Wednesday, September 10, 2014
 |
BEKI mpya wa Manchester United,
Marcos Rojo amerejea kutoka
kwenye majukumu ya taifa lake,
Argentina kujiandaa kuanza
kuichezea klabu yake hiyo mpya
dhidi ya QPR Jumapili.
Rojo bado hajaichezea klabu yake
hiyo mpya licha ya kusajiliwa wiki
tatu zilizopita kutokana na
kuchelewa kupata hati ya kufanyia
kazi England.
Aliiwakilisha nchi yake kwenye
Kombe la Dunia na akacheza kwa
dakika zote 90 katika mchezo wa
kirafiki dhidi ya Ujerumani,
Argentina ikilipa kisasi cha
kufungwa kwenye fainali ya
Kombe la Dunia.
Amerudi kazini: Rojo akiwasili
katika hoteli anayoshi mjini
Manchester baada ya kuwa na
timu ya taifa ya Argentina
Muargentina huyo anatarajiwa
kuanza kuichezea United Jumapili
katika Ligi Kuu ya England, baada
ya suala lake la hati ya kufanyia
kazi kupatiwa ufumbuzi.
Ujio wa beki huyo ni faraja kwa
Louis Van Gaal, ambaye timu yake
ilionekana kuwa na tatizo katika
safu ya ulinzi, kiasi cha kufanya
vibaya kwenye mechi za
mwanzoni.
Safu ya ulinzi ya Mashetani hao
Wekundu imeyumba baada ya
kuondoka kwa mabeki wote
wakongwe mwishoni mwa msimu,
Patrice Evra, Nemanja Vidic na Rio
Ferdinand. |
0 comments:
Post a Comment