Wednesday, September 10, 2014
 |
PAMOJA na kuonekana kama
mchezaji mtukutu uwanjani, lakini
Mario Baloteli ameonyesha ni mtu
anayejali masuala ya elimu baada
ya kuposti ujumbe mzuri wa
kuwatakia kila la heri wanafunzi
wakirejea shuleni wiki hii.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool
ameandika kwenye akaunti yake
ya Instagram ujumbe usemao: "Hi
watoto, leo mnaanza shule
kwenye nchi nyingi. Ni kama
mwanzo wa msimu kwenye soka.
Huo ni wakati wa kufanya vizuri ili
kujenga mustakabali mzuri wa
maisha yako. Kila la heri!'
Ujumbe huo ameuambatanisha na
video fupi, amnayo mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 24
aliyewahi kuchezea pia
Manchester City, Inter Milan na AC
Milan amesema: "Soma kwa vidii
na chez a kwa bidii, nawatakia
watoto wote kila la heri katika siku
yako ya kwanza shule,". |
0 comments:
Post a Comment