MSHAMBULIAJI Diego Costa ataukosa
mchezo wa Jumanne wa Ligi ya Mabingwa
Ulaya, timu yake Chelsea ikimenyana na NK
Maribor Uwanja wa Stamford Bridge,
amesema kocha Jose Mourinho.
Costa alikuwa nje ya kikosi cha Chelsea jana
kikishinda 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika
Ligi Kuu ya England na ataendelea kupata
tiba kwa muda.
Mpachika mabao huyo wa zamani wa
Atletico Madrid aliumia akiichezea timu yake
ya taifa Hispania na Mourinho
amesikitishwa mno na kumkosa nyota wake
huyo mkali wa mabao.
Diego Costa atakosekana Chelsea ikicheza
Ligi ya Mabingwa Ulaya keshokutwa
"Baada ya mechi na Arsenal akaenda timu
ya taifa, akacheza mechi mbili kubwa na
amerudi akiwa na hali ambayo hawezi
kucheza,"amesema Mourinho.
"Nafikiri atakuwa katika hali nzuri katikati ya
Novemba kurejea katika timu ya taifa.
Tutakuwa makini mno juu yake. Atacheza
kwangu atakapokuwa huru baada ya
kumaliza majukumu ya timu ya
taifa,"amesema. |
0 comments:
Post a Comment