa ndani ya mjengo hup na familia yake. “Hatushindani na mtu katika maisha yetu bali cha msingi tunaangalia nafsi zetu zinataka nini, kuhusu gharama yake, niache kidogo,” alisema Flora.Wema amepanga nyumba ya kawaida maeneo ya Kijitonyama jijini Dar.

BAADA YA MAMBO KUMFIKA SHINGONI: MISS TZ 2014 AKIMBILIA KANISANI

Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu aliopotangazwa mshindi. Ziba masikio, fanya yako! Wakati watu wakichonga juu ya sakata la madai ya kuwa na mtoto na utata juu ya umri wake, Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu anadaiwa kukimbilia kanisani. Habari za uhakika zilidai kwamba, baada ya kutwaa taji hilo hivi karibuni na kuibua sintofahamu, mrembo huyo alikimbilia kwenye Kanisa la Ufunuo kwa Nabii Yaspi Bendera lilipo Yombo-Buza jijini Dar kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha ndoto yake ya kuwa Miss Tanzania. Ilidaiwa kwamba, Sitti ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Temeke kwa leseni ya CCM, Abbas Zuberi Mtemvu, akiongozana na mama yake, walikwenda kwenye kanisa hilo kwa ajili ya kutoa shukrani kwa wema aliomtendea Mungu. “Watu wanaendelea kumsema mtoto wa mwenzao huku yeye anamshukuru Mungu kwa sababu hata kabla hajatwaa taji hilo alikuwa akisali hapa hivyo Mungu amepokea maombi yake na si vinginevyo kama watu wanavyomsimanga,” alisema muumini mmoja wa kanisa hilo.

 BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI 

OMMY DIMPOZ: ASANTE VANESSA MDEE KWA KUNIPOKEA FUKO LANGU

Baada ya kusambaa kwa picha ya Ommy Dimpoz anayoonekana akiwa kama kijana wa kijijini aliyetua mjini Dar es Salaam na watu wengi kuhisi ni picha yake ya zamani aliyopigwa wakati anatua Dar (kitu ambacho si kweli), ameamua kuelezea hisia zake.Akiweka picha nyingine kwenye Instagram lakini awamu hii akiwa na Vanessa Mdee (ambayo inaonesha kuwa ni moja ya kazi zake zitakazokuja), Ommy amesema amejifunza mengi kutokana na jinsi watu walivyoiongelea picha hiyo.

 BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI 

ALICHOFANYIWA DIAMOND FIESTA…NIMEAMINI MAISHA BILA UNAFKI HAYAENDI

Nakumbuka miaka mitano iliyopita aliyekuwa nguli wa filamu Nchini Tanzania marehemu “”Steven Kanumba”” alienda kwenye jumba la Big Brother….

amini usiamini bila sababu yyte ya maana watanzania ndo walikuwa wa kwanza kuanza kumsema kuwa hajui kuvaa, nani alimchagua , hajui kiingereza mpaka kufikia kumuigiza!!! Walisahau hata watu maruufu kama Messi na wengine wengi hawajui kuongea kabisa lugha hiyo..

Baada ya kifo chake watanzania hawahawa wakaanza kusema alikuwa nguli aliyetuwakilisha vizuri nje ya nchi na kulia sana!!!kumbe wakati akiwa hai tulikuwa tunamshusha chini..

Miaka mitano baadae Tanzania imempata mtu anayeiwakilisha vizuri nje ya mipaka na kuitangaza vizuri nchi yake..

Pasipokuwa na sababu za msingi (chuki binafsi tu)anapangiwa njama za kuzomewa na kuabishwa katika ardhi ya nchi yake ambayo kwa namna moja au nyingine kuna watu wameifahamu sababu yake!! Ukiuliza sababu za wengi wao kumchukia ni mafanikio yake lakini hata kama humpendi mtu hivi ndo hadi umzomee kwa kiasi kile !!!

leo na kesho naye huyu akitoka utaskia hawahawa waliokuwa wanamzomea wanaanza kusema jamaa alikuwa anatuwakilisha vizuri sana , ametutangaza sana kimataifa!! lakini Watanzania wenzake ndio vinara wa kumuangusha..

Si lazima kila mtu ampende Diamond ila kutumia nguvu kubwa sana kumuangusha mtu ni ishara ya uwoga na Roho ya kimaskini…

Nimeamini “”maisha bila unafki hayaendi”

UONGOZI MZIMA WA MDADISIBLOG UNAMTAKIA HAPPY BIRTHDAY MR BOB MAU

happy birhday my super frend Mr Bob Mau kwa kutimiza miaka kadhaa

MASTAA WOTE WABONGO KWANINI MSIIGE MFANO WA HUYU

Kutoka nianze kufuatilia akaunt mbalimbali za masuper staa wabongo sijawahi kumwona staa yeyoyte anayemsifia mpenzi wake au hata mume au mke zaidi ya floramvungi . Naomba mastaa wengine waige mfano wa huyu dada

BAADA YA VIPIGO MFULULIZO NDANDA FC YAAMUA KUFANYA FUKUZA FUKUZA

UGENINI SHINYANGA. Ndanda FC imemfuta kazi kocha wake, Denis Kitambi. Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa ndanda zinaeleza kuwa, uongozi wa klabu hiyo umechukua uamuzi huo baada ya vipigo viwili dhidi ya Mtibwa Sugar na kile cha nyumbani jana dhidi ya Ruvu Shooting. Taarifa nyingine zimeeleza kuwa Kocha wa Makipa, Mohammed Mwarami 'Shilton' naye ametimuliwa pia. Imeelezwa kumekuwa na kikao cha dharura leo asubuhi na viongozi wamefikia uamuzi huo. Juhudi za kuwapata viongozi wa Ndanda FC zimekuwa zikikwama kutokana na viongozi hao kutopokea simu. Lakini mchezaji mmoja wa Ndanda FC amelithibitisha hilo. “Tumeambiwa kuwa wamemtimua kocha, ila bado viongozi hawajafika kutueleza,” alisema.

HII NI KWA MASHABIKI WA CHELSEA! HIKI NDO KITU KINACHOENDELEA KUHUSU DIEGO COSTA

MSHAMBULIAJI Diego Costa ataukosa mchezo wa Jumanne wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, timu yake Chelsea ikimenyana na NK Maribor Uwanja wa Stamford Bridge, amesema kocha Jose Mourinho. Costa alikuwa nje ya kikosi cha Chelsea jana kikishinda 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika Ligi Kuu ya England na ataendelea kupata tiba kwa muda. Mpachika mabao huyo wa zamani wa Atletico Madrid aliumia akiichezea timu yake ya taifa Hispania na Mourinho amesikitishwa mno na kumkosa nyota wake huyo mkali wa mabao. Diego Costa atakosekana Chelsea ikicheza Ligi ya Mabingwa Ulaya keshokutwa "Baada ya mechi na Arsenal akaenda timu ya taifa, akacheza mechi mbili kubwa na amerudi akiwa na hali ambayo hawezi kucheza,"amesema Mourinho. "Nafikiri atakuwa katika hali nzuri katikati ya Novemba kurejea katika timu ya taifa. Tutakuwa makini mno juu yake. Atacheza kwangu atakapokuwa huru baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa,"amesema.

BAADA YA SARE YAO, HIKI NDICHO KILICHO MBELE YAO SIMBA NA YANGA, MWAKA HUU KAZI IPO!

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MIAMBA ya soka Tanzania, Simba na Yanga iligawana pointi Jumamosi baada ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sare hiyo inaifanya Simba SC itimize pointi nne baada ya awali kutoa sare tatu pia, wakati Yanga SC inafikisha pointi saba baada ya mechi nne, ikiwa nyuma ya Azam FC na Mtibwa Sugar zenye pointi 10 kila moja kileleni mwa Ligi.
Pamoja na kushinda 2-1 mara mbili dhidi ya Prisons na JKT Ruvu, lakini Yanga SC ilikutana na upinzani mkali na matokeo yangeweza kuwa kinyume kama si bahati yao.

RATIBA RAUNDI MBILI ZIJAZO LIGI KJUU BARA
Oktoba 25, 2014
Stand United Vs Yanga SC
Ndanda FC Vs Mgambo JKT
Kagera Sugar Vs Coastal Union
Azam Fc Vs  JKT Ruvu
Prisons Vs Simba SC
Ruvu Shoot Vs Polisi Moro
Oktoba 26, 2014
Mbeya City Vs Mtibwa Sugar
Novemba 1, 2014
Kagera Sugar Vs Yanga SC
Coastal Union  Vs Ruvu Shooting
JKT Ruvu Vs Polisi Morogoro
Ndanda FC Vs Azam FC
Stand United Vs Prisons
Mtibwa Sugar Vs Simba SC
Novemba 2, 2014
Mgambo JKT Vs Mbeya City
Yanga SC sasa watasafiri hadi Shinyanga kuwafuata Stand United waliopanda Ligi Kuu msimu huu, mchezo utakaofanyika Jumamosi Uwanja wa Kambarage.
Stand imeonyesha ni timu imara ikifanikiwa kuvuna pointi tano katika mechi za ugenini, kutokana na sare mbili dhidi ya Simba SC na Kagera Sugar na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Mgambo.
Stand ilipoteza mchezo wa kwanza nyumbani kwa kufungwa 4-1 na Ndanda FC ya Mtwara iliyopanda pia Ligi Kuu msimu huu, lakini baada ya hapo imecheza mechi tatu ugenini bila kufungwa.
Pata picha Yanga SC wanakwenda kukutana na upinzani wa aina gani katika mchezo huo Jumamosi.
Simba SC sasa. Watacheza na Prisons ya Mbeya Jumamosi Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Prisons ilionyesha upinzani ikifungwa na Yanga SC 2-1 na pia ilishinda ugenini 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya kutoa sare ya 0-0 na Azam FC Mbeya.
Jana, Prisons wamefungwa 2-1 na JKT Ruvu Mbeya na baada ya mchezo huo, kocha Juma Mwambusi akasema amekubali matokeo na anaelekeza nguvu zake katika mchezo ujao.
Simba SC ambayo haijashinda mechi msimu huu kwa kutoa sare nne, unafikiri inakabiliwa na mechi ya aina gani mwishoni mwa wiki?  

Sunday, October 19, 2014

TAZAMA PICHA ZA HARUSI YA MSANII HUSSEIN MACHOZI

DIVA WA CLOUDS AFUNGUKA MAZITO KUHUSU MAHUSIANO YAKE YA KIMAPENZI!

Diva Loveness wa Clouds Fm Kwa Mara Nyingine Amemuongelea Mpenzi Aliye nae Kwa Sasa Grazy GK Kupitia Blog yake, na Haya Ndio aliyoyasema: “The secret life to My happiness is the love of My life.. i believe that Love is the Greatest Gift life can give you, nilipo separate na hao waliopita thought i’d never love again but you can’t rule your heart, My bae is sucha great Person and incredibly loyal , he is the only man who seduced me with not only his charm but also his intelligence , he is matured positive and optimistic , very Passionate . we always on dinner for two with flowers ,table settings and the conversation always Brilliant and lovely….. you know when we started dating i had a feeling that i wasn’t a good enough person for him and normally that feeling wuld have made me want to leave but this time i couldn’t because i was too much in love with him, and its not about the money or fame but amma grown up sitaki mtu anieleze nani ananifaa nani type yangu nani niwe nae. i just go wit My territory. setting up my own rules in life. nishakuwa na hao wenye vyeo, pesa, majina but sikuwa na Amani. and Yol know that I am at Peace and am so Happy nilipo , am just with the Person i love most and there is no better feeling than that, couldn’t ask for more , i always put joyous smile on my face , My baby is like An Angel , the plan kati yangu na yeye was to be happy and creating some nice memories , we’ve been in tears and laughter, #PerfectMoment.❤️��