UGENINI SHINYANGA.
Ndanda FC imemfuta kazi kocha wake, Denis
Kitambi.
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa ndanda
zinaeleza kuwa, uongozi wa klabu hiyo
umechukua uamuzi huo baada ya vipigo
viwili dhidi ya Mtibwa Sugar na kile cha
nyumbani jana dhidi ya Ruvu Shooting.
Taarifa nyingine zimeeleza kuwa Kocha wa
Makipa, Mohammed Mwarami 'Shilton' naye
ametimuliwa pia.
Imeelezwa kumekuwa na kikao cha dharura
leo asubuhi na viongozi wamefikia uamuzi
huo.
Juhudi za kuwapata viongozi wa Ndanda FC
zimekuwa zikikwama kutokana na viongozi
hao kutopokea simu.
Lakini mchezaji mmoja wa Ndanda FC
amelithibitisha hilo.
“Tumeambiwa kuwa wamemtimua kocha, ila
bado viongozi hawajafika kutueleza,” alisema. |
0 comments:
Post a Comment