Sunday, September 14, 2014
 |
KIUNGO wa Chelsea Cesc Fabregas ameweka
historia katika Ligi Kuu ya England baada ya
kuibuka mchezaji wa kwanza kutoa pasi za
mabao katika mechi sita mfululizo.
Huo ni mwendelezo wa tangu akiwa Arsenal,
ambako alitoa pasi za mabao katika mechi
zake mbili kubwa za mwisho kabla ya
kuondoka The Gunners kurejea Barcelona
mwaka 2011.
Fabregas amevunja rekodi kwa pasi mbili za
mabao kwa Diego Costa kwenye ushindi wa
The Blues wa 4-2 dhidi ya Swansea ambao
unawaweka kileleni mwa Ligi Kuu England.
Pia alimsetia Costa mabao aliyofunga dhidi
ya Everton na Hazard dhidi ya Leicester
akithibitisha kocha wa Chelsea Jose
Mourinho hakukosea kumnunua.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania
alinza na moto wake katika urejeo wake
England akiseti mabao ya Andre Schurrle na
Branislav Ivanovic katika wiki ya kwanza ya
msimu na Burnley.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27,
baada ya kung'ara Arsenal sasa
anafanya vita pia Magharibi mwa London.
Fabregas alimsetia Robin van Persie kufunga
wakifungwa na Bolton baada ya kutoka
kumsetia Theo Walcott na van Persie katika
sare ya 3-3 na wapinzani wao wa Kaskazini
mwa London, Spurs.
Kabla ya mechi na Swans, Fabregas alikuwa
miongoni mwa wachezaji sita waliotoa pasi
za mabao katika mechi tano mfululizo
walizocheza Ligi Kuu ya England.
Lakini shujaa huyo mpya wa Chelsea, sasa
anawapiku Darren Anderton, Gianfranco
Zola, Ryan Giggs, Thierry Henry na Antonio
Valencia kwenye chati ya vinara wa kutoa
pasi za mabao. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment