Friday, September 12, 2014
 |
PIGO lingine katika safu ya ulinzi ya
Manchester United, baada ya Phil Jones
kuumia akiichezea England dhidi ya Uswisi
Jumatatu mechi ya kuwania tiketi ya Euro
2016 na sasa atatakiwa kuw anje kwa wikihadi
tatu.
Beki huyo wa Manchester United amekuwa
chini ya uangalizi wa timu ya madaktari ya
klabu tangu amerejea kutoka Basle, ambako
alicheza kwa dakika 77 kabla ya kumpisha Phil
Jagielka.
Kulikuwa kuna wasiwasi kwamba Jones
anaweza kuwa nje kwa mwezi mmoja, lakini
vipimo vimeonyesha anaweza kuwa nje kwa
wiki mbili hadi tatu.
Jones wazi sasa atakosa mechi za Manchester
United dhidi ya QPR Uwanja wa Old Trafford
Jumapili ambako wachezaji wanne wapya
wanawexa kuanza kuitumikia klabu hiyo.
Radamel Falcao na Daley Blind
walitambulishwa jana kama wachezaji wapya
wa klabu hiyo na wanaweza kuungana na
wenzao wengine wapya, Luke Shaw na Marcos
Rojo.
Kocha Louis van Gaal bado anasotea ushindi
wa kwanza katika Ligi Kuu England, baada ya
mwanzo mbaya ambao imeshuhudiwa
akiambulia pointi mbili tu huku akitolewa na
timu ndogo MK Dons katika Kombe la Ligi,
maarufu Capital One Cup. |

Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment