Sunday, September 14, 2014

FABREGAS AWEKA REKODI MPYA YA HATARI, NDIYE MFALME WA PASI ZA MABAO ENGLAND DAIMA MILELE

KIUNGO wa Chelsea Cesc Fabregas ameweka historia katika Ligi Kuu ya England baada ya kuibuka mchezaji wa kwanza kutoa pasi za mabao katika mechi sita mfululizo. Huo ni mwendelezo wa tangu akiwa Arsenal, ambako alitoa pasi za mabao katika mechi zake mbili kubwa za mwisho kabla ya kuondoka The Gunners kurejea Barcelona mwaka 2011. Fabregas amevunja rekodi kwa pasi mbili za mabao kwa Diego Costa kwenye ushindi wa The Blues wa 4-2 dhidi ya Swansea ambao unawaweka kileleni mwa Ligi Kuu England. Pia alimsetia Costa mabao aliyofunga dhidi ya Everton na Hazard dhidi ya Leicester akithibitisha kocha wa Chelsea Jose Mourinho hakukosea kumnunua. Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alinza na moto wake katika urejeo wake England akiseti mabao ya Andre Schurrle na Branislav Ivanovic katika wiki ya kwanza ya msimu na Burnley. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, baada ya kung'ara Arsenal sasa anafanya vita pia Magharibi mwa London. Fabregas alimsetia Robin van Persie kufunga wakifungwa na Bolton baada ya kutoka kumsetia Theo Walcott na van Persie katika sare ya 3-3 na wapinzani wao wa Kaskazini mwa London, Spurs. Kabla ya mechi na Swans, Fabregas alikuwa miongoni mwa wachezaji sita waliotoa pasi za mabao katika mechi tano mfululizo walizocheza Ligi Kuu ya England. Lakini shujaa huyo mpya wa Chelsea, sasa anawapiku Darren Anderton, Gianfranco Zola, Ryan Giggs, Thierry Henry na Antonio Valencia kwenye chati ya vinara wa kutoa pasi za mabao.

Posted via Blogaway

Friday, September 12, 2014

HILI NI PIGO LINGINE KUBWA WALILOPATA MAN UNITED

PIGO lingine katika safu ya ulinzi ya Manchester United, baada ya Phil Jones kuumia akiichezea England dhidi ya Uswisi Jumatatu mechi ya kuwania tiketi ya Euro 2016 na sasa atatakiwa kuw anje kwa wikihadi tatu. Beki huyo wa Manchester United amekuwa chini ya uangalizi wa timu ya madaktari ya klabu tangu amerejea kutoka Basle, ambako alicheza kwa dakika 77 kabla ya kumpisha Phil Jagielka. Kulikuwa kuna wasiwasi kwamba Jones anaweza kuwa nje kwa mwezi mmoja, lakini vipimo vimeonyesha anaweza kuwa nje kwa wiki mbili hadi tatu. Jones wazi sasa atakosa mechi za Manchester United dhidi ya QPR Uwanja wa Old Trafford Jumapili ambako wachezaji wanne wapya wanawexa kuanza kuitumikia klabu hiyo. Radamel Falcao na Daley Blind walitambulishwa jana kama wachezaji wapya wa klabu hiyo na wanaweza kuungana na wenzao wengine wapya, Luke Shaw na Marcos Rojo. Kocha Louis van Gaal bado anasotea ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu England, baada ya mwanzo mbaya ambao imeshuhudiwa akiambulia pointi mbili tu huku akitolewa na timu ndogo MK Dons katika Kombe la Ligi, maarufu Capital One Cup.

Posted via Blogaway

Kumbe wimbo wa Walalahoi wa Izzo B unafanana na wimbo huu wa nje..

Inawezekana ni kufanana kwa melody au namna ya uimbaji ambayo hufanya mahadhi ya wimbo mmoja kwenda mwingine kufanana,miongoni mwa nyimbo zilizotajwa kuwa za mfumo huo ni wimbo wa Izzo B. Izzo B wimbo wake ambao kaupa jina la Walala Hoi inasemekana unafanana na wimbo wa Migo na Drake unaoitwa Versace,

Posted via Blogaway

HIKI NDO KITUKO KIKALI ALICHOANZANACHO BALOLETEL AKIWA LIVERPOOL

Huu kweli mcharuko; Mshambuliaji Mario Balotelli jana aliteremsha bukta yake namna hii mazoezini Melwood akiwa na timu yake Liverpool. Huu ni mfululizo wa vituko vya mshambuliaji huyo.

Posted via Blogaway

ARSENAL NAMNA HII NI MARA YA KWANZA TANGU 2005

Wachezaji wapya Sanchez na Welbeck wakiwa na kiungo mwenyeji kikosini Jack Wilshere (katikati) wakati wa upigaji picha
Wachezaji 31 wa kikosi cha Arsene Wenger wakiwa na mataji yao kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2005
Wachezaji wapya wa Arsenal, Mathieu Debuchy, Calum Chambers, David Ospina, Danny Welbeck na Alexis Sanchez

KLABU ya Arsenal imepiga picha ya kikosi chake kizima kipya wachezaji wakiwa na Kombe kwa mara ya kwanza tangu mwaka
2005, The Gunners wakiwa wamepozi na mataji ya FA na Ngao ya Jamii.
Picha hiyo inahusisha wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu, sambamba na makinda waliopandishwa kutoka timu ya
vijana.
Danny Welbeck, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka Manchester United katika siku ya
mwisho ya kufungwa kwa pazia la usajili amesimama katikati ya wachezaji wenzake wapya Calum Chambers na beki kinda wa
pembeni Hector Bellerin mstari wa pili,wakati Alexis Sanchez ni mchezaji pekee mpya aliyekaa mstari wa mbele.


Posted via Blogaway

SIJUI NI BANGI AU NI NINI??? CHEKI JUSTIN BIEBER ALIVYOVUA NGUO LIVE AKIWA JUKWAANI

Mwimbaji Justin Bieber amejitoa ufahamu wakati akiwa katika show ya mitindo iliyokuwa ikirushwa Live kwenye TV, Jumanne, September 9 na kuchojoa nguo mbele ya kadamnasi.Bieber alifika jukwaani ambapo watuwengi walihudhuria, na alipofika alimwambia Lara Stone kuwa hajisikii huru hadi avue nguo zote.Sekunde chache baadae alianza kuvua nguo moja moja hadi alipobakina nguo ya ndani pekee aka boxer.Show iliendelea na Bieber alionesha mwili wake akiwa ndani ya vazi hilo la ndani tofauti na matarajio ya wengi na Lara Stone aliendelea naratiba kwa kumpandisha jukwaani Rita Ora

Posted via Blogaway

CHEKI KISA HIKI KILICHOTOKEA COCO BEACH, JAMAA AIBA GARI LA MAMA YAKE NA KUPATA NALO AJALI BAADA YA KUMPA DEMU WAKE

Imetokea Mitaa ya Coco Beach DARImetokea pande za COCO BEACH kuna JAMAA bana aliiba NDINGA kwa BI MKUBWA wake akaenda naloBEACH alipofika kwa mbwembwe akamkabidhi DEMU wake aendeshe kumbe DEMU hajui KUNYONGA banasi akalipandisha milimani kule kwa mwedo wa kasi akashindwa kufunga breki akaliangusha toka juu mlimani mpaka chini kwenye yale maporomoko.Kwa sasa DEMU yupo MUHIMBILI ICU kaumia vibaga sana na mchizi nae kavunjika MKONO wa kushoto sa sijui alikua anataka kulizuia NDINGA kwa mikono daaaah Mbwembwe hazifai.Bi mkubwa alipovutiwa waya alifika fasta eneo la tukio na alipoliona NDINGA lake lipo kwenye hali ya UCHAPATICHAPATI aliangua kilio kama kafiwa na mumewe.NB: Imewekwa kama ilivyotumwa. CREDIT:GONGMIX

Posted via Blogaway

Thursday, September 11, 2014

Jux azungumzia tetesi za kuhusu wimbo wake mpya ‘Sisikii’ kama amemuimbia Vanessa Mdee

Wednesday, September 10, 2014

Tambwe: Mmemleta Okwi ? mtakiona

KOCHA Patrick Phiri alipopata taarifa kuwamshambuliaji wao mpya Emmanuel Okwi ameruhusiwa kucheza Simba alishindwa kuzuia furaha yake na kutamka kuwa sasakazi imeanza rasmi.Straika namba moja wa Simba, Amissi Tambwe amefurahi kupita kiasi na kutamka kwamba: “Mmeniletea Okwi, mtaona kazi itakavyonoga.” Tambwe aliiambia Mwanaspoti kwamba: “Ni mchezaji mzuri ambaye ana kila sifa ya mshambuliaji kama tutashirikiana vizuri Simba itafika mbali sana na kila mtu atashangaa, tunajipanga kufanya kazi ya maana.”Tambwe alisema mchezaji huyo ni makini kutokana na aina yake ya uchezaji aliyoiona kuanzia siku za nyuma mpaka alipotua mazoezini Simba.Juzi Jumapili jioni Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake Richard Sinamtwa ilipitia mkataba wa mchezaji huyo na kusikiliza hoja za pande zote mbili Yanga na Okwi na kubaini kwamba mkataba kati ya pande hizo ulivunjika kwa kukiuka kipengele cha 8 kinachohusu malipo ya usajili.Mpaka sasa Yanga ilimlipa Okwi Dola 50,000 (Sh 80 milioni kwa wakati huo) ya usajili huo na hivyo ikawa inadaiwa Dola 50,000 kwa makubaliano ya usajili wa Dola 100,000 (Sh 160 milioni kwa wakati huo) jambo ambalo lilipelekea mchezaji huyo kugoma kuichezea Yanga kwa madai kuwa mpaka amaliziwe fedha zake.Phiri alikuwa akifuatilia kwa karibu juu ya utata wa usajili wa mshambuliaji wake huyo ambaye Yanga walipinga usajili wakeSimba kwa madai kuwa bado ana mkataba na timu hiyo, huku Phiri akieleza kwamba angependa kuona Okwi anaichezea Simba kuliko kukaa bila kucheza kwani kipaji chake kingekufa.“Nafurahi sana kusikia Okwi ni mchezaji huru nami nitakuwa huru kumtumia katikakikosi changu, kwa kweli nimejawa na furaha kubwa kwa hilo, Okwi ni mchezaji mzuri na anapendwa na mashabiki wa soka nchini.“Tunarudi Zanzibar ambako nitalazimika kukaa na wachezaji wangu kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ambayo naamini tutafanya vizuri, ila nitazungumza nao kuhusu umakini katika soka na kufanya juhudi katika ligi,” alisema Phiri.Okwi atangaza vitaOkwi aliiambia Mwanaspoti kwamba: “Nimefurahishwa na uamuzi huu wa TFF, nilijua kwamba kama wakizingatia ukweli na haki, nitawashinda Yanga na imekuwa hivyo, nawashukuru sana, sasa nataka kucheza mpira.”“Unajua nimepoteza muda mwingi katika kesi hizi mbalimbali, kwa mbali ni kama zilikuwa zinakimaliza kipaji changu sasa nataka kucheza mpira Simba, naomba watu waniache nicheze mpira nataka kurudi katika uwezo wangu,” alisisitiza Okwi.

HIKI NDO KITU KIPYA KABISA KINACHO MUHUSU BEKI MARCOS ROJO NA MAN UNITED KWA UJUMLA

BEKI mpya wa Manchester United, Marcos Rojo amerejea kutoka kwenye majukumu ya taifa lake, Argentina kujiandaa kuanza kuichezea klabu yake hiyo mpya dhidi ya QPR Jumapili. Rojo bado hajaichezea klabu yake hiyo mpya licha ya kusajiliwa wiki tatu zilizopita kutokana na kuchelewa kupata hati ya kufanyia kazi England. Aliiwakilisha nchi yake kwenye Kombe la Dunia na akacheza kwa dakika zote 90 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ujerumani, Argentina ikilipa kisasi cha kufungwa kwenye fainali ya Kombe la Dunia. Amerudi kazini: Rojo akiwasili katika hoteli anayoshi mjini Manchester baada ya kuwa na timu ya taifa ya Argentina Muargentina huyo anatarajiwa kuanza kuichezea United Jumapili katika Ligi Kuu ya England, baada ya suala lake la hati ya kufanyia kazi kupatiwa ufumbuzi. Ujio wa beki huyo ni faraja kwa Louis Van Gaal, ambaye timu yake ilionekana kuwa na tatizo katika safu ya ulinzi, kiasi cha kufanya vibaya kwenye mechi za mwanzoni. Safu ya ulinzi ya Mashetani hao Wekundu imeyumba baada ya kuondoka kwa mabeki wote wakongwe mwishoni mwa msimu, Patrice Evra, Nemanja Vidic na Rio Ferdinand.

UJUMBE WA BALOTELLI KWA WANAFUNZI WOTE DUNIANI, JAMAA KUMBE 'MCHARUKO' TU, LAKINI KICHWANI ZIMO

PAMOJA na kuonekana kama mchezaji mtukutu uwanjani, lakini Mario Baloteli ameonyesha ni mtu anayejali masuala ya elimu baada ya kuposti ujumbe mzuri wa kuwatakia kila la heri wanafunzi wakirejea shuleni wiki hii. Mshambuliaji huyo wa Liverpool ameandika kwenye akaunti yake ya Instagram ujumbe usemao: "Hi watoto, leo mnaanza shule kwenye nchi nyingi. Ni kama mwanzo wa msimu kwenye soka. Huo ni wakati wa kufanya vizuri ili kujenga mustakabali mzuri wa maisha yako. Kila la heri!' Ujumbe huo ameuambatanisha na video fupi, amnayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliyewahi kuchezea pia Manchester City, Inter Milan na AC Milan amesema: "Soma kwa vidii na chez a kwa bidii, nawatakia watoto wote kila la heri katika siku yako ya kwanza shule,".

HIVI NDO JINSI YANGA WALIVOTAKA KUMFANYA KITU MBAYA EMMANUEL OKWI

“Kwa niaba ya mteja wetu, Emmanuel Arnold Okwi, napenda kutoa maelezo kuhusu Uamuzi wa kihistoria katika soka la Tanzania ambao umefanywa na Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji ya TFF. Uamuzi huo ni wa kihistoria kwa misingi ifuatayo:
MOSI: Ni mara ya Kwanza katika historia ya soka la Tanzania ambapo Kamati inakaa kujadili haki ya mchezaji dhidi ya klabu kubwa na hatimaye kuamua kwa manufaa ya mchezaji, tena pasipo kupiga kura kwa misingi ya upenzi na unazi. Kamati ya Mwanasheria Mashuhuri na mwenye Msimamo Bw. Richard Sinamtwa iliamua kustafsiri kanuni kwa kufuata ushahidi uliopo na kwa haki kabisa pasipo kujiingiza katika mtego wa kupiga kura kama ambavyo tumekua tukiiona huko nyuma.

Emmanuel Okwi (kulia) akiichezea Yanga SC kabla hawajatibuana

PILI: Kamati ikiongozwa na Mwenyekiti ilitumia busara ya hali ya juu kwa kukataa ombi la Yanga la kutengua uteuzi wa Bw. Hans Pope katika Kamati hiyo. Ikumbukwe kuwa Yanga ilileta hoja ya kumkataa Bw. Hans Pope kwa misingi ya mgongano wa kimaslahi na kumtaka mwenyekiti atoe uamuzi juu ya suala hilo. Endapo mwenyekiti angetoa maamuzi ya kumuondoa Hans Pope, basi angejiingiza katika uvunjaji wa Katiba ya TFF kwasababu yeye sio mamlaka ya uteuzi wa Hans Pope katika Kamati hiyo. Mwenye mamlaka hayo ni Kamati ya Utendaji ya TFF. Hivyo Yanga walipaswa kuelewa hilo na si kuishinikiza kamati, hususan Mwenyekiti, amuondoe Hans Pope kwenye Kikao.
TATU: Maamuzi ya Kamati yamefungua njia kwa wachezaji wengi ambao mikataba yao inachezewa na vilabu kwa muda mrefu pasipo kuwa na nafuu yoyote ya kisheria kwa wachezaji hao ambao ndio nguzo ya muhimu katika mpira wa Tanzania. Hata hivi sasa kuna wachezaji ambao bado hawajalipwa stahili za mikataba yao ndani ya Yanga. Tunawaomba wajitokeze ili tuwasaidie wapate haki zao za kisheria kama ambavyo imetokea kwa Okwi.
NNE: Pamoja na madai ya Yanga ya kukata rufaa FIFA / CAS, naomba wajue kuwa haki yao ya kukata rufaa inatokana na ukweli kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF imetekeleza wajibu wake. Uamuzi huo wa Kamati umejenga msingi muhimu sana katika suala zima la kuheshimu na kutekeleza mikakaba kwa mujibu wa kanuni za FIFA. Endapo Yanga watakata rufaa kama wanavyodai, itakuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha nguzo ya kuheshimu mikataba ya wachezaji inapewa msisitizo unaostahili.

MGOGORO KATI YA YANGA NA OKWI
Mkataba wa Yanga na Okwi, ambao ulisainiwa tarehe 12 Disemba 2014 umekuwa na mapungufu yafuatayo:
1. Mkataba huo umempa majukumu mchezaji kufuatilia ITC na suala zima la yeye kupata vibali vya kucheza. Hii ni kinyume na Kanuni za FIFA ambao zinatamka bayana kuwa jukumu la kufuatilia ITC ni la wanachama wa FA, lakini Yanga walimtwisha Okwi zigo hilo. Okwi alitekeleza jukumu hilo.
Kamati ililiona hilo na kusema wazi kuwa hilo sio sahihi. Ni vema wachezaji wajue kuwa hilo sio jukumu lao.
2. Pili Yanga, kwa mujibu wa mkataba, walikuwa na haki ya kumkata mchezaji theluthi moja ya mshahara wake wa mwezi endapo atakosa mechi tatu au zaidi. Yanga walimkata Okwi Mishahara ya miezi mitano, kinyume na matakwa ya mkataba na pasipo maelelzo yoyote.
3. Yanga na Okwi walikubaliana kuwa mchezaji atalipwa ada ya kusaini mkataba (signing on – fee) ya US$ 100,000, kwa Awamu mbili. Awamu ya kwanza wakati wa kusaini mkataba na awamu ya pili tarehe 27 Januari 2014. Mpaka hivi sasa, Yanga wamelipa US$ 50,000 tu na bado kuna deni la US$ 50,000. Huu ni uvunjaji wa mkataba wa wazi kabisa.
4. Kipindi chote mchezaji akiwa na klabu ya Yanga, hajapewa nyumba kama ambayo walikubaliana. Huu ni ukiukwaji mwingine wa mkataba.
Baada ya Okwi kuanza kudai haki zake tajwa hapo juu, Yanga waliamua kutomlipa mteja wetu mishahara ya miezi mitano kinyume na matakwa ya mkataba kati yao.

MPANGO WA SIRI WA YANGA
Yanga walikuwa na mpango wa siri wa kuvunja mkataba na Emmanuel Okwi ili wamkomoe mteja wetu, ashindwe kucheza mpira, kiwango chake kiporomoke na itumike kama onyo kwa wachezaji wengine ambao wanadai haki zao. Mpango huu ulitekelezwe kama ifuatavyo:
a. Tarehe 27 Juni 2014, Yanga waliandika barua kwenda TFF, ikiitaka TFF, pamoja mambo mengine, itambue kuwa mkataba kati yao na Okwi umefutwa. Barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
b. Tarehe 25 Julai 2014, Yanga waliandika barua ya pili kukumbushia barua yao ya tarehe 27 Juni 2014. Barua hiyo ya pili haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
c. Tarehe 20 Agosti 2014 Yanga waliandika barua nyingine tena wakikumbushia hoja zao tajwa hapo juu. Kwa mara ya tatu, barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
d. Yanga waliandika barua nyingine ya nne tarehe 25 Agosti 2014 ikiwa na hoja zile zile za kusitisha mkataba na mteja wetu. Kwa mara ya nne barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
Baada ya TFF kupanga tarehe ya kikao cha Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji na kutoa barua ya wito tarehe 27 Agosti 2014 ndipo kwa mara ya kwanza mchezaji Emmanuel Okwi akafahamu kuwa Yanga wameomba kuvunja mkataba wake.
Tarehe 27 Agosti 2014, Emmanuel Okwi aliiandikia Yanga KUKUBALI ombi lao la kuvunja mkataba.

Mambo muhimu ya kujiuliza ni:
Mosi, Kama Mkataba ulikuwa ni kati ya Yanga na Okwi, ni kitu gani kiliifanya Yanga ishindwe kumpa angalau nakala ya barua nne ambazo ilizipeleka TFF?
Pili, Wakati Yanga wanaomba kuvunja mkataba, walikuwa wameshamlipa Okwi stahili zake kwa mujibu wa Mkataba huo?
Tatu, Je visingizio vya kuvunjwa kwa mkataba wa Okwi vina uhusiano na idadi ya majina ya wachezaji wa kigeni wa Yanga?
Ni bayana kuwa Yanga walitafuta kila aina ya kisingizio ili mteja wetu aonekane kuwa ndio amevunja mkataba wakati ni wazi kuwa Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kuvunja mkataba huo tarehe 27 Januari 2014 kwa kushindwa kumlipa mteja wetu US$ 50,000 za ada ya kusaini mkataba.

HOJA MBELE YA KAMATI
Mbele ya Kamati Yanga walileta hoja kuwa: Hans Pope ana mgongano wa maslahi kwa kuwa amemsajili Okwi Simba na yeye ni mjumbe wa Kamati hii; Okwi amekataa kuongeza au kupunguza mkataba kama ilivyopendekezwa na Yanga; Okwi ameleta madai yasiyo na msingi ya kutaka apewe nyumba ya kuishi; hajacheza mechi 6 hivyo kuikosesha Yanga ubingwa. Okwi amefanya makubaliano na Klabu ya Wadi Geldi ya Misri wakati ana mkataba na Yanga. Hivyo basi Yanga waliitaka Kamati itamke kuwa mkataba kati yao na Okwi umesitishwa, imfungie Okwi kucheza mpira Tanzania Maisha na ailipe Yanga dola za kimarekani laki mbili.
Tukimwakilisha Okwi, tulitoa hoja kuwa: Mteja wetu amekubali ombi la Yanga la kuvunja mkataba ambalo limo katika barua zake nne; Yanga ndio wamevunja mkataba kwa kushindwa kulipa signing fee US$ 50,000; Mishahara ya miezi mitano US$ 15,000 na kodi ya nyumba US$ 2,800. Madai hayo ni kwa mujibu wa mkataba.
Baada ya Maswali toka kwa Kamati kwa pande zote mbili, Yanga waliomba kufuta barua zao, ombi ambalo lilitupiliwa mbali na kamati.
Kamati, hatimaye ilifanya maamuzi ya kihistoria katika kulinda haki za kimkataba za wachezaji kama ambayo imeelezwa hapo juu. Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu, anapaswa kuipongeza kwa dhati kamati kwa maamuzi ambayo wanajenga mpira wa nchi hii. Vilabu vinapaswa kufahamu kuwa haki za mchezaji lazima ziheshimiwe.
Hoja za Yanga kuwa hakukuwa na madai ya fedha sio sahihi kwasababu Majibu toka kwa Okwi na mabishano ya maneno mbele ya kamati hiyo ilijadili kwa kina madai ya fedha ya Okwi na hata Yanga walikiri kutolipa madai hayo. Hivyo basi si sahihi kusema kuwa eti suala la madai ya fedha halikujadiliwa. (ona kiambatisho MNA1)
Msingi wa malalamiko ya Yanga ni barua ya tarehe 27 Juni 2014, ambayo hakuna sehemu ambayo inatamka suala la Simba. Kama kuna kesi dhidi ya Simba, wasubiri wakati wa kupitia pingamizi za usajili lakini suala ambalo Yanga walilalamikia ni kusitisha mkataba na Okwi na madai ya fidia.
Kamati ya Sheria na Mwenyekiti wake hawana mamlaka ya kujadili uteuzi au uwepo wa Hans Pope kwenye kikao hicho. Mamlaka ya Uteuzi ndio, kwa mujibu wa katiba ya TFF, yenye uwezo wa kutoa uamuzi kuhusu suala hilo.
Kwakuwa rufaa ni haki ya kila mtu, Uamuzi wa kukata rufaa Fifa / CAS ni haki ya kisheria lakini tuwakumbushe Yanga kuwa “UKITAKA HAKI, TENDA HAKI KWANZA”.
“Imeandikwa na Dk. Damas Daniel Ndumnbaro (PhD) wa kampuni ya Maleta & Ndumbaro Advocates, ambao ni Mawakili wa Mchezaji Emmanuel Okwi”

LULU MICHAEL KWA PICHA HII AINGIA KATIKA LIST YA MASTAA MALIMBUKENI WANAPOPATA PESA

Kumezuka katabia Kwa Wasanii Mastaa Kuonesha Pesa zao Kwenye Mitandao ya Kijamii Kama Facebook na Instagram wanapozipata kwa Mkupuo , Lulu Michael nae ameingia katika list ya wasanii hao, Juzi Kapost picha hiyo Hapo Juu akionesha zigo laPesa...Je ni Sawa kwa staa kama LuluKufanya Hivyo au ni Ulimbukeni wa Pesa?

Tuesday, September 09, 2014

OKWI AWAJIBU MASHABIKI WA YANGA KISTAHILI HII

STRAIKA wa Simba, Emmanuel Okwi, anajiamini kupita kiasi na akawaambia mashabiki wa Yanga, waendelee kumzomea hivyo hivyo, kwani kelele zao zinaingilia kulia na kutokea kushoto na mwisho wa siku watampenda tu.Okwi raia wa Uganda, ana utata na Yanga ambayo ana mkataba nayo lakini ameukana mkataba huo na kusaini Simba kutokana na sababu mbalimbali ambapo juzi Jumamosi aliichezea kwa mara kwanza klabu hiyo ya Msimbazi kwenye mechi ya kirafiki waliyoifunga Gor Mahia mabao 3-0.Katika mchezo huo, Okwi alipata tabu kutoka kwa mashabiki wa Yanga ambao kila alipogusa mpira walikuwa wanamzomea jambo ambalo limeelezwa na wadau wengi wa soka kuwa litamfanya ashindwe kucheza mpira.Lakini alipozungumza na Mwanaspoti, Okwi alisema: “Hiyo zomea zomea yao, watazomea sana lakini kamwe hawataweza kunifanya nishindwe kuchezampira.“Mimi ni mchezaji mkubwa, najielewa, hicho wanachikifanya ni kujisumbua tu, nitacheza na kupiga mabao kama kawaidana wakibisha wataona.”Beki wa Yanga, Mbuyu Twite, ambaye awali alikuwa kwenye rada ya Simba aliwahi kukumbana na zomea zomea ya Simba waliokuwa wakimkejeli kwa kumuita mwizi kwa madai kwamba alichukua fedha zao za usajili akaingia mitini.Tofauti na Twite ambaye alikuwa akiwajibu kwa ishara mbalimbali akiwa uwanjani, Okwi alifanya jambo dogo sana ambapo kila alipokuwa akiitwa jina hilo alikuwa akiwanyooshea dole mashabiki wa Simba ambao walijibu kwa kumshangilia kwa nguvu jambo lililoleta raha.Kocha Mkuu wa Simba Patrick Phiri amefurahishwa na uwezo ulioonyeshwa na Okwi lakini akampa jukumu moja kubwa ambalo anatakiwa kulikamilisha mapema ili aweze kutisha.“Namjua Emmanuel (Okwi) ni kijana mzuri, lakini amenifurahisha sana na uwezo aliouonyesha amecheza vizuri kwa kiasi chake lakini bado ananafasi ya kufanya vizuri zaidi,” alisema Phiri.“Bado hayupo sawa sana, lakini hilo lipo mikononi mwake. Kuhakikisha anajituma zaidi mazoezini, anaweza kuwa sawa zaidiendapo atajituma kufanya mazoezi ya nguvu.“Kama akifanikiwa hilo atarudi katika uwezo na kuweza kuisaidia Simba.” source mwanaspoti

Baada ya Okwi kuidhinishwa Simba, hiki ndio walichoamua Yanga

Siku moja baada ya shirikisho la sokanchini TFF kumtangaza mchezaji Emmanuel Okwi kuwa huru na hivyo anaweza kusajiliwa na klabu ya Simba – leo hii uongozi wa klabu ya Yanga umeitisha mkutano wa waandishi wa habari na kuzungumza juu ya uamuzi wa keshi yao dhidi ya Okwi.Uongozi wa Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru.Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo.Mapande amesema kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.Alisema kuwa cha kushangaza, kamati hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao wameshangazwa nayo.“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakinicha kushangaza maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande.Alisema kuwa mazingira yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajilila Okwi limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama utaratibu ulivyo,” alisema.Alisema kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mwenyekiti wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa kimaslah

LULU ADAIWA KUWA NA UBABE NA KISIRANI CHA KUTODUMU NA MWANAUME, TAJIRI WA MADINI ASALIMU AMRI.

New gossip zinasema kuwa star wa filamu nchini aliyejaaliwa mvuto pia Lulu Elizabeth Michael hadumu na mwanaume sababu ya kuendekeza ubabe na kutaka kum-control mwanaume anayekuwa nae.Inadaiwa Lulu hataki mchezo mwanaume akishakuwa nae basi lazima ahakikishe hafurukuti. Inadaiwa kuwa hivi miezi ya karibuni alikuwa na jamaa mmoja mdogo kimapenzi akamwaga na baada ya muda akawa anatoka na tajiri mmojakijana wa madin toka Arusha lakini tajiri huyo alinyoosha mikono juu baada ya Lulu kama kawaida kuruhusu majeshi yake yam-control jamaa huyo. Chanzo kimoja kikizungumza naSanikilisema "\"Ni mtu mwenye isirani kwa wanaume, hadumu nao, wengie wanaokuwau nae ni wale wavumilivusana, nadhani ana matatizo ambayo yanahitaji mtaalam wa saikolijia ya mahusiano, akizinguliwa tu hachelewi kuvnja simu na kurejesha kila kitu alichokuwa amepewa" kilisema chanzo hicho kilichodai ni mshikaji wa karibu na Lulu.

MSANII WA BONGO MOVIE AUMBUKA BAADA YA PICHA ZAKE ZA UTUPU KUVUJA MITANDAONI.....AMTUPIA LAWAMA NAY WA MITEGO

Msanii wa Bongo Movies, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ aliyewahi kuripotiwa kujiachia kimahaba na mwanamuziki Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’ ametia aibu kubwa baada ya picha zake za utupu kuzagaa mitandaoni. Kutokana na picha hizo ambazo zimeonekana kuzagaa katika mitandao mbalimbali na kuacha viulizo kwa wasanii wengi wanaomfahamu, mwandishi wetu alimtafuta Bozi ambaye alionekana kutafunatafuna maneno na kumtupia lawama nzito Nay wa Mitego ambaye aliwahi kumtumia picha hizo walipokuwa wapenzi. alisema msanii huyo. “Mungu wangu sijui nitaweka wapi sura yangu, nilishtuka sana baada ya kuona picha hizo ni aibu kubwa kwangu, nashindwa hata kuelewa zimesambaa vipi maana hizi picha alikuwa nazo Nay, nilimtumia kabla hatujaachana sasa hata yeye namuuliza anasema hajazisambaza

WEMA ATOA MANENO YA KEJELI KWA KAJALA, SOMA ALICHOKISEMA HAPA

Ngoma nzito kauli ya sexy lady wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kuwa yupo tayari kumtumikia msanii mwenzake Kajala Masanja ‘K’ kwenye kampuni yake ya KAY Entertiment tena bila malipo yoyote, imetafisiriwa kuwa ni kejeli. NGOMA nzito! Sexy lady wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ Hivi karibuni Wema alikaririwa akisema: “Nakubali kwamba Kajala anaweza kuwa na maisha mazuri ya kiasi hicho na akanifanya mfanyakazi wake katika kamusi yake kwa sababu sioni cha kumfanya ashindwe kuwa hivyo, naamini anaweza kuniajiri na wala sina kipingamizi! hahahaa!” Msanii wa Bongo Movie Kajala Masanja ‘K’. Baada ya kauli hiyo ya Wema, mashabiki wake waliikataa kwa maelezo kuwa alilenga kumkejeli Kajala ambaye awali aliwahi kumwajiri kwenye kampuni yake ya Endless Fame Production.

WEMA ATOA MANENO YA KEJELI KWA KAJALA, SOMA ALICHOKISEMA HAPA

Ngoma nzito kauli ya sexy lady wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kuwa yupo tayari kumtumikia msanii mwenzake Kajala Masanja ‘K’ kwenye kampuni yake ya KAY Entertiment tena bila malipo yoyote, imetafisiriwa kuwa ni kejeli. NGOMA nzito! Sexy lady wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ Hivi karibuni Wema alikaririwa akisema: “Nakubali kwamba Kajala anaweza kuwa na maisha mazuri ya kiasi hicho na akanifanya mfanyakazi wake katika kamusi yake kwa sababu sioni cha kumfanya ashindwe kuwa hivyo, naamini anaweza kuniajiri na wala sina kipingamizi! hahahaa!” Msanii wa Bongo Movie Kajala Masanja ‘K’. Baada ya kauli hiyo ya Wema, mashabiki wake waliikataa kwa maelezo kuwa alilenga kumkejeli Kajala ambaye awali aliwahi kumwajiri kwenye kampuni yake ya Endless Fame Production.

Friday, September 05, 2014

MWANAFUNZI WA KIKE WA SHULE YA MSINGI AKAMATWA AKIIBA NDANI YA DALADALA JIJINI DAR

Waandishi wa ahabari nao wahakuwa nyuma kufuatilia sakata hilo.
Maofisa Usalama wakimpeleka mtoto huyo kituo cha Polisi ili kuweza kupata maelezo zaidi na kusubiri wazazi wake waende kumtoa.

DAR Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. Leo mapema asubuhi tulikutana na kituko cha mtoto ambaye ukiangalia unaweza kukuta anaumri wa miaka 12 alikamatwa akimwibia abiria katika daladala na baadae alikamatwa na maofisa usalama wa Jeshi na kuanza kuhojiwa ndipo alipogundulika anamakosa mengi.

Mwanafunzi huyo wa kike wa Shule ya Msingi Upendo iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam aliyejulakana kwa jina la Irene alipoanza kupekuliwa na maofisa usalama ilionekana mara ya mwisho kuandika ilikuwa ni Aprili 15, 2014 tokea hapo hajaandika, kumbe huwa anawaaga wazazi anakwenda shule huku akiishia Posta jijini Dar es Salaama akilanda landa na mpaka leo alipodakwa.

Katika mahojiano mafupi yaliyofanywa na maofisa hao, ilibainika kuwa mtoto huyo amekuwa na utoro uliokidhiri jambo ambalo hata alipopigiwa mwalimu mkuu wa shule yao ya msingi anaposoma alikiri hilo na kuongeza kuwa mtoto huyo amekuwa akikataa shule kwa muda mrefu pamoja na kupewa taarifa kwa wazazi wao hawakulifuatilia.


Posted via Blogaway